Tuesday, August 9, 2016

MWONEKANO MPYA WA KAPULYA WENU... WA MWAFRIKA HALISI KABISA...


Hapa sijui mapozi au ndo furaha 
Baada ya kuangalia sana nikaona nywele zangu si nyeusi si isipokuwa zimepata ugeni ...angalia tu utaona :-) Unajua nini nimependa sana hiyo na naahidi sitamfukuza mgeni huyo kwani kuna wengine wanamtafuta ...Ila duh sijui nitaweza kuchana kila siku maana ni kipilipili/ulezi hasa

9 comments:

Ester Ulaya said...

UMEKUWA MWAFRICA HALISI DADA

ray njau said...

Hujambo Yasinta binti Ngonyani?

Yasinta Ngonyani said...

Ester mdogo wangu....ahsante.Ila ni mwafrika halisi tangia...nilijificha tu labda.
Kaka Ray! Mie sijambo.

Anonymous said...

Hujambo da Yasinta? Umependeza kweli kweli. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Ka'Salumu...kitambo hujaonekana mie sijambo. Ahsante kwa mtazamo wako...

NN Mhango said...

Mimi najua siku zote u mwafrika. Sema uko orijino kabisa. Je hiyo ving'aravyo ni mvi au macho yangu?
Kwa ujumla umetokelezea na kupendeza dada.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango! Ahsante. Macho yako yapo sahihi kabisa ni muvi. Ahsante tena-:)

emu three said...

Hongera, ndugu yangu, ukiona hivyo ujue ule umri wa hekima zaidi umeingia. Enzi hizo wewe unapewa mamlaka na heshima kwenye vikao, lkn huku bongo, kwa hivi sasa ukianza kufikia huo umri unaanza kuogopa...ila nikuambie kitu, Utu uzima dawa. Tupo pamoja

Yasinta Ngonyani said...

emu thtree! Ahsante...Unajua ni juzi tu ilikutana na mdada mmoja akaniangalia sana kiasi kwamba nikajisikia aibu...nikashindwa kuvumilia kama nilivyo na ukapulya wangu nikamuuliza kulikoni....akasema una mvi lakini unaonekana u msichana mdogo sana ...nilicheka sana...Nawe ndugu yangu unasema ingekuwa enzi hizo ningepewa mamlaka na heshima kwenye vikao...Kaaazi kwelikweli...Pamoja daima.