Wednesday, August 17, 2016

KUMBUKUMBU :- LEO NI MIAKA KUMI NA MBILI (12) KAMILI TANGU MAMA YETU MPENDWA ALANA NGONYANI ATUTOKE!!

KUZALIWA 2/10/1952-KUFA 17/8/2004
Mama ni miaka kumi na mbili  sasa tangu ututoke. Umetuacha na majonzi pia maumivu moyoni mwetu. Tunaukumbuka sana uwepo wako, tukiamini Mungu angekuacha japo kwa miaka michache. Midomo yetu haiwezi kuelezea jinsi tulivyokupenda. Lakini Mwenyezi Mungu anajua ni jinsi gani tulivyokupenda. Na jinsi gani tunakukumbuka, mapenzi yako, wema wako. Pia kama mama kwa mwongozo wako katika nyumba yetu, ambayo sasa ni upweke mtupu bila wewe.
Tunakukumbuka sana,  sisi wanafamilia wote pamoja na ndugu wote na pia marafiki. KIMWILI HAUPO NASI, BALI KIROHO UPO NASI DAIMA. MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI. AMINA!!!

2 comments:

Anonymous said...

Nani kama mama. Pepo ipo miguuni kwa mama.
ukikosa radhi ya mama umekosa pepo. RIP mama. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu!Ahsante sana kwa kuwa nasi katika maombi ya mama yetu Alana.