Wednesday, May 25, 2016

LEO TUTEMBELE MOROGORO MJI KASORO BAHARI NA MILIMA YAKE....

Milima ya Uluguru ileeee...
Kilichonipendeza hii picha/taswira ni huu udongo mwenkundu pia shamba la mahindi...nimekumbuka mbali sana

Hapa tunaona milima ya Uluguru na shamba la katani....Najua wengi wetu tunakumbuka historia ya mashamba ya katani...

3 comments:

ray njau said...

China na Tanzania zinavyoendeleza kwa pamoja kilimo cha mkonge
Katika miaka ya hivi karibuni, zao la mkonge limekuwa linavutia uwekezaji wa vitega uchumi vya nchi mbalimbali duniani. Ikiwa kampuni kubwa ya kilimo ya China, Kampuni kuu ya mashamba ya China inajitahidi kuendeleza kilimo cha mkonge nchini Tanzania, na kupata mafanikio mazuri.

Tanzania ni nchi iliyopo katika sehemu ya joto. Kutokana na hali ya hewa inayofaa, katani ya nchi hiyo ni maarufu sana ulimwenguni, na Tanzania inasifiwa kuwa ni, "Mfalme wa zao la mkonge". Mashamba maarufu ya katani ya mkoa wa Morogoro yako umbali wa kilomita 300 kutoka magharibi ya Dar es-Salaam, mji mkuu wa Tanzania. Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari alitembelea mashamba mawili ya Kampuni kuu ya mashamba ya China nchini Tanzania kwenye sehemu hiyo.

Kampuni ya mashamba ya China nchini Tanzania ilianzishwa mwezi Februali, mwaka 1999, ambapo ilinunua mashamba ya Rudewa na Kisangata mwezi Februari, mwaka 2000. Maeneo ya mashamba hayo yanafikia hekta 5900.

Baada ya jitihada za zaidi ya miaka 3, kazi ya Kampuni ya mashamba ya China ilipata mafanikio mazuri, na kujulikana sana katika sehemu hiyo. Waziri mkuu wa Tanzania Frederick Sumaye aliongoza maofisa wa serikali kuyatembelea mashamba hayo tarehe 15, mwezi Februali, mwaka 2003. Baada ya kuuliza kwa makini habari zinazohusika, Bw. Sumaye alisifu sana mafanikio yaliyopatikana katika mashamba hayo, pia alisema anatumai Tanzania itapata uzoefu mzuri wa China, na kuimarisha ushirikiano huo na China.

Majani ya mkonge wa Tanzania yana urefu wa mita 1. Kwa wastani, mkonge unaweza kuishi miaka 13 hadi 14, ambapo idadi ya majani yake yanaweza kufikia 200 hadi 300 katika maisha yake. Majani hayo yanaweza kutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali, kama vile: kamba nene, magunia na mazuria. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, bidhaa za mkonge zinaweza kutumika katika nyanja mbalimbali za mitambo, mawasiliano, mafuta, usafiri baharini, misitu na kilimo. Kutokana na hayo, soko la kimataifa lina mahitaji makubwa ya mkonge. Wakati huo huo, mahitaji ya mkonge kwa China yanaongezeka kwa asilimia 20 kila mwaka. Wakati mkonge ulipozalishwa kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania, uzalishaji wake uliweza kufikia tani laki 2.3, na thamani yake ya bidhaa nje ilichukua theluthi kwa thamani ya jumla ya bidhaa nje za kilimo nchini Tanzania, na kiasi hicho kilichukua robo ya soko la monge la kimataifa. Lakini kutokana na ukosefu wa fedha, na tatizo la usimamizi, pamoja na kukabiliwa na ushindani mkubwa wa bidhaa za nailoni, kilimo cha mkonge nchini Tanzania kiliathirika sana. Hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 20, uzalishaji wake wa mkonge haukufikia tani elfu 20. Lakini, baada ya kuingia katika miaka ya 90 ya karne ya 20, bei ya mkonge kwenye katika soko la kimataifa ilianza kupanda, na mahitaji kwa bidhaa za mkonge yalizidi kuongezeka. Uzalishaji wa mkonge ulianza kuwa kazi yenye mustakabala mzuri.

Kutokana na hali hiyo, Tanzania iliamua kuvutia uwekezaji wavitega uchumi kutoka nchi za nje, ili kuendeleza kwa pamoja kilimo cha mkonge, ambapo Kampuni kuu ya mashamba ya China ilichukua fursa hiyo nzuri, kununua mashamba yenye maeneo ya hekta 5,900, na kufufua kilimo cha mkonge nchini humo. Hadi kufikia mwezi Desemba, mwaka jana, maeneo ya mashamba ya mkonge ya Kampuni ya mashamba ya China nchini Tanzania yalifikia hekta 1000, na itajitahidi kutimiza lengo lake la kufanya maeneo hayo kufikia hekta 1500 ifikapo mwaka 2005. Mashamba ya Rudewa na Kisangata yalikuwa sehemu maarufu ya mkonge nchini Tanzania. Hivi sasa mkonge za Rudewa bado unajulikana sana katika soko la Ulaya. Lakini kutokana na usimamizi mbaya, shamba hilo lilibadilika kupanda mazao mengine, kama vile mahindi, alizeti, mbono, maharagwe na tumbaku.
(Habari kwa hisani ya CRI)

ray njau said...

Mwandishi wa habari alikutana na meneja mkuu wa Kampuni kuu ya mashamba ya China nchini Tanzania Bw. Jia Qingquan. Alisisimka sana akikumbuka jinsi uanzishaji na uendelezaji wa mashamba hayo ya mkonge. Alisema, mwanzoni mashamba hayo yalikuwa hayakulimwa kwa miaka 20. Ili kufanya shamba hilo liweze kupandwa mkonge, wataalamu 5 wa China waliwaongoza wafanyakazi zaidi ya 60 wa kienyeji, wakagawanyika katika vikundi viwili na kufanya kazi mashambani. Baada ya jitihada za nusu-mwaka, walirudisha ardhi yenye maeneo ya hekta 166 katika hali nzuri kabla ya majira ya masika kuwadia, na kuanza kupanda mkonge. Tangu mashamba hayo ya mkonge kufufuliwa kuanzishwa mwaka 2000, kutokana na jitihada kubwa za wataalamu wa China, watanzania waliondoa wasiwasi wao juu ya kazi hiyo.

Akizungumzia mavuno yatakayopatikana, meneja Jia alisisimika sana. Alimwongoza mwandishi wetu wa habari kuingia katika shamba la mkonge wenye urefu wa mita 1.7, akisema kuwa, hivi sasa, kwa wastani urefu wa majani ya mkonge huo yanaweza kufikia zaidi ya mita 1, ambapo inaweza kuzalisha nyuzi za mkonge zenye urefu wa 90 c.m. Hivi sasa bei ya nyuzi za mkonge inazidi dola za kimarekani 900 kwa tani katika soko la kimataifa, hivyo faida ni kubwa sana.

Meneja Jia ana matumaini kuwa, kilimo cha mkonge itapata mafanikio makubwa zaidi kwa jitihada za pamoja za China na Tanzania.
(Habari kwa hisani ya CRI)

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa hiyo habari ndugu Njau ama kweli Elimu kuelimishana. Bonge la historia fupi ya Mkonge/katani