Tuesday, March 1, 2016

NI MWEZI MPYA, SIKU MPYA YA JUMANNE NA JIKONI LEO ILIKUWA HIVI:-.....

 Nilianza kwa kuandaa saladi ya karoti- ambayo ilikuwa na karoti 3-4, nusu kitunguu maji, mbegu za maboga zilizokaushwa vijiko viwili vya mezani, vijiko viwili vya mezani mafuta upendayo chumvi kidogo na pilipili manga kidogo pia limau kwa mbali.  Unaweza kula kama ilivyo au mkate kidogo lakini mimi/sisi tuliamua....
... sahani iwe hivi samaki, njegere, viazi vya kuponda  na hiyo saladi ya karoti ikawepo. Na kuteremshia ni gilasi ya maji. .....KARIBUNI TUJUMUIKE.....

8 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Wow yummy! Natamani ningekuwapo nikazikamua hizo njegere hata kama ni za kuvundikwa kwenye jokofu kwa muda mrefu!

Yasinta Ngonyani said...

Hahaaa...kaka Mhango...nilijua utakuwa wa kwanza kusema kwa jinsi upendavyo njegere...karibu

Anonymous said...

Hongera kwa mapishi mazuri, yaani nimebakia kula kwa macho tu duh siku ingine nipostie cha kwangu mana kinaonekana kuwa kitamu sana sana. Hiyo kachumbari ya karoti nimeipenda sana ntajaribu kuitengeneza ila sasa kupata mbegu za maboga zilizokaushwa ndo mtihani kwa huku Tz, au nifanyaje? nishauri hapo......! vinginevyo nisipoweka hayo mafuta je? na badala ya liamua au ndimu nikaweka apple cider vinegar itakuwaje? Nia ni kutengeneza kama yako kila kitu.Asante.

Anonymous said...

Mie ni anonimas wa hapo juu nimesahau kuuliza carrot umezigrate au umekata kata na kisu au machine kipaba? yaani sitaki kupata sifuri kwenye hilo zoezi la majaribio ntakayotengeneza hivyo naulizia kila kitu kabisa ili kiwe sawa na chako. Halafu nishauri kuhusu mbegu za maboga huku kupata za unga duh ni mtihani? Naomba unipe ujanja kwa hapo. halafu nimeona mayonnaise au kwa mbali kwenye sahani karibu na mashed potatoes.....

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina...nimefurahi kwa jinsi ulivyotamani hiyo saladi/kachumbali ya karoti. Ni hivi hizo mbegu za maboga kama huna basi unaweza kutumia mbegu za alizeti na mafuta ya olive oil pia apple cider vinegar. Kuhusu vipi nimekata karoti..hapana ni kwamba nimekuna. Lakini pia unaweza kukata na kisu kama una uvumilivu...na haya sio mayonnaise ni crem/yoghourt nimechanganya na chumvi na sukari kwa mbaliii

emuthree said...

tupo pamoja

Yasinta Ngonyani said...

Eehhhh! ndugu wa mimi emuthree nimekukumbuka mno baada ya kukusoma hapa. Karibu tujumuike. Pamoja daima!

Anonymous said...

Asante sana Dada kwa maelekezo mazuri, nitajaribu na kukupa mrejesho.