Wednesday, March 16, 2016

PALE MTU UNAPOTAMANI MATUNDA UYAPENDAYO LAKINI BEI NAYO INAKOMOA MPAKA HAMU INAKWISHA

Ni juzi tu nilikuwa dukani kapata mahitaji kama kawaida binadamu lazima ale/tule..Nikafika kwenye matunda nikakutana na matunda ya kila aina mojawapo lilikuwa tunda la  EMBE,  nikapata hamu LAKINI KUJA KUANGALIA BEI NIKANYWEA...EMBE MOJA NI Tsh. 4868...mmmhhh nikakumbuka nyumbani jinsi miti ya miembe ilivyozunguka nyumba nikaacha.....nikaendelea na matunda mengine.......
 Nikakutana na karakara (Passion) nikaangalia weee nikapumua kwa hiyo bei tena ...Tsh. 1696 kwa karakara (passion) moja nikaanza kukumbuka.....
Kazi ya mikono yangu...mikarakara yangu(mapassion)

........karakara (passion) zangu nilizonayo nyumbani Ruhuwiko-Songea. Ambazo ni freshi kabisa yaani kutoka tu nje na kuchuma. Nakwambia nusu nilie:-(  Ebu angalia  hapa...basi nikaamua kufanya ubahili. Yaani sikununua nimepata hasira  ya kuanza kuongeza kupanda miche ya mikarakara (mipassio/mipasheni) zaidi... Nguja niache  niwaachie na wengine wasema...panapo majaliwa wapendwa.

2 comments:

Anonymous said...

Dada yangu siungenua tu! hujaaacha ubahili? haya itabidi ule ya kwenye miti ya ruhuwiko......ya kikweli kweli supermarket umayaacha shauri ya bei kubwa, ila ndio matumiziya pesa hayo. Au ndio mambo ya budget ulaya? hongera kwa kuwa na mashamba ya matunda ruhuwiko. karibu sana Tz.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina wa 5:03 kwanza nasema ahsante. Pia kutonunua hayo matunda kuna sababu nyingi sio ubahili tu. kwanza huwezi kujua unachonunua ni kizima au kimeoza kwa bai hiyo..pila hakuna cha BUDGET...