Thursday, April 9, 2015

WANAUME NA SIFA

Mwanaume siku zote anauawa na sifa, anauawa na kutaka kwake mwanamke  amuone kwamba yenye ndiye mwanaume bora kabisa na asiyeshindwa na jambo. Kwa hali hiyo, adui yake namba moja ni kukosolewa. Siyo kwamba mwanamke anapokosolewa hafurahi, hapana, lakini haimpi shida na haichukulii kama jambo kubwa kama inavyotokea kwa mwanamume. Mwanamke anapokosoa mwanamume anakuwa hajui kwamba mwenzake siyo kama yeye, kwamba kwa mwenzake kukossolewa ni kama kudungwa sindano ya sumu- anauawa kisaikolojia.
Ukweli ni kwamba,  ukienda kwenye ndoa ambazo  mume hukosolewa sana, tatizo la mume kama huyo kukosa nguvu za kushiriki tendo la ndoa ni la kawaida. Mwanamume anapokosolewa na mkewe huumia sana. Kuumia huku ambako hutokea kwenye mawazo ya kawaida na yale ya kina, humfanya mwanamume kuona kama vile amenyangánywa uanaume wake. Ndiyo maana  maumivu haya huendelea kuwepo hadi kitandani kwa sabababu mwanamumu huyu hufikia kuamini kwamba haba uanaume.
Kwa mwanamke, kwa sababu amekuwa akikosolewa tangu miaka miliono iliyopita na kutupiwa lawama hata pale ambapo kosa ni la mwanamume, kukosolewa na kukosoa kwa upande wake siyo jambo lenya kuweza kumpa mtu jazba. Lakini hivi sivyo ilivyo kwa mwanamume. Kwa bahati mbaya mwanamke hajui, anadhani anatarajia mwanamume kuwa kama yeye. Anapokosoa anadhani na kuamini kwamba atambadili mwanamume, wakati anaielekeza ndoa yake shimoni.
CHANZO:  Maisha na mafanikio na  MUNGA TEHENAN.

1 comment:

NN Mhango said...

Huu uchambuzi kuhusu wanaume una mapungufu mengi tu. Kwanza si kweli kuwa mwanaume anajiona hawezi kushindwa jambo. Pili si kweli kuwa kukosolewa kunaumiza vinginevyo anayekosolewa awe si mwelewa. Kimsingi, marehemu Munga alikuwa akiongea vitu ambavyo watu walitaka kusikia badala ya kuchimbua vilivyo. Hata hivyo, huwezi kumlaumu kutokana na kiwango chake cha elimu na ile hali ya kutaka kutumia uwanja huu kama njia ya kujipatia mkate bila kujali upotofu unaoweza kutokana na mjumlisho wake ambao kitaaluma ni jambo la mwisho msomi kufanya.