Monday, April 20, 2015

ASILI HAICHAGUI


Mwili wa mwanadam umeumbwa mfano wa kompyuta, kompyuta unapoinunua kuna programu ambazo unazikuta humo humo kwenye kompyuta na kuna programe zingine wewe mwenyewe unaweka, kompyuta yako itafanya kazi kutokana na idadi ya programe utakazoweka, ukiweka programu zenye faida kompyuta yako itakuwa yenye faida, ukiweka programu zisizokuwa na faisa ndio hivyo kompyuta yako itakuwa haina faida, lakini pia utendaji kazi wa kompyuta moja na kompyuta nyingine vinatofautiana kulingana na idadi ya programu zilizomo kwa mfano kompyuta ambayo ina micro soft word, ina adobe,power point, itaweza kuandika barua, kuedit picha, na kuandaa presentation.
Lakini kopyuta ambayo itakuwa na pungufu ya hizo program haitaweza kufanya kazi sawa na yenye hizo program, ndivyo na maisha ya yalivyo, unapozaliwa kuna program unazaliwa nayo (KIPAJI), na kila mtu anakipaji chake,lakini unapokuja huku duniani sasa program zingine unaweka mwenyewe.
Hapa ndipo utofauti wa maisha ya mtu mmoja na mtu mwingine unaanza kuonekana, ASILI HAICHAGUI hii inamaana kwamba chochote utakoweka kwenye akili yako lazima kitaonyesha maisha yako halisi, ukiweka mambo mabaya tu kwenye akili yako hayo ndio yatatokea kwenye maisha yako maana hiyo ndio program umeweka kwenye kompyuta yako, ukiweka uoga, uvivu, kushindwa wewe kila kitu huwezi, ndio hivyo utakuwa.
Watu wengi sana tunahangaika kuwa maisha magumu, maisha magumu lakini kiuhalisia sio kweli kuwa maisha ni magumu bali tunatumikia program tulizoweka kwenye kompyuta zetu, mfano kazi yako wewe ni kuangalia muvi masaa 12, kupiga story masaa mengi, kuchat facebook na watsap asubuhi hadi jioni, magazeti ya udaku,unafikiri ubongo wako utakuwa na uwezo gani,na utazalisha nini?
Uwezo wako utakuwa finyu kwasababu kwa asilimia kubwa unapokea mambo yasiyo na maana, lakini hebu angalia uwe unasoma vitabu, unahudhuria semina, unaangalia video za watu waliofanikiwa kiuhalisia hata kama ulikuwa hujawaza kufanikiwa utaona unaanza kupata mbinu za kufanikiwa,kwanini umeweka program ambayo sasa inaleta matunda.
Tatizo kubwa kwenye akili zetu kwa asilimia kubwa tumeweka program za kushindwa, uvivu, kutaka mafanikio ya haraka, uoga, kupoteza muda, na kufanya mambo yasio na maana matokeo yake ndio maisha tulio nayo.Nakumbuka wakati nimeamua kuanza kufanya biashara na Neptunus nilikuwa sijui chochote kuhusu biashara,kwasababu nilikuwa muajiriwa tu, nilikuwa sijui chochote kuhusu kusoma vitabu na nilikuwa nikisoma ukurasa mmoja tu nalala, lakini nilichogundua kuwa ASILI HAICHAGUI chochote nitakachoweka ndani yangu kitatumika, nikaanza kujifunza alhamdulillah nilipo sasa sipo nilipokuwa mwaka mmoja uliopita.kumbe vyoyote unavyotaka kuwa kwenye haya maisha unaweza kuwa kama ukiamua kubadilisha program ulizoweka au ulizowekewa kuwa wewe huwezi,
 
CHANZO :- IMETOLEWA NA BASSANGA MWALIMU WA UJASIRIAMALI.
 

2 comments: