Saturday, April 25, 2015

KARIBU:- KUNA USHIBE!!

Naanza bila mpango, Kwa tenzi pia na tungo,
Niyafumbue mafumbo, Ugali na mbogamboga.
Wanadharau mapishi, Wanayabeza mapishi,
Mapishi ya Waswahili, Ugali na mbogamboga.
Umeyasifu matango, Mazuri sana kwa macho,
Huleta ngozi nyororo, Ugali na mbogamboga.
Na uyoga asilia, Kushiba bila ya kula,
Nashiba na kutazama, Ugali na mbogamboga.
Ugali huo wa sembe, Sembe nyeupe pepepe,
Na dona usiutupe,Ugali na mbogamboga.
CHANZO : KWA MJENGWABLOG

8 comments:

Vimax Pills said...

hemm i like it

Meizitang Botanical said...

Nice blog

Anonymous said...

Msosi baba kubwa. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kwnaza napenda kwakaribisha Vimax na Meizing Botanical karibuni sana na ahsante kwa mchango wanu. Kaka Salum ni kwel:-)

NN Mhango said...

Hao vimax na meizitang si wa kukaribisha. Ni blog za kishenzi zinazodandia kwa wengine kutangaza utumbo wao uwe makini ili siku moja wasijeiteka blog yako.

Yasinta Ngonyani said...

Hee! kumbe Ahsante kwa TAARIFA KAKA MHANGO

ray njau said...

Dona,mchicha na samaki,usitaje!

obat cytotec said...
This comment has been removed by a blog administrator.