Ndugu wasomaji wa kibaraza hiki, leo nataka tujifunze namna ya kuomba maji kupitia lugha za makabila tofauti tofauti.Si mnajua jinsi maji yalivyo muhimu kwa sisi biadamu. Yaani pale unapokuwa na kiu sana na kuomba maji inabidi utumie lugha pekee ambayo unatakiwa kuwasiliana na lugha inayotumika haya ebu tuangalie baadhi ya hizi hapa chini ..Tuanze na KINGONI
Kingoni: Nimwomba manji ga kunywa/Nitangatilai manji mlongo wangu=Naomba maji ya kunywa/naomba maji ya kunywa ndugu yangu
Kihehe:Ndisuka Ululenga= Naomba maji ya kunywa
Kibena : Ninyilika/ninyilika Magasi= Naomba maji ya kunywa
Kimatengo: Naa masi kuunywa= Naomba maji ya kunywa
Kinyawezi:Nalilomba minze kakunwa=Naomba maji ya kunywa
Kichaga: Ngikundi Mringa= Naomba maji ya kunywa
Kichaga: Ngikundi Mringa= Naomba maji ya kunywa
Kipare: Nighenja mazi ya kunwa=Nisaidie maji ya kunywa
Kipogoro: Nyagu Mashi ga kulanda= Naomba maji ya kunywa
Kisukuma: Nalilomba Minzi agung´wa/Kifogo= Naomba maji ya kunywa
Kimanda: Nisuka Masi ga kunywa= Naomba maji ya kunywa
Kinyakyusa: Ngusumo amisi= Naomba maji ya kunywa
Kisimbiti: Ndasabha amanshe ghukunywa= Naomba maji ya kunywa
Kimasai:Njaaghe Ngare= Naomba maji ya kunywa
Kimeru:Ngitelewa Mringa= Naomba maji ya kunywa
Kijaluo:Miaa pi= Naomba maji ya kunywa
Kimeru:Ngitelewa Mringa= Naomba maji ya kunywa
Kijaluo:Miaa pi= Naomba maji ya kunywa
Kihaya: Ninshaba Amaizi= Naomba maji ya kunywa
Naona na wenzangu jazieni hapo maana Tanzania kuna makabila mengi sana .....Pamoja Daima!!
6 comments:
Kichaga: Ngikundi Mringa wonyo= Nataka maji ya kunywa
----------------------------------
Kichaga: Ngiterewa Mringa wonyo= Naomba maji ya kunywa
safi sana. Kweli Mnara wa Babel kiboko
kiarusha;NJOKI ENGARE NAWO=NIPE MAJI YA KUNYWA
Ninga mukha wena. Kimachame hicho. Doty
Jasiri haachi asili...................
Ndinyirika lulenga au ndisuha lulenga. Kibena
Post a Comment