Tuesday, June 24, 2014

KAKA S. ANAMPONGEZA MTOTO WAKE KWA KUPATA KOMONIO YA KWANZA

KILINDA SAMUEL MBOGO
Jumapili  22/6 Kijana Kilinda alipata komonio yake ya kwanza. Bahati mbaya sikupata nafasi kwenda kuhudhuria siku hii. Ila nimehudhuria kwa kuangalia picha kama muonavyo. Nimetumiwa picha nami nimeona niwashirikishe wenzangu maana baadhi yetu tunakumbuka sana siku hii...HONGERA SANA KILINDA SAMUEL MBONGO KWA  SIKU HII...HII NI ZAWADI YANGU KWAKO....SHANGAZI YAKO YASINTA a.k.a Kapulya/kadala.

3 comments:

KAKA CHE JIAH said...

HONGERA MWENETU MTUMIKIE MUNGU ENZI YA UTOTO WAKO NA HII IWE NI NGUZO YAKO KUU KULIKO ZOTE NA KUBWA KULIKO NI ILE ISEMAYO WAHESHIMU BABA YAKO NA MAMA YAKO UPATE HERI DUNIANI

HONGERAAAAAAAAA SANA BWANAAWEE UMEPENDEZA

BABA TAZAMA MWANAO NA MWANA TAZAMA BABA YAKO NADHANI NI MANENO MAZURI HAUSHANGAI ALISEMA NANI MUWE NA SIKU NJEMA DADA .TUNASHUKURU KUWEKA KIBARAZANI PICHA HII
SIKU NJEMA

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Che Jiah...Ahsante kwa kumpongeza mwanetu kwa siku hii.

SAm mbogo said...

Unajuwa wakati najaribu kumshawishi huyu jamaa(mwanangu) kuanza mafundisho ilikuwa kazi sana hatimaye tulifikia muhafaka.ila nachotaka kusema ni kwamba hawa watoto wetu hasa huyu wangu kwa malezi ya huku ulaya vitu vingi ama mambomengi nikujadiliana na kama hataki ni hataki unajikuta kama mzazi unatafuta njia ambayo hatakuletea matatizo. huku mtoto hapigwi,anahakizote mzazi inabidi umsikilize, amasivyo serikari itamchukuwa. ila nashkuru mikwaruzano yetu iliisha vizuri. pia sasante kaka che jiah kwamaneno mazuri kwa kijana, bila kumsahau shangazi mtu mgoni yasinta!!.kaka s