Tuesday, June 3, 2014

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MWANETU,KAKA, MJUKUU, RAFIKI YETU ERIK

HONGERA KUTIMIZA MIAKA 14 ERIK
Nachukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa nguvu sisi wazazi/walezi kwa kuweza kumlea mtoto/kijana Erik na leo ametimiza miaka kumi na nne/14. Hakika miaka inaenda  nikiwa kama mama naona kama ilikuwa juzi tu alizaliwa kijana huyu. Mwenyezi Mungu azidi kuwa naye katika masomo, na mengine yote afanyayo ili yawe mazuri. Ampe oyo wa upendo kwa walezi, ndugu jamaa na marafiki. Samahani nimeshindwa kupata picha yake yupo shule. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA ERIK!

8 comments:

Anonymous said...

Hongera sana Erick! Happy birthday Erick. Nakutakia maisha marefu yenye afya njema, amani, furaha, na upendo. Ombi langu ukirudi toka shule mama akupige picha atuwekee hapa ili tukuone siku hii ya leo ya kuzaliwa kwako.
Mungu awabariki wazazi wanaomlea, waalimu wake na pia jamii nzima.

Anonymous said...

Kwa niaba ya wanablog tunaomba sana kuona picha yako ya leo Erick. Mama ametuwekea huo mpira tukijuwa kuwa unapenda sana kucheza mpira. Ila itabidi tukuone tu kwa leo. Asante kukubali ombi Erick. Hapa napita pita nikutane na picha yako tu.

Ester Ulaya said...

Hongera sana kaka Erick kwakutimiza miaka 14 ya kuzaliwa. Hongereni wazazi kwa kumkuza kijana, twamuombea afya njema na Mungu amkuze vema, Amen

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu yangu hapo juu kwa niaba ya Erik nasema AHSANTE SANA. Kuhusu picha ili kumwona alivyokuwa tutafikiria. Ahsante kwa kupita hapa na kuacha yako ya maoyoni na huo mpira si mpira wa kawaida ni keki ionekanaye kama mpira kwa vile ni mpenzi sana wa mpira kaka Erik.

Mama Alvin! Ahsante sana na nitafikisha salamu ka Erik.

Anonymous said...

Happy birthday Erik and many years to come. Be a nice boy and study very hard to reach your destination. By Salumu.

sam mbogo said...

Hongera sana kidume cha mbegu,Erik mungu akusimamie katika kila jambo ulifanyalo. kaka s

NN Mhango said...

Happy birthday Erik hata kama nimechelewa uncle wako. Si unajua maisha ya kuhanja hapa na pale na kujiweka sawa kiakili, kimwili na kiroho mbali na ulezi wa wajomba zako.

Yasinta Ngonyani said...

wajomba Salumu , Sam na NN Mhango ahsanteni sana kwa kuwa nami na pia kwa maombi yenu mazuri. Erik