Wednesday, June 11, 2014

TANZANIA INA MAKABILA MENGI SANA NA LEO NIMEONA TUUNGANE NA NDUGU ZETU WAHADZABE AMBAO WANAISHI KASKAZINI YA KATI YA TANZANIA

Najivuna sana kuwa mTANZANIA/MWAFRIKA... ebu angalia hapa furaha teleeee HAKUNA KULALA HATA KAMA HUJALA....MMMHH MARA nikaona wanaimba  nikaona niweke hapa pia hata kama sielewi nini wanaimba....ebu sikiliza na wewe.:-)


na hapa hakuna ngoma wala nini  yaani mpaka raha nimekumbuka mbali sana. Kama nilivyosema hapo juu ni kwamba Wahadzabe wanaishi kaskazini mwa Tanzania karibu na ziwa Eyasi jirani na Serengeti. Kabila hili idadi yao haizidi 1000... Na kati ya 300-400 huishi kwa kutegemea uwindaji.

2 comments:

Anonymous said...

Wahadzabe wameishaanza kuvaa nguo??Mana nafahamu walikuwa hawavai nguo hao! Ni watu wa asilia kwa kila kitu mpaka wazungu wakati fulani walikuja Tz kuwafanyia utafiti, ila huo utafiti ulikuwa sio mzuri mana ilikuwa kama kuwadhalilisha na kudhalilisha waafrika, na watanzania wote kwa ujumla hivyo watanzania walikataa! Ni hayo tu nimekumbuka kuhusu hao ndugu zetu wahadzabe. Mungu ibariki Tz na watu wake, naipenda sana nchi yangu Tz.

ray njau said...

utamaduni ni kioo cha jamii