Wednesday, September 18, 2013

NILIKUWA NATEGEMEA KULA HAYA MABOGA LEO KUMBE....HAYALIWI .....

Mavuno ya maboga..Nimepata manne na leo nilipanga iwe siku ya kuyala nilitaka kutengeneza supu, kuchemsha na futari. Lakini wifi yangu kaniambia hayaliwi eti ni chakula cha nguruwe tu na yeye ndiye alinipa mbegu. Sasa hapa najiuliza kama nguruwe anakula na kupona kwanini binadamu asile...Kuyatunza kwote nilikofanya yaani ni kazi ya cheka bure kweli???,,Na ndo nikaamua niwaulize ndugu zanguni je ni kweli?...Maana majani yake yana  mibamiba zikukuchoma zinawasha na majani ni mapana kuliko ile mboga ya maboga ya Njombe na ile ya kawaida...Au sijui ni mabuyu/ yale ya kutekea maji au kunywea maji yaani kata?...Duh kaaaazi kwelikweli hapa sasa nimekwama inabidi nianza upya kuwaza cha kula:-(.

11 comments:

ray njau said...

M PISHI mmoja katika Israeli la kale ambaye hakuwa mwangalifu alikusanya maboga ya mwituni ambayo ‘hakuwa anayafahamu.’ Aliyatia ndani ya mchuzi. Walaji, waliohofia kwamba chakula hicho kilikuwa na sumu walilia na kusema: “Kuna kifo ndani ya chungu hiki.”—2 Wafalme 4:38-41.

Kama mfano uliotajwa unavyoonyesha, tunapaswa kuwa waangalifu kuhusu chakula ambacho hakikutayarishwa vizuri kwa kuwa kinaweza kutudhuru au hata kutuua. Kwa hiyo, ili kuzuia magonjwa yanayosababishwa na vyakula, jifunze kutayarisha na kuhifadhi chakula kwa uangalifu.

Anonymous said...

Siku ingine ukienda Tz ubebe mbegu zako za maboga, ona sasa yaliyokukuta leo!!!!!???? Chakula cha jioni hakuna tena labda mnywe chai na mkate.....! jamani ulivyohangaika nayo na kuuliza yataiva yatakuwa njano duh sasa mwisho wa safari hata hayaliki! Kwani huyo wifi yako ni mzungu? hakukwambia tangia unapanda kuwa hayaliwi? Sasa majani na miiba mlikuwa mnakulaje au nayo hujawahi kuyala? Duh pole sana dada Yasinta. Ila no sweti figiri zetu si bado zipo au???

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray na usiye na jina Ahsanteni kwa ushauri....Wifi yangu si mzungu ..hakujua bali mbegu zilichanganyika.....Figiri bado ipo harikisha ni mwishomwisho sasa

Penina Simon said...

ha ha ha mbona bado hayajawa tayari???

Yasinta Ngonyani said...

Dada P. Nilipoona majana yanakauka nikajua yapo tayari kuliwa mwenzia :-)

Makrina Mbawala said...

za magono mlongowangu.unikubwishi maboga.lelulelu nihamba kugula maboga.chabwina kuteleka na kiki kangi?malombi na chai ande?

Haya utama bwina aloo kotoka kulya sumu.

Yasinta Ngonyani said...

Nambavala!!nihekeli kweli hamba kagulayi halafu unilasayi...Usengwili kwa ushauri wku yatinilya lepi.

Interestedtips said...

ila yanatakiwa yakomae, hapo yanaonekana bado mateke(si komavu)

Anonymous said...

Yanaliwa hayo na si chakula cha nguruwe, kihehe yanaitwa makisi. Ni matamu saaaana, sithani kama kweli ni sumu.

Anonymous said...

Yanaliwa hayo na si chakula cha nguruwe, kihehe yanaitwa makisi. Ni matamu saaaana, sidhani kama kweli ni sumu.
Kama alivyosema Ester yanatakiwa yakomae kabisa.

Anonymous said...

Yanaliwa hayo, but kama hayajakomaa hv!