Friday, September 13, 2013

MDADA KAPULYA SI MTU WA KUTULIA ..MSIMU WA BUSTANI UNAKARIBIA KWISHA NA SASA WAJA MSIMU KUCHUMA UYOGA NAYE NI MPENZI SANA WA KAZI HII KWA HIYO LEO ALIKWENDA MSTUNI NA HAPA NI MATOKEO YAKE....

 Kuchuma uyoga ni kitu ambacho nakipenda sana , unakuwa na wakati mzuri wa kutafakari, pia mazoezi nahalafu unapata mboga ..Mboga hii mimi nimeipata bure leo mstuni lakini kama ningekwenda kuinunua dukani kwa kilo ni kama kwa kila shilinga 23000/= . Nami nilipata lita kama tano hivi. Sasa kazi nyingine unaporudi nyumbani ni kuusafisha na ndio hapo nafanya kutoa mchanga na takataka nyingine,,,,
 Baada ya masaa matatu uyoga tayari umetolewa takataka zote na upo safi kwa kuliwa.....
 ...Uyoga upo kwenye plain pan tayari kwa kuandaliwa kwa ajili ya mlo wa jioni......
 .....baada ya dakika tano umepungua kiasi hiki na maji mengi yamejitokeza ..naendelea kukausha maji...
 ---Maji yamekakamia na hapa sasa ni kuweka chumvi, sukari kiduchu kwa ajili ya ladha..na pilipili manga kidogo na kikubwa zaidi siagi kama kijiko kimoja cha mezani unakaanga kwa dakika kumi....
 ...baada ya hapo unaweka krimu ya maziwa na kama huna krimu basi weka unga wa ngano kijiko kimoja cha mezani na maziwa kikombe cha chai,,,,
Na mwisho mlo ukapatikana hivi:- Wali, kuku, uyoga uloungwa kama nilivyosema hapo juu  ikiwa na nyanya kutoka bustanini  kwetu, tango na majani ya ruccula. Na hivi ndivyo ilivyoisha IJUMAA YA KAPULYA na mpishi ni YEYE MWENYEWE KAPULYA:-) TUTAONANA TENA PANAPO MAJALIWA !!

10 comments:

Rachel siwa Isaac said...

Duuhh njaa inazidi jamanii...

Anonymous said...

Unatutamanisha sana, hivi hakuna uwezekano ukatutumia kwa posta kidogo tukaonja! By Salumu.

Anonymous said...

Ladha yake ipoje cjawahi kula

ray njau said...

Ama kweli maisha na mafanikio ni kupanga na kupanga ni kuchagua.Asante kwa mlo mzuri ambao kila mdau wa kibarazani ameweza kuhudhuria japo washiriki ni wewe na familia yako.

Anonymous said...

jamani jamani jamani da Yasinta jamani mbona hivyo? njaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Sasa nifanyeje na tayari chakula kimeisha! Duh! Uyoga uyoooooooga!! Leo naona umeamua kuninyima chakula chako sawa!Haya msosi mwema na familia yako tu. Mie nalia macho tu.

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii na kuwashukuruni wote mliopita hapa na kuacha yaliyo ndani ya moyo...Ahsanteni sana ila mjadala bado unaweza kuendelea...

Mija Shija Sayi said...

Hivi Yasinta ulipitia Forodhani? kile chuo cha hotelia?

Yasinta Ngonyani said...

Mija HAPANA! hata iliko sijui kwanini umeuliza hivi?

Anonymous said...

Jamani huwa napenda sana comments za Dada Mija, unaonyesha kuwa mcheshi sana sana! Yani uwe una comment kila wakati mana unapoteaga sana wakati mwingine. Sijui nifanyeje ili nipinge urafiki na wewe Mija.

Ester Ulaya said...

nakutamania mno, uyoga mtamu jamaniiiii duh