Tuesday, September 3, 2013

TUSISAHAU METHELI ZETU ZA KISWAHILI....!!!!!

1. Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.
2. Yote yangáayo usidhani ni dhahabu.
3. Ungelijua alacho nyuki, usingelionja asali.
4. Radhi ni bora kuliko mali.
5. Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kapu ukavune.
NAWATAKIENI JUMANNE NJEMA WOTE NA KAMA UNA METHALI PIA ONGEZEA:-)

4 comments:

Said Kamotta said...

Ahsante kwa methali nzuri, zangu hizi hapa:
1. Chovya chovya yamaliza buyu la asali.
2. Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno.
3. Hasira, hasara.
4. Hiari ya shinda utumwa.
5. Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
6. Kinywa ni jumba la maneno.
7. Kuishi kwingi ni kuona mengi.
8. Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.
9. Kupoteya njia ndiyo kujua njia.
10. Mchagua jembe si mkulima.

ray njau said...

Asante dada Yasinta kwa elimu bila kikomo.Ni kweli wanazuoni wameulizwa na majibu hawajatoa kuhusu utamu wa asali.Kwa asali iwe halali kwao na vingine viitwe haramu wakati nyuki mali ghafi zake anazipata huko huko kwenye vile viitwavyo vya haramu?Najaribu tu kuwaza kwa sauti!Ungalijua alacho kuku wala nyama yake usingetia mdomoni.
"Wewe ukisema cha nini na wenzio wanasema watakipata lini?"{Yenu mwayafunikia mwiko na wenzenu mwayachezea mdundiko}

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Said...Ahsante kwa kuongeza hpo nami nimejifunza maana baadhi sikuwahi kuzisikia...

Kaka Ray!! Elimu ni kugawana ---Usengwili kwa mchango wako.

obat vimax said...

vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg