Friday, September 20, 2013

MNAKUMBUKA NILIWAHI KUWAAMBIA NIMEPANDA DODOKI ? HAPA NI MAENDELEO YAKE!!!!!

 Hicho chungu cha bluu ndio mmea wa dodoki/madodoki mwenyewe umekuwa na umetambaa mpaka kwenye paa ya varanda...sasa leo  nimegundua -----
 Mmea huo umeanza kutoa maua na pia dodoki zimeanza kujitokeza hakika nimefurahi sana. Ila sasa najiuliza nitaumewka wapi maana kaubaridi kameanza na mmea huu unataka joto  ....maana mwisho wako
...ndo dodoki linakuwa hivi hapa tayari lishakomaa na kukauka tayari kwa kujisugulia mwilini. Hili nilinunu Songea Sokoni mwaka huu...Kweli hili hapo juu karibu na ua litakuwa kama hili?...Mwenye ushauri naomba  tafadhali!! Nawatakieni jioni yenye upendo na amani.

6 comments:

Anonymous said...

Uhamishe sitting room isije ikapata snow na kujifia. Vipi mapapai bado? By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu! Nikihamishia sitting room basi itabidi mwenyewe nisikae hapo maana linatambaa kwa haraka kweli ....Ahsante kwa ushauri

Ester Ulaya said...

labda uliingize ndani likae karibu na dirisha liwe linapata mwanga

ray njau said...

Mhhh;sawasawa kabisa!

Anonymous said...

dodoki in english wanaitaje

Anonymous said...

Ridge gourd i think so..