Sunday, September 8, 2013

NAPENDA KUWATAKIENI JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGUNI WOTE!!

Nachukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda, kuniongoza, kunifanya nipate chakula, na kuniepesha na yasiyo mema. Nakutumaini wewe Mungu wangu , eh Mungu, wewe ni mwamba imara katika maisha yangu ...... Pia napenda kuwaombea familia, ndugu, wazazi/walezi, marafiki, majirani, wafanyakazi wenzangu pia hata madui zangu. Mwenyezi Mungu na atushushie wote baraka na upendo pia amani ...AMINA. . NA UJUMBE WA LEO NI:- SISI SOTE NI NDUGU,WATOTO WA BABA MMOJA.

5 comments:

sam mbogo said...

Asnte kwa sala nzuri na tamu, dada yasinta.siyo mbaya maramojamoja kutuombea na sisi japo huwa siamini katika kuombewa hupenda kuomba mimi mwenyewe.jumapili njema nawewe.
kaka s

Anonymous said...

Jumapili njema kwa wote da Yasinta. Mungu awalinde. By Salumu

ray njau said...

Yasinta;
Asante kwa moyo wenye fadhili zenye upendo na rehema.Nawe upate yale yote yaliyo ya wema katika familia yako.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana wote kwa kupita hapa Maisha na Mafanikio na kuacha kile kilichokuwa moyoni wenu..na pia ahsante kwa wale waliopita tu..Mungu awabariki

sharode darche said...

Asante sana mwenzangu