Monday, September 30, 2013

JUMATATU HII YA MWISHO WA MWEZI HUU WA TISA INATUKUMBUSHA AFRIKA....TANZAN IA NA MALIASILI YAKE...MBUGA!!!


Nawatakieni wote mwanzo mwema wa wiki hii. Binasi  nina furaha isiyo kifani leo kwani rafiki yangu mpendwa tumeongea leo..tulikuwa tumepoteana miezi kadhaa. AHSANTE MUNGU KWA HILI.

7 comments:

ray njau said...

Karibu sana nyumbani Tanzania na hongera sana kwa kupata fursa ya kuongea na rafiki yako baada ya kupotezana muda mrefu.

Anonymous said...

Tanzania Tanzania! Nakupenda kwa moyo wote........ Ingawa nimezaliwa TZ na kukulia (utotoni) ndani ya TZ, lakini mimi sio mTZ. Mimi ni raia wa.......By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray Ahsante sana ..nami ninawakaribisha wengine wote.
Kaka Salumu...Basi uwe na amani na Tanzania yetu...Kwa hiyo wewe ni raia wa wapi?...manaana hujamalizia hapo:-)

Anonymous said...

Da Yasinta. Nina ndugu ndani ya Tz. Siwezi kuitupa daima. Sitaki kujitangaza hadharani, ila kama utataka nikuambie wewe binafsi uraia wangu, nitumie email yako to shedhany@yahoo.com na mimi nitakujibu. By Salumu.

Emmanuel Mhagama said...

Tatizo ni moja tu. Nchi yetu ni nzuri na tunaipenda, lakini mambo yanayoendelea katika nchi hii, nahisi kama imeshauzwa. Nina wasiwasi ipo siku itaibuka mtu na hati miliki na atatutaka tuhame tumwachie nchi yake.
Kama twiga wanaweza kuvuka mipaka ya nchi kwa kupitia Uwanja wa ndege wa kimataifa halafu wanaohusika wanasema hawajui chochote, usalama uko wapi?

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu! Nitafanya hivyo Ahsante kwa yote.

Kaka Mhagamo mlongo wa mimi...usemayo yanaweza kuwa kweli maana inaonyesha kama kwamba viongozi wengi hawana uchungu na nchi hii. Ila duh itakuwa bonge la kupoteza nchi...Mungu apishe mbali kabisa jambo hili

Justine Magotti said...

Asante kwa kunijuza kwa taarifa nzuri