Wednesday, July 10, 2013

PICHA ZA WIKI:- KAPULYA NA NYWELE ZAKE!!

Hapa ni ijumaa wakati nasaka msusi...na ghafla jumamosi akanipa taarifa atanisuka kwa hiyo kazi sasa ni kufumua hizo nywele za kimasai...kazi ikaanza jumamosi..
 ..na jumatatu mzigo umekwisha sasa kazi kuchana eeeh bwana wewe si unaona hapa na afro yangu..leo jumatano ndo naenda kusuka ...nikirudi nitawaonyesha vipi imekuwa...Haya basi baadae:-)

11 comments:

Unknown said...

Dah umetokelezea sana na hiyo afro pia nimekependa rangi yako chocolate dada.

Manka said...

Yaani Dada yangu from another mother unapendeza kote kote,uwe umesuka au afro...nasubiri kwa hamu kuona msusi alivyokupendezesha.

Rachel Siwa said...

Umependeza Kadala. . Tusubiri picha mpya.

Kadala unajua kusuka?

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

achilia hilo afro kwa mwezi mzima tujinome maana na hapo unapendezeya!

Anonymous said...

Ni kweli Wambura nakuunga mkono kuwa dada Yasinta ungechana hata kwa muwa wa mwezi mana unapendeza pia na afro, unasuka mabutu usiku na asbhi ukiwa unatoka au kazini au muda wa kutoka wowte unafumua na kuchana afro inabakia safi tu na hivi sasa ni summer hali ya hewa nzuri hata kwa nywele sio kama winter mana huwa zinakatika mno. Pia una bahati ukisuka na ukifumua nywele zako hazikatiki. Tunasubiria style mpya ya nywele kwa hamu sana.

Anonymous said...

Dada wakati mwingine ni vizuri kupumzika na rasta na kuchana au pia kufanya style nyingine hii inakusaidia kurelaxisha muscules za kichwani mana naona wewe mwaka mzima ni rasta, je umewahi kulifikiria hilo? Jaribu hata kupumzisha misuli ya kichwani. Haya ni mawazo yangu tu.

ray njau said...

Mhhhhhhhhh;hakika mambo yote ni mema na sifa zipae hadi mbinguni wa Muumba wa mbingu na ardhi.Hongera kwa matiti uliyonyonya na mikono salama iliyokukuza.

Mija Shija Sayi said...

Yasinta hizi rasta ulitoka nazo bongo nini?

Hivi umeshawahi kufikiria kusuka rihanna style..(nakuchokoza dada)nasubiri jibu..

https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcT6JqNzvzLeE5R2QDaSZu5UIbwk_r6kkt8W3GoTiYVkxwJYB_IW

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote jamani...kama muonayo hapo juu nismeshasuka....
Mija dada mkuu msaidizi. ..kweli ae mchokozi. .Rihanna ndo nini? Ndiyo nilisika bongo.

Mija Shija Sayi said...

Nimekuwekea hiyo link uone Rihanna..

obat telat bulan said...

obat cytotec i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing cytotec