Monday, July 1, 2013

TUANZA MWEZI HUU MPYA NA JUMATATU HII NA SWALI HILI:-TABIA YA KUWAACHIA WAZAZI WATOTO MPAKA LINI?

BIBI NA WAJUKUU WAKE

Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza kuhusu hii tabia ambayo, bado inazidi kukua tu katika jamii zetu. Hasa inapokuja kwa sisi wadada/wanawake. Hii tabia ya kuwaacha watoto kwa wazazi, hivi hii haijalishi ya kwamba wazazi wamekwisha fanya kazi yao yaani kuku/kututunza sisi na sasa ni wewe/sisi inabidi pale inapowezekana tuwatunze wao?
Utakuta wazazi wanawatunza wajukuu na hapo hapo wanakuwa na majukumu mengine na ulemuda wa kupumzika unakuwa haupo. Halafu utakuta wanaweke wengine wameolewa, na kabla yake amezaa na yule/hao watoto anawaacha kwa wazazi je Huyo mume wake hawapendi watoto hao? Afadhali anemwacha mtoto kwa ajili ya kwenda shule.
Je? huu kweli ni uungwana...???

4 comments:

emu-three said...

Na watoto hawo wakikua na kujaliwa kuwa na maisha mazuri, hawo wazazi wanajitokeza, hawajui bibi /babu waliteseka kuwalea hawo watoto, ukizingatia maisha ya kijijini

ray njau said...

Ni Nani Anayepaswa Kuwafundisha Watoto Kumhusu Mungu?
===================================
“Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, lakini kila mtu aliyefundishwa kikamili atakuwa kama mwalimu wake.”—LUKA 6:40.

BAADHI ya wazazi huhisi kwamba hawana uwezo wa kuwafundisha watoto wao kumhusu Mungu. Huenda wakafikiri kwamba hawawezi kuwa walimu wazuri kwa sababu hawana elimu wala ujuzi wa kutosha kuhusu dini. Kwa hiyo, huenda wakamwachia mtu wa ukoo au kiongozi wa dini daraka hilo muhimu.

Ni nani basi , anayefaa zaidi kuwafundisha watoto kweli za kidini na maadili mazuri? Ona yale Biblia inayosema kuhusu jambo hilo, na uyalinganishe na yale ambayo watafiti wamegundua.

Baba Ana Daraka Gani?

Biblia inafundisha nini? “Akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.”—Waefeso 6:4, “Union Version.”

Watafiti wamegundua nini? Akina baba wananufaika jinsi gani wanapositawisha imani yenye nguvu? Makala Fathers’ Religious Involvement and Early Childhood Behavior, iliyochapishwa mwaka wa 2009, ilisema: “Kushirikiana na kikundi fulani cha kidini kunaweza kuwasaidia wanaume kuwa baba wazuri. Dini inaandaa utegemezo na mwelekezo na pia mafundisho na miongozo katika maisha.”

Biblia inaonyesha kwamba baba ana daraka kubwa katika kulea na kufundisha watoto. (Methali 4:1; Wakolosai 3:21; Waebrania 12:9) Lakini shauri hilo linafaa leo? Katika mwaka wa 2009, Chuo Kikuu cha Florida kilichapisha makala iliyozungumzia uvutano ambao akina baba wanakuwa nao juu ya watoto wao. Watafiti hao walitambua kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa watoto ambao baba zao walijihusisha sana katika malezi yao kuwa wenye huruma na wenye kujiheshimu. Pia, walitambua kwamba wasichana walikuwa na afya nzuri zaidi ya kiakili, huku wavulana wakiwa wenye adabu zaidi. Bila shaka, shauri la Biblia bado linafaa.

Daraka la Mama Ni Muhimu Kadiri Gani?

Biblia inafundisha nini? “Usiiache sheria ya mama yako.”—Methali 1:8.

Yale ambayo watafiti wamegundua: Katika mwaka wa 2006 kitabu Handbook of Child Psychology kilisema: “Kwa kawaida wakati ambao akina mama wanatumia pamoja na kila mtoto ni kati ya asilimia 65 na 80 zaidi ya ule unaotumiwa na akina baba. Na hali iko hivyo katika nchi nyingi.” Kwa kuwa mama anatumia wakati mwingi hivyo pamoja na mtoto wake, basi maneno, matendo, na mtazamo wake unakuwa na uvutano mkubwa katika ukuzi wa mtoto.

Wazazi wanaposhirikiana kuwafundisha watoto wao ukweli kumhusu Mungu, wanawapa angalau zawadi mbili zenye thamani. Kwanza, watoto wanapata nafasi ya kufanya urafiki pamoja na Baba yao wa mbinguni, urafiki ambao unaweza kuwanufaisha katika maisha yao yote. Pili, kutokana na mfano huo wa wazazi wao, watoto wanajifunza jinsi mume na mke wanavyopaswa kushirikiana ili kufikia malengo muhimu. (Wakolosai 3:18-20) Ingawa huenda wengine wakawasaidia wazazi, wazazi hao ndio wenye daraka la kuwafundisha watoto wao kumhusu Mungu na jinsi anavyotaka familia iwe.

Nancy Msangi said...

Sio uungwana kabisa tena unakuta mama wala hana sababu ya msingi ya kumwacha mtoto kwa bibi yake na pengine hata matumizi asitume jamani, kwn kuna mtu kakulazimisha kupata hao watoto❓na ndio mn watoto wa mitaani hawaishi dada natamani wote wanayofanya haya wangeiona hii mada.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni mliotangulia! Nakubaliana kabisa na mliyosema. Bibi na babu wamechafanya kazi yao kwa hiyo sasa ni kazi yetu. Kama mlivyosema wengine hawatumi chochote kile kwa hiyo bibi na babu wanaona ni majukumu yao. Afadhali basi wenye watoto wangekuwa wanapeleka chakula au kuweka watu walime kwa ajili ya watoto pamoja na bibi na babu. Wanashindwa kusema wamechoka tu....