Wednesday, July 24, 2013

HITORIA YETU:- HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA HAPO ZAMANI TANGANYIKA AMBAYO SASA NI TANZANIA....

 Ocean Road Hospital Dar-es -Sallam enzi ya wajerumaniYakobo Lumwe, ambaye pia aliitwa Yakobo Ng'ombe, alikuwa ni Mchungaji (Padri) wa kwanza mwenyeji wa kanisa la kiprotestanti pwani ya kaskazini mwa Tanganyika. Alitumika ndani na katika mzunguko wa maeneo ya Tanga mjini, sehemu ambayo sasa ni ya Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri katika Tanzania. [1] Maisha yake na kazi ni mfano wa kusifu jinsi gani wakristo wananchi walivyojishughulisha katika kueneza Injili na kujenga kanisa pamoja na wageni wamissionari.Kanzu ndio lilikuwa vazi la Padri hadi leo hii kote duniani! Tusisahau historia zetu ...MUWE NA SIKU NJEMA!!


3 comments:

Anonymous said...

Asante kwa kukumbusha historia ya Tanzania. Ila Lutheran hawana padri na hawatumii neno padri! Lutheran wana mchungaji tu. Hivyo hapo naona kama umechanganya. Either ungeelezea maelezo mengine mapya yaanayohusu padri kwa kanisa la Roman, vinginevyo inatia shaka kama unajua mana zake vizuri. Padri haoi na mchungaji anaoa, jaribu kutoyaweka pamoja kama ulivyofanya. Ni hayo tu, siku njema.

ray njau said...

Historia hii ni njema kwetu na watoto wetu ili jehazi la maisha na mafanikio lisizame.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina hapo juu..unachosema ni kweli lakini mimi nilipokuwa na kupata akili nilikuwa nasikia tu padri...na baadae baada ya kufika ulokole ndo nikaanza kusikia hili neno mchungaji kwa kwa hii ndio maana nimeandika hivyo...

Kaka Ray! Inabidi iwe hivyo ili wasisahau wapi ni kiini chao.