Saturday, July 6, 2013

UNAMKUMBUKA MZEE WA UTAMBUZI KAKA SHABAN KALUSE? BAADA YA KIMYA KIREFU KARUDI KWA KASI KUBWAAA ..KARIBU KAKA!!!

Habari zenu ndugu zangu....Nimerudi jana jioni baada ya wiki moja kuwa kwenye kasafari kidogo...Nimerudi kuja kuvuna mboga zangu, kuangalia mazingira nk. Baada ya kutembeatembea katika vibaraza na kuona kama kuna kipya au? Nimekutana na mzee wa UTAMBUZI  baada ya kimya kirefu amerudi kwa kasi. Ukipata kaupenyo mtembelee HAPA ufaidi mambo. KAKA KARIBU SANA TENA KATIKA ULIMWENGU HUU WA KUBLOG. PANAPO MAJARIWA TUTAONANA KESHO DOMINIKA....Ngoja niendelee na usafi wa mazingira na kupalilia mboga zangu.

2 comments:

Anonymous said...

Mwanamke mazingira, kazi njema Yasinta.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina. .. ahsante yaani nimefanya kazi kama farasi.. na sasa nipo hoi. Ila nimefurahi pamependeza. Karibu