Wednesday, July 31, 2013

NADHANI MNAKUMBUKA KIPENGELE CHETU CHA JUMATANO MAREDIO YA MADA, PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI LEO KATIKA PITA PITA ZANGU NIMEKUTANA NA HII...EBU SOMA....

Ndugu zangu kile kipengele cha JUMATANO YA MARUDIO KIMERUDI TENA MIKIKIMIKIKI ILIKUWA MINGI MNO. Haya karibuni na panapo majaliwa tutaonana tena:-) MWANAMKE: JE, BADO UNA HISIA ZA KUMPENDA MPENZI MLIYEACHANA...?


Kuondokana na hisia za mapenzi dhidi ya mpenzi uliyetokea kumpenda sana lakini mkaachana katika mazingira ambayo hukuyatarajia, si jambo rahisi na hasa kama wewe ndiye uliyeachwa. Unaweza kujiambia kwamba amekosea sana kukuacha na kamwe hatoweza kumpata mwanamke atakayempenda kama ulivyompenda wewe. Lakini kiukweli ndani ya moyo wako unampenda na kitendo cha kukuacha bado kinakuumiza na kukutesa. Inawezekana pia ukawa unatamani sana akurudie kwa sababu ulimpenda sana na unahisi upweke moyoni. Kwa mwanamke aliyeachwa, kuwaza hivyo ni jambo la kawaida kabisa, labda kama hukutokea kumpenda mwanaume huyo. Lakini kama miezi na miaka inapita na bado unaendelea kuwa na mawazo ya aina hiyo, basi hilo litakuwa ni tatizo, na hapa chini nitajaribu kueleza namna ya kuondokana na mawazo ya aina hiyo na kuendelea na maisha, kwani kuachwa na mpenzi sio mwisho wa dunia.               
1.Unamuwaza muda wote Hili ni jambo la kawaida, lakini duh, kama unajikuta unamuwaza mpenzi aliyekuacha muda wote na kujikuta unashindwa kufanya mambo yako ya msingi kwa ustawi wa maisha yako, basi hilo ni tatizo ambalo linahitaji kupatiwa ufumbuzi. Ingawa waswahili husema “lisilo machoni, halipo moyoni,” lakini mimi nasema sio kila lisilo machoni halipo moyoni, kwa swala la mapenzi nadhani iko hivyo. Ukweli ni kwamba hujui yuko wapi, anafanya nini au yuko na nani na hapo ndipo utakapojikuta ukitafuta picha mlizopiga mkiwa pamoja wakati wa kilele cha mapenzi yenu, na wakati mwingine unaweza kusikia wimbo fulani ambao aliupenda sana ukakukumbusha tukio lililowakuta mkiwa pamoja ambalo linahusiana na wimbo huo. Kwa kifupi ni kwamba, ni jambo la kawaida sana kumkumbuka mpenzi mliyeachana mara kwa mara baada ya kuachana. Lakini kama mawazo hayo yanaonekana kukuumiza na kukupotezea muda basi jua kwamba, jambo hilo linaweza kukuletea matatizo makubwa sana kiafya. Namna gani utaondokana na tatizo hili: Muda ni nyenzo muhimu sana katika kuponya. Kama unashindwa kupata suluhu ya namna ya kuondokana na mawazo ya huyo mpenzi mliyeachana naye, basi jipe muda, kwani kwa kujipa muda zaidi unajipa nafasi ya kuponya majeraha ambayo yanaonekana kukutesa. Kwa jinsi muda unavyochukua nafasi ndivyo unavyomudu kusahau na ndio maana waswahili husema yaliyopita si ndwele tugange yajayo Endelea kusoma zaidi HAPAhttp://kaluse.blogspot.se/2013/07/mwanamke-je-bado-una-hisia-za-kumpenda.html JUMATANO NJEMA SANA WOTE!!!

3 comments:

ray njau said...

“Inaonekana kuwa rahisi sana kumpenda mtu kuliko kudumisha upendo huo.”—DAKT. KAREN KAYSER.

ONGEZEKO kubwa la ndoa zisizo na upendo yamkini si jambo la kushangaza. Ndoa ni uhusiano tata wa kibinadamu, na wengi huingia katika uhusiano huo bila kujiandaa vya kutosha. “Inatubidi kuwa na uzoefu kiasi fulani kabla ya kupokea leseni ya kuendesha gari,” asema Dakt. Dean S. Edell, “lakini cheti cha ndoa chahitaji tu sahihi.”

Kwa sababu hiyo, ingawa ndoa nyingi hunawiri na kuwa na furaha tele, ndoa kadhaa hunyong’onyea katika matatizo. Huenda mwenzi mmoja au wote wawili waliingia katika ndoa wakiwa na matumaini makubwa lakini hawana ujuzi unaohitajika ili kudumisha ndoa. “Watu wanapopendana mara ya kwanza,” aeleza Dakt. Harry Reis, “kila mmoja huwa na uhakika mno na mwenziwe.” Wao huhisi kana kwamba mwenzi wao ndiye “mtu pekee duniani mwenye maoni sawa na yao. Nyakati nyingine hisia hiyo hufifia na inapokuwa hivyo, ndoa huathiriwa sana.”

Jambo la kupendeza ni kwamba ndoa nyingi hazifikii hatua hiyo. Lakini acheni tuchanganue kwa ufupi sababu kadhaa zinazosababisha upendo kufifia katika baadhi ya ndoa.

Unknown said...

Ni kweli Da yasinta mtu uliempenda kumtoa moyoni n kazi Sana me naona Ni vyema kutulia kwnz mpk utakapoona sasa unaweza kukabiliana na yote mn ukikurupuka kwasababu tu swala la mapenzi lipo utaishia pabaya, mn utaanzisha mahusiano bila kumjua mtu ambaye anakufaa kwny maisha yako mn kwa upande wng naona swala la mapenzi n kubwa so yahitaji maamuzi ambayo hutajuta bdae,

emu-three said...

Mimi nawaza tu, kuwa `mapenzi ni dhana ya `kufikirika' zaidi ya `uhalisia'