Wednesday, July 24, 2013

MAPISHI:- LEO MLO NILIOANDAA NI HUU ANGALIA HAPA CHINI !!!!

 Hapa ni mishikaki ya kidali cha kuku ambayo imeandaliwa kwa kuwekwa kwenye mafuta kidogo,soya kidogo, kitunguu saumu,tangawizi na limau. Na baada ya hapo ikatundikwa kama mishkaki kama muonavyo tayari kwa mchomo....
 Na hapa ni sahani zitakazotumika kwa vile tutakuwa nje basi vilibebwa vingine pia kwenye sinia hilo. ambavyo ni nyanya, tikiti maji, njegere mbichi kutoka bustanini na zeituni za rangi mbili kijani na nyeusi.
 Mishkaki imeweka kwenye moto tayari kwa kuchomwa na dada Kapulya ...bahati mbaya haonekani kwenye picha kwani anakimbia ndani na nje kuangalia wali....
 Baada ya dakika kumi mishkaki inaonekana hivi nimechoma dakika tano kila upande..tayari kuliwa ..KARIBUNI TUJUMUIKE....
Na hii ni sahani ya Kapulya mshkaki mmoja, tikiti maji na nyanya pembeni, njegere, wali, na kitamu zaidi MCHICHI KUTOKA BUSTANI YANGU....MMMMMHHH. Hakika kulima raha..si mnaona eeeeh ..KARIBUNI ..ILA NIMEUKOSA UGALI..NITAANDAA KESHO NA MBOGA MABOGA:-)..HAYA MUWA NA JIONI/USIKU AU LABDA MCHANA AU ASUBUHI NJEMA. KAPULYA/KADALA.

13 comments:

Rachel Siwa said...

KADALA..Kumbe nawe mzuri kwenye mapishi...Hongera sana na mnibakishie..naja huko!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Eeeeeh weewe kachiki hukujua hili mpaja kuchoma nimo...wahi twakudsubiri ..

Rachel Siwa said...

Kweli KADALA Unafaa haswa..naja..

Anonymous said...

Hongera kwa mapishi ambayo wengine tumekula kwa macho! Ila kama kawaida yangu usisahau kunibakishia.

Anonymous said...

Msosi nangae, msondo na biso!Hakuna raha kama kujipikia mwenyewe. Hongera da Yasinta.Wabheja sana. By Salumu.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Nilifikiri kitimoto dah !!!

Amina mzava said...

Da yasnta wenzio swaumu watutamanisha

ray njau said...

Huu hakika ni mlo ndani ya mlo!!

Anonymous said...

Yasinta usisahau kunipostia chakula hicho jamani! vyombo ntavituma kukurudishia.

Unknown said...

Da yasinta mate yamenijaaje mdomoni upo juu kwenye mapishi hongera sana

emu-three said...

Duh, unanitamanisha wakati tumefunga...lol

Mija Shija Sayi said...

Duuh! Yasinta uko mbali kwa kweli..

Yasinta Ngonyani said...

Ni furaha ilioje kuwa nanyi
Pro masangu karibu sana sana tena nilikutangaza umepotea nashukuru umerufi. Si unajua ndugu......mija ......kawaida tu.