Tuesday, July 30, 2013

BUSTANI:- BUSTANI YANGU IMEINGILIWA NA VIWAVI/BUU WANAKULA FIGIRI YANGU:-)

Kutunza bustani ni kazi kidogo leo nimeamka asubuhi hii na kwenda kuangalia bustani yangu nakutana na wadudu wanakula figiri yangu nimechukia mno tena mna na nimengóa yote na sasa nataka ushauri wenu kwa yeyote anajua jinsi ya kuwaua buu/viwavi maana sijakata tamaa nataka kujaribu tena kupanda figiri nyingine. 

 
 Mboga yaa maboga inastawi sa tena vibaya mno yaani mpaka raha hapo nimechuma jana hivyo.....
 Mchicha nao inatia nanga unapendaza..nitauchuma kesho si mnajua akiba haiozi karibuni tu hapa kutakuwa na baridi kiasi kwamba hata kuchimba shima ni shughuli....
 ....Sasa hapa ndipo nilipoudhika kwa kweli angalia figiri yangu ilivyoliwa. Nimejaribu kila njia kuwatoa viwavi/buu hawa lakini nimeshindwa. Je kuna anayejua dawa ya kuwatoa hawa wadudu/buu?...kaka Bennet upo nisaidie...nimeudhika sana sana kiasi kwamba-----
Nimengoa figiri yote lakini nipo mbioni kupanda nyingine tena leo hii nitaatika...

13 comments:

Anonymous said...

Pole da Yasinta! Jaribu kuulizia kwa Bwana Shamba anaweza kukusaidia. pengine figiri zako zina sukari guru! By Salumu.

Bennet said...

pole, ungekuwa Bongo ungewapulizia maji ya muarubaini au utupa wangeisha

ray njau said...

Kilimo uchumi

Utupa (Tephrosia vogelii) ni mmea wa jamii ya mikunde ambao huishi kwa muda unaozidi miaka mitatu. Mmea huu hutoa maua mengi, kuzaa mbegu nyingi na una majani mengi. Mmea huu hukua haraka pia ni rahisi kuzalisha. Huweza kukua hadi kufikia urefu wa futi 10. Inashauriwa kuukata baada ya miaka mitatu ili kurefusha maisha yake na kuwezesha kutoa majani mengi.

Mmea huu hustawi vizuri sehemu mbalimbali na zipo aina kuu tatu. Aina hizo zinatofautishwa kwa maua yake kama ifuatavyo: inayotoa maua ya njano, pinki na meupe.

Utupa unaoteshwa kwa mbegu na unakuwa tayari kutumika baada ya miezi 4-6 tangu mbegu zipandwe. Sehemu yenye sumu katika utupa ni majani na mizizi. Inadhuru visumbufu wa mimea vinapokula na kugusa, hii inavisababishia kukosa hamu ya kula.

Utupa unaweza kutumika kama kiuatilifu cha wadudu kama vile kupe, utitiri, kimamba, cabbage headworm, viwavi, sota funza wa vitumba, bungua wa mahindi, vithiripi, fuko, viroboto, chawa na magonjwa ya ngozi.

Pia utupa unafaa kutandaza shambani na kurutubisha ardhi.
Kutayarisha dawa ya majani ya utupa Kwa ajili ya kuua wadudu

Chuma majani mabichi kulingana na mahitaji ya shamba lako (hasa kabla mmea haujatoa mbegu kwani wakati huo dawa aina ya tephrosine ipo nyingi zaidi).

Yatwange mpaka yawe laini.

Loweka katika lita 20 za maji safi kwa muda wa masaa ishirini na nne katika uwiano wa 1:20 (kg 1 ya utupa kwenye lita 20 za maji).

Chuja mchanganyiko huo vizuri ili kuondoa vipande vya majani. Unaweza kutumia chujio la bomba.

Nyunyizia mboga zako au mimea mingine kama dawa nyingine. Tofauti iliyopo kati ya dawa hii na madawa ya kemikali ni kwamba haina harufu kali na madhara kwa afya ya mnyunyiziaji.

Dawa hii huweza kuua viwavi wa nyanya, nondo wa kabeji, wadudu mafuta na funza wa mabua ya mahindi (stalk borers), wadudu wanaoshambulia matango na kahawa.

Inapendekezwa itumike kabla mimea haijashambuliwa. Huua pia wadudu walao majani na mashina kama viwavi jeshi.

Unga unaotokana na majani ya utupa unaweza pia kutumika kuhifadhi nafaka hasa kwa ajili ya mbegu.
Kutayarisha dawa ya unga wa utupa

Twanga majani hadi yawe laini na uanike.

Saga majani yaliyotwangwa na kuanikwa kuwa unga.

Wakati wa kuotesha mazao, changanya unga wa dawa na mbegu ya zao unalotaka kupanda.

Tumia shambani kwa kunyunyizia dawa kwa kushika kwenye vidole vitatu kwa shina moja la kabichi.
Matumizi ya ghalani

Majani ya utupa yanatumika pia kuhifadhia mazao ghalani.

Yanatumika kufukuza fukuzi na mende wa maharage.

Chuma majani ya utupa, anika kwenye kivuli, twanga majani kupata unga.

Pima na changanya gm 100 katika kg 100 za nafaka/mikunde.

Dawa hii inatumika pia kuhifadhi mahindi.
Tahadhari kwa watumiaji

Kuvaa kinga ya mwili mzima wakati wa unyunyuziaji

Tumia dawa baada ya uchunguzi wa visumbufu

Usile mazao kabla ya siku 10- 14 kwisha baada ya kunyunyuzia dawa

Iwekwe mbali na watoto, maji na mifugo

Utupa ni sumu kali kwa samaki, inaweza kuua wadudu marafiki na wanyama.

Kwa nafaka za chakula hakikisha unga wa dawa unakaushwa vya kutosha kwani unaweza kusababisha harufu kali kwenye nafaka.

Rachel Siwa said...

Pole KADALA.. Huwezi kuuliza kwenye maduka ya mimea hapo kwenu?

Anonymous said...

Jamani jamani hao viwavi (Caterpillars) wameniudhi hata na mie sana tena sana tu! Ni vizuri ulivyoingòa ili wasiendelee. Ila nakushauri usipande figili bila ya kuwa na njia muafaka za kuzuia hao viwavi jeshi...mana wanakuja kama jeshi. Kama ulivopewa ushauri hapo juu either utumie njia asili ya huo mmea au madawa. Ila nakushauri kuhusu madawa yanataka uangalifu wa hali ya juu sana na pia kujizuia wakati wa kupuliza mana mengi yanawasha mwilini! mana unazuia mpaka uso yani kwa mask. Gloves na koti unavaa na chini buti dada Yasinta. Madawa pia yana madhara sana. Pia kuosha mboga vizuri na kwa maji mengi sana ukizichuma kabla ya kuzipika. Ushauri wangu kama hujawahi kutumia madawa heri usitumie kwanza, kwa kuwa eneo lako sio kubwa sana na ni bustani ya nyumbani tu, ila kama umewahi unaweza kutumia. Mara nyingi bustani za nyumbani ndogo ndogo huwa wengi hatupendelei kuweka madawa unless kama ni shamba kubwa au eneo kubwa sana. Kuna risk nyingi za hayo madawa dada Yasinta. Dawa asilia ni nzuri sana kama ulivyoelezewa na kaka hapo juu, ila nayo nadhani ukiwa na eneo kubwa inakuwa rahisi zaidi. Kwa ushauri wangu usipande leo tena hizo mboga kama hutatumia njia yoyote kuondoa hao viwavi mana watarudi tena na utakuwa umepoteza nguvu zako na muda. Paache kwanza hapo ulipochuma au utapanda eneo jingine? ila matokeo yanaweza kuwa hayo hayo ukipanda hapo ulipozichuma mana watarudi tena. Summer hii imekuwa na wadudu sana hapa Sweden sijui kwa kuwa jua limewaka kali mana hata hapa kwangu nje kulikuwa na mchwa na haijawahi kutokea. Wapigie simu wale wa madawa ya fumigation hapa Sweden wanaitwa ANTICIMEX wanaweza kukusaidia zaidi. Je kwa sheria zao za mazingira unaruhusiwa kupuliza dawa shambani kwako mwenyewe bila kuwajulisha wataalamu hapa Sweden? mana Sweden wapo makini sana na mazingira na wanajitahidi kuyatunza kwa hali ya juu hasa kwenye kutumia pesticides au niseme kemikali ambazo ni za kuua wadudu wa mimea shambani na wengine hata kama sio shambani.

ANTICIMEX (WADUDU) namba zao ni hizi hapa kwa Sweden:
Tel : 08-517 633 00
Fax : 08-517 634 42

Anonymous said...

Samahani mesg. hapo juu nikisema madawa yana madhara nina maanisha pesticides (madawa yenye kemikali). Madawa asilia au njia asilia hazina matatizo zaidi.Dada Yasinta tujulishe umefikia wapi mana natamani sana kujua, kilimo kwanza. Hao wadudu natamani niwachape viboko jamani walivyoniudhi dada, we acha tu. Hapa kwetu hawa ants(mchwa) walishambulia maua kwa nje yani mpaka wakawa wanaingia ndani hata sijui wanapitia wapi ukiamka asubuhi nawakuta ila anticimex walileta dawa yao kwenye chombo wakaweka hicho chombo ndani kina kama maji ambayo nadhani ilikuw adawa Fulani, kilikuwa wazi kikubwa kiasi hivi kwenye maua nje. Na baada ya hapo hatukuwaona tena mpaka leo. siku njema. Ni mie niliyeandika hapo juu (July 30, 2013 at 3:47 PM)

Anonymous said...

Dust plant foliage with Bacillus thuringiensis, or Bt, powder. Bt is a natural bacteria that kills caterpillars, but it does not harm most other beneficial insects. Hii nimeisoma ila ulizia zaidi kwa wataalamu dada. Ni natural pesticides haina madhara Bt (Bacillus thuringiensis): Pia ungejua ni aina gani ya viwavi jeshi hao? umewapiga picha? Ungepiga picha kabla hujangoa.

Anonymous said...

Tena hao wanatafuna usiku ndio wanavamia jamani jamani! caterpillars wabaya sana. Figili mboga tamuu sana na ndio wameionea.

Unknown said...

Jamani nimeumia km ndio mm pole Sana Da yasinta ungeulizia kwenye maduka ya dawa za mifugo pole Sana jaman

Yasinta Ngonyani said...

Duh! kaaaaazi kwelikweli...kwanza samahani kwa kuchelewa kusema kitu mambo ni mengi na maudhi ya viwavi bado ninayo. Nashukuru sana wote kwa mawazo/ushauri wenu. Nitafanya utafiti maana huwa sipendi sana kupulizia madawa. KWA KAWAIDA huwa hawawi hivi nadhani kama alivyosema msomaji mmoja hapo juu labda kwa ajili ya joto. Naanza kupata hofu wasije wakaamia kwenye nyanya zangu ambazo nitaanza kula wiki kesho...au mchicha ..ila kuna mbinu nimegundua nitawaambia nikifanyikiwa:-)

Anonymous said...

tuambie hiyo mbinu dada

Yasinta Ngonyani said...

Sitawaambia Bali nitawaonyesha ongezeni tu subira muda si mrefu mtaona...

Kajunason said...

Safi sana kama umefanikiwa kupata njia ya kuzuia hao viwavi jeshi ambao wanaharibu mazao yetu.