Thursday, January 17, 2013

Wanawake hupenda kuonewa wivu……!

Kama ulikuwa hujui, ni kwamba wanawake hupenda kuonewa wivu, lakini kwa kiasi kidogo tu. Lengo lake hasa ni kutaka kujua kama unamjali kwa kiasi gani. Wakati mnapoingia kwenye mghahawa ama kwenye Baa, mwanamke angependa ugundue kwamba kuna mtu amevutiwa naye, hata kama mtu huyo ni muhudumu. Pia wakati wanaume wengine wanapowakodolea macho unapokuwa naye barabarani, ama wafanyabiashara wa mitaani wanapopiga kelele na miluzi ya kumsifia, angependa kuona utalichukuliaje hilo. Unapoonekana kutofurahishwa na vitendo hivyo na kumtaka mtafute sehemu nyingine ambayo haitakuwa na rabsha, ama nawe utakapoonekana kuona fahari ya kuwa na mwanamke anayevutia watu, basi mpenzi wako huyo naye ataona kwamba yeye ni muhimu kwako. Lakini ni lazima uwe mwangalifu usije ukajenga ama kuonesha wivu wa kupindukia, kwani hilo litamfanya mpenzi wako ahisi unamuona yeye si mwaminifu, au ni Malaya. Kumbuka wivu ukizidi sana huwa kero. HABARI HII NIMEIPATA UTAMBUZI NA KUJITAMBUA....

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Katika maisha ya ndoa inabidi kuwa na uvumilivu kwani huwa na mikwaruzo mingi sana, kutofautiana pia kuko..kwa hiyo hapa inachotakiwa na uvumilivu, kuaminiana na kuwasiliana. Ndiyo wapo wangine hawajali hata mke/mume akipendwa au tu hata ile kuonana/kuongea na watu..anaona ni kawaida tu. Lakini wapo wengine ni moto kweli, anataka kila wakati yeye na mkewe/mumewe..mara nyingi nimekuwa nikijiuliza kama kweli hii ni sahihi lakini sijapata jibu kamili zaidi ya inaonyesha kama mmoja hapa anataka kumchunga wenzake kila dakika ambayo ni mbaya sana katika maisha ya ndoa.

emuthree said...

Imekaa vyema hiyo tupo pamoja, mpendwa pole na safari

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Ingawa kunaweka kuwepo ukweli, huwa sipendi hitimisho la jumla. Inategemea ni wanawake wa eneo na mila gani. Kuna wengine kuonewa wivu ni kupoteza muda--- wao wanajali pesa babangu. Uwanee wivu unajitesa bure Rua! Kwa wanaojua mapenzi wivu muhimu. Ila kwa akina pesa babangu wivu ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Je na wanaume wanapenda kuonewa nini?

gadiel mgonja said...

thts perfect,ila hawa wanawake ukiwasifia sana wanajisahau wanalega sifa baadae wanaharibu hadi tabia zao nzuri kwa kusifiwa.kwani mke mwingine anaweza akasifiwe lea kwa namna alivyikua sasa unajikuta kesho anafanya maboresho akijua anazidi kujijengea umaarufu kumbe maskini wawatu ndo anaharibu kabisa.

ray njau said...

Wengi leo huona ndoa kuwa ya muda tu. Wanaingia katika ndoa haraka-haraka kwa kuwa wanafikiri itatosheleza mahitaji yao, lakini wanatazamia kwamba watatoka kwa urahisi mambo yakichacha. Hata hivyo, kumbuka kwamba Biblia inapozungumzia kifungo, kama vile kifungo cha ndoa, inatumia mfano wa kamba. Kamba za meli hukusudiwa kudumu, zisikatike-katike wala kufumuka hata kunapokuwa na dhoruba kali sana. Vivyo hivyo, ndoa imekusudiwa kudumu. Kumbuka kwamba Yesu alisema: “Kile ambacho Mungu ameunganisha mtu yeyote asikitenganishe.” (Mathayo 19:6)Ukifunga ndoa, unapaswa kuwa na maoni hayohayo kuhusu ndoa. Je, uwajibikaji wa aina hiyo huifanya ndoa iwe mzigo? Hapana.
Kila mmoja anapaswa kuendelea kuwa na maoni yanayofaa kuhusu mwenzi wake wa ndoa. Kila mmoja wao akifanya yote awezayo kukazia fikira sifa nzuri na bidii ya mwenzake, ndoa hiyo itakuwa yenye furaha na yenye kuburudisha. Je, kuwa na maoni yanayofaa kuhusu mwenzi asiye mkamilifu ni kujifanya kipofu? Yehova hawezi kamwe kuwa kipofu, hata hivyo, sisi hutazamia awe na maoni yanayofaa kutuelekea. Mtunga-zaburi alisema: “Kama ungekuwa unaangalia makosa, Ee Yah, Ee Yehova, ni nani angesimama?” (Zaburi 130:3) Waume na wake pia wanapaswa kuwa na maoni yanayofaa na kuwa tayari kuwasamehe wenzi wao wa ndoa.—Wakolosai 3:13.
Kadiri miaka inavyopita, ndoa inaweza kuwa baraka hata zaidi. Biblia inazungumzia ndoa ya Abrahamu na Sara walipokuwa wazee. Bila shaka maisha yao yalikuwa na mabonde na milima. Wazia hali ya Sara. Huenda alikuwa na umri wa miaka 60 na kitu alipoondoka makao yake yenye starehe katika jiji lenye ufanisi la Uru na kwenda kuishi katika mahema maisha yake yote. Hata hivyo, alijitiisha chini ya ukichwa wa mume wake. Alikuwa kikamilisho na msaidizi kwelikweli kwa Abrahamu, na kwa heshima alimsaidia kufanikisha maamuzi yake. Ujitiisho wake haukuwa wa kijuujuu. Hata “ndani yake mwenyewe,” alimwita mume wake bwana. (Mwanzo 18:12; 1 Petro 3:6) Alimheshimu Abrahamu kutoka moyoni.
Bila shaka, hilo halimaanishi kwamba Abrahamu na Sara walikubaliana katika kila jambo. Siku moja alitoa pendekezo ambalo “halikumpendeza Abrahamu hata kidogo.” Lakini Abrahamu alitii maagizo ya Yehova, na kwa unyenyekevu akaisikiliza sauti ya mke wake, nayo familia yao ikabarikiwa. (Mwanzo 21:9-13) Waume na wake leo, hata wale ambao wamekuwa katika kifungo cha ndoa kwa miaka mingi, wanaweza kujifunza mengi kutokana na wenzi hao wenye kumwogopa Mungu.