Thursday, October 18, 2012

YASINTA:-HIVI KWA NINI NINYI WAAFRIKA MPO HIVI?

Ni maswali nililoulizwa na wafanyakazi wenzangu pamoja bosi wangu..
Yasinta:Nikawauliza tupoje?
Wafanyakazi wenzake: Wakasema ninyi wakati wote mna furaha tu mkila, mkiwa na njaa. Mkiwa na nguo na msipokuwa na nguo ninyi/waafrika kwenye ni furaha tu. Inakuwaje?
Yasinta: Ndivyo tulivyo, hakuna sababu ya kumnunia jirani  itakuwa kazi bure.
Wafanyakazi: Au kwasababu kila wakati kunakuwa na jua ndo maana watu wanakuwa na furaha wakati wote?
Yasinta: Nikatabasamu..labda
Wafanyakazi: Yasinta, inasemekana kwamba ninyi/waafrika ni wepesi sana kucheza ngoma je? ni kweli?
Yasinta: Ni kweli.
Wafanyakazi: kwanini?
Yasinta: kwa sababu ni aina ya mila zetu.
Wafanyakazi: safi sana.
Na mwisho nikaa na kutafakari maswali yao nikagundua ni kweli tuna tabia hizo ila sina uhakika na majibu yangu na ndio nimeona nisaidiwe na ninyi ndugu zangu. Nitashukuru sana ....

8 comments:

ray njau said...

75/100

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! 75/100, unamaanisha nini? je unaweza kufafanua? ntashukuru!!

ray njau said...

Katika hili somo hizo ni alama zako!!

Yasinta Ngonyani said...

mmmhhh..na wewe ungejibu zipi?

ray njau said...

Mhhhhhhhhhhhhhhhhh!!
Hapana Yasinta!Sema Asante!
Ulivyojibu yatosha sana.Na hiyo na hiyo ni 100/100 lakini imewekwa 75/100 ili iwe changamoto kwako usisinzie.

batamwa said...

Majibu uliyotoa Yasinta ni tosha kabisa usione sasahivi watu wanaleta haya mambo ya kuvunja makanisa na kutukanana kwenye nyumba za ibada sisi waafrika ndio asili yetu,kwanza zamani babu ilikuwa mwiko kulachakula bilakuwa na mjukuuwake pembeni au mfano unaenda baa kunywa peke yako na uponajirani yako pembeni hujisikii vizuri hivyo unajikuta umeisha kuwa kampany moja hiyo inatokana na upendo tuliozaliwa nao tena nyinyi wa ulaya ndio mmetuletea tabia za huko maana nasikia hatakwenda kwa jirani bila taarifa hupokelewi

Mtesuka said...

Nimelipenda jibu lako la .. "ndivyo tulivyo". linaujumbe mzito.

MARKUS MPANGALA said...

Nakuunga mkono mpendwa wangu dada Yasinta. Unajua hata kaka yetu Ndesanjo Macha aliwahi kuelezea jambo hiyi kwa kina jinsi waafrika tunavyotoa mafunzo kwa walimwengu. Nimeipenda sana hii