Wanablog wenzangu nimetumiwa ujumbe huu kwa njia ya barua pepe nami nimeona palipo na wengi hapakosi... au Umoja ni nguvu kwa hiyo naomba tusaidiane kulijibu swali hili kwani nina uhakika wengi tutakuwa tumejifunza kitu hapa. Haya hapa chini ndio ujumbe wenyewe:-
----------------------------------------------------------------------------------
Hujambo?
Mimi ni Mkenya na ninapenda kusoma makala yako kwenye blogi yako. Ningependa unitafutie jina mwafaka la wazazi wa mume na mke wanavyopaswa kuitana. Nimepekuwa kwenye kamusi lakini juhudi yangu haijazaa matunda.
Nitashukuru.
10 comments:
JIBU NI "WAKWE"
Hata mimi ningesema ni WAKWE yaani mama mkwe na baba mkwe.
Malkiory na yasinta hapana! lenu ni jina la watoto kuwaita wazazi wa upande wa pili. huyu jamaa anataka jina la wao wazee wakikutana waitaneje au watambulishaneje. wewe ukikutana na baba/mama aliyekuzalia mke/mume unamwita 'mkwe'(na nyumbani kwao ni 'ukweni'). swali la huyu jamaa ni wataitanaje mfano baba yako na baba wa mke/mme wako?
kurahisisha. tuseme mmeoana kutoka kijiji kimoja. wazazi wenu wote wanne wapo hapo kijijini. na nyie mpo dar es salaam au stockholm. sasa wao wanakutana wao kwa wao katika kilabu au msiba fulani pale kijijini, wataitanaje au watatambulishanaje? hilo ndio swali.
unyakyusani (nadhani na makabila mengine mawili ama matatu) wazazi wanaitana 'kajemba'
Ok kaka john umenifumbua macho na akili kule kwetu ungonini wataitana "wayamba" au mmoja "myemba" Ahsante.
John, nakubaliana nawe kuwa tumechemsha.
Sasa,kama mlichemsha si mtoe jibu! :-)
Mimi najua kwa kilugha chetu lakini kwa kiswahili chenu mmmh hapo sioni ndani ila ungeniuliza kwa kinyamwezi au kisukuma jibu ningewapa.
Acha tusubiri wajuzi watujuze, swali zuri.
unyamwezini wanaitana "kivele"
uhayaniwanaitana ENSHANZI YANGE.
vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg
Post a Comment