Monday, August 23, 2010

Unapojikuta unashindwa kujieleza nini maana ya baadhi ya maneno kwa kiswahili!!

Wakati nipo likizo nimepata swali kutoka kwa msichana mmoja ambaye alikuwa juzi juzi tu Tanzania, Zanzibar na Mombasa. Aliniuliza kwanini waswahili tunasema/itana BWANA NA NDUGU?
Mmmmhh! nikasema hapa ipo kazi, nikarudi nyumbani nikafanya upekuzi kwanye KAMUSI sanifu ya kiswahili. Na hapo nilipata kama zifuatazo:- Bwana- Ni jina la heshima la mwanamume bwana ni mume, bwana ni mwanamume umfanyiaye kazi, mtu mwenye cheo, tajiri, mwajiri. Bwana ni Mwenyezi Mungu, Allah. Pia bwana hutumika kumfanya mtu asikilize, hutumika kumgutusha mtu.

NDUGU:- Ni watoto waliozaliwa tumbo moja, yaani baba na mama mmoja au mama mmoja au baba mmoja. NDUGU- n watoto wa jamaa au ukoo mmoja, NDUGU ni rafiki mkubwa, NDUGU ni mtu mwenye kushirikiana naye katika shughulu za dini au siasa.
Haya yalikuwa maelezo yangu kwa msichana huyu. Lakini hata hivyo hakunielewa kwani alisedma alisikia watu wakiitana haya majina hata kama hawakuwa wanafahamiana. Je? ungekuwa wewe ungemjibu nini? naomba msaada wenu!!!!!

8 comments:

emu-three said...

Unajua kiswahili kina maneno ambayo yanaweza kutumika sehemu mbalimbali kwa neno hilohilo, inategemea umekusudia nini, lakini msingi na maana ya maeneo hayohayo yapo palepale kama ulivyokokotoa kwenye kamusi.

Kwa mfano utasikia mtu anasema
'we ndugu yangu we acha tu' huyu anamwambia jamaa ambaye hata hamjui, lakini kwa kuwakilisha uumbe wake katumia neno ndugu!
Kwa kifupi mwambie kiswahili maneno yake hayajitoshelezi moa kwa moja, ya kuwa wakati mwingine inabidi kutumia neno maja sehemu mbalimbali, lakini maana ikawa ile ya ujumbe!

EDNA said...

kamusi imesema kweli...

Mija Shija Sayi said...

Kama hadi hapo hajaelewa ingekuwa mimi ningefanya jitihada nimkutanishe na Matondo...lol!!!!

Hata hivyo naungana na M-3(emu-three)

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

binadamu wote ni ndugu na...ni moja!!!!

unadhani damu kundi O la mzungu haiwezi kuwekwa kwenye mwili wa mweusi a.k.a m-black?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kama alivyosema chacha, sisi sote tu wamoja, we are one! believe in unity na sio upungufu wa kiswahili

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Matondo wa nini tena wakati Kamusi imesema kila kitu? Kama hajaelewa chukua kiboko umtandike!

Mwikuyu Peter said...

Jibu ni kuwa Kiswahili kinakua siku hadi siku, uliyo mweleza ndio maana sanifu jumatano njema

obat vimax said...

vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg