Monday, August 30, 2010

Umejiuliza kwa nini mwanafunzi wa kike anakutaka?

Wanafunzi wasichana wakiwa katika picha ya pamoja

Wapo wanaofanya ngono kwa lengo la kusambaza magonjwa waliyo nayo. Nakumbuka niliwahi kusoma habari moja kuhusu mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu fulani aliyetenmbea na wanaume zaidi ya 100 kwa lengo tu la kuwaambukiza ugonjwa wa Ukimwi
Umejiuliza kwa nini wanafunzi wa kike au wanawake wanafanya ngono? Inawezekana kusiwepo na jibu la moja kwa moja na kwa wewe msomaji wa makala hii labda unaweza kutaja sababu kadhaa kama vile kutafuta watoto, kujiridhisha nafsi zao na hata ishara kuwa wanawapenda wanaofanya nao tendo hilo. Mwandishi Wetu Christine Chacha anafafanua zaidi.
UNAWEZA kuendelea kutaja sababu kadhaa unazozijua lakini ukweli ni huu, wanawake wana sababu nyingi sana zinazowasukuma kufanya ngono tena nyingine unaweza usizijue.
Kwa mujibu wa kitabu kilichochapishwa hivi karibuni kiitwacho " Why Women Have Sex kuna sababu 237 zinazowafanya wanawake kuvutiwa na tendo hili.
Hivi ndivyo wanavyosema wanasaikolojia wawili Cindy Meston na Davis Buss walioandika kitabu hiki kilichopata umaarufu mkubwa wa kupendwa na watu wengi duniani.
Unaweza ukashangaa lakini huu ndio ukweli, sababu nyingi zinazotajwa na wanawake zaidi ya 1000 waliohojiwa hazihusiani kabisa na kitu kinachoitwa mapenzi na kwa zile zinazohusiana basi si kwa uhusiano wa ukaribu.
Kwangu, habari hii niliipokea kwa mstuko kwa kuwa najua hakuna hata mmoja asiyezungumzia kwa nini tumekuwa tukifanya ngono.
Nilichokuja kukimaizi mwishoni ni kwamba sababu zinazowasukuma wanawake kujihusisha na tendo hili zinatofautiana kwa sababu za kiumri na nyakati.
Nitoe mfano kwa wanafunzi wa shule za sekondari hasa ile ya juu, wengi wetu tuliweza kufanya tendo hili kimajaribio, tulitaka tudadisi ladha ya jambo hili hatimaye tukapoteza usichana wetu.
Kwa ngazi ya chuo kikuu, ngono haikuwa tena mchezo wa majaribio bali kitu tofauti, kipi hicho? Wengi tulifaya kama mojawapo ya njia za kujipa raha na kila mmoja alikuwa akifanya.
Muulize mwanachuo yeyote wa kike hatosita kukwambia kuwa njia rahisi zaidi ya kumpata mwanamume basi zungumza naye kuhusu ngono. Huwezi kufeli kama utamkabili kwa kutumia mtego huu. Wapo hata waliokuwa wakilazimika kufanya ngono ili wawe karibu na wanaume ili hatimaye waje kupata alama nzuri katika masomo.
Leo ninapohudhuria katika sherehe za kuwafunda wanawake wanaoolewa maarufu kama kitchen party, ngono huku imechukua sura nyingine. Wanaotarajia kuolewa wanaambiwa ngono ni sawa na kazi ama jukumu lao muhimu pale wanapokuwa kwa waume zao. Na lazima jukumu hili walikamilishe ipasavyo wanapokuwa katika maisha ya ndoa.
Tena jukumu hili ni maalum kwa ajili ya kumfurahisha mume na ilivyo wanatakiwa walifanye kiustadi mkubwa ili wawavutie waume zao ili wasipate mawazo ya kwenda nje kutafuta wanawake wazuri zaidi katika tendo hili. Hapa ngono hailengi kumpa raha mwanamke bali mwanaume.
Kwa mujibu wa kitabu nilichokitaja hapo awali, asilimia 84 ya wanawake walisema wanafanya ngono kuwaridhisha wanaume zao na si kama wanafurahia kwa kiwango kikubwa kufanya hivyo.
Mpaka hapa nikawa hoi, ndipo niliopoamua kutafiti hapa mkoani Dar es Salaama nikitaka kujua kwa nini wanawake wanajihusisha na tendo la ngono.
Visasi
Kumbe kulipiza kisasi kunaweza kuwa sababu ya wanawake kujiingiza katika tendo la ngono hasa pale wanaposalitiwa na wapenzi wao. Wengine hutaka tu kuwarusha roho wanaume zao kwa kuwapa hisia kali za wivu.
Martha Peter (29) anayefanya kazi za usanifu kurasa ni mfano mzuri wa wanawake walioamua kufanya ngono kulipiza kisasi baada ya kusalitiwa na wapenzi wao waliowachunuku kwa kiwango kikubwa.
"Nilitaka alipe kwa mabaya aliyonitendea, nilitaka nimkabili katika njia ambayo ingemuumiza sana,’" anasema
Nini alichokifanya kumuumiza mpenzi wake wa zamani? Anasema, "Nilijua ukaribu aliokuwa nao na kaka yake wa kufikia hivyo nikatembea naye, kilichotokea ni vurumai kubwa katika familia yao, baadaye nikaachana na wote."
Kusambaza magonjwa
Wapo wanaofanya ngono kwa lengo la kusambaza magonjwa waliyo nayo. Nakumbuka niliwahi kusoma habari moja kuhusu mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu fulani aliyetenmbea na wanaume zaidi ya 100 kwa lengo tu la kuwaambukiza ugonjwa wa Ukimwi.
Alipoulizwa alisema alifanya hivyo kulipiza kisasi baada ya yeye kuambukizwa na mpenzi wake wa kiume waliokuwa wakisoma pamoja chuoni.
Ngono kama njia ya kujifurahisha
Leo wanawake wanakataa ule usemi eti kwa sababu za kijinsia wao hufanya ngono kwa kuwa tu wanawapenda wapenzi wao na kwamba wanaume wao ndio pekee wanaolichukulia tendo hilo kama njia ya kujipa raha.
Ilivyo hata wanawake nao wanapenda kufanya ngono kwa kuwa wanaburudika kufanya hivyo. Tena kwa wanawake vijana hii ni njia nzuri ya kuburudika na kujiliwaza kimwili. Kama ilivyo kwa wanaume, hii nayo ni raha na wala hawajuti kufanya hivyo.
" Nafanya ngono kwa sababu nataka kufanya hivyo, ngono inaburudisha na kusisimua," anasema Bella Roman, Meneja wa Fedha wa kampuni moja nchini.Anaongeza kwa kusema:
"Tupo katika jamii huru, sina sababu nyingine ya kufanya ngono.
Kwa nini nami nisifanye nikafurahi kama wanaume."
Roman (34) anashangaa kwa nini jamii inakubali wanaume kupenda ngono lakini ikitokea kwa wanawake wanashukiwa kwa sababu kadhaa kama vile kuitwa makahaba. Anauita huu kuwa ni mtazamo wa unaopaliliwa na hisia za mfumo dume.
“Inawafanya wanawake kujihisi vibaya pale wanapotaka kutimiza matakwa yao ya kufanya ngono. Naweza kufanya ngono kama kujiridhisha moyoni na wakati huo huo nisiwe kahaba, jamii lazima ilikubali hili,†anatetea mtazamo wake.
Roman anakiri kuwa ana marafiki kadhaa wa kiume na wote anafanya nao ngono pale anapojisikia. Na wanaume hawa wote wanajua kuwa hawana mkataba naye kwa kuwa anawatumia kutimiza haja zake kingono.
Kumchunga mwanaume
Baadhi ya wanawake akiwemo Aysha anayesoma chuo kikuu wanaamini kuwa ukitaka mwanamume awe wako pekee basi usimyime raha.
"Nimekuwa nikifanya ngono na rafiki yangu wa kiume ili kumweka karibu nami katika uhusiano na asijaribu kunitoroka. Niliamua kufanya hivi baada ya kuomba ushauri kutoka kwa marafiki walioniambia huwezi kumchunga au kummiliki mwanamume kwa kumpenda tu, waliniambia nitumie ngono kumweka katika himaya yangu," anafafanua.
Aysha hana jinsi amekuwa akifanya ngono ili kumridhisha mpenzi wake ambaye hakika ndiye aliyekuwa kinga’ng’anizi wa kutaka kufanya kitendo hicho. Na kwa kuwa hataki kumpoteza Aysha hana jinsi ila kujisalimisha.
Anawakilisha wanawake wengi ambao wamekuwa wakifanya mgono kwa kuwa kwa namna fulani wanalazimishwa na wapenzi wao japo wao wenyewe hawapo tayari.
Wengine huruma huwaponza, kwa nini wasiwape unyumba wanaume wanaowazengea kwa muda mrefu wakiomba kupewa bahati ya kukutana nao kimwili? Kwa wengine hawa wana lao jambo, wanataka ngono na wanaume ili kujua tu ukubwa wa maumbile walioyajaaliwa.
Fanya ngono umsahau wa zamani
Kwa hili Aysha ana haya ya kusema: " Baadhi ya marafiki zangu nami nikiwemo baadhi ya nyakati tunafanya ngono kama njia ya kuwasahau wanaume wa zamani. Sote tunaamini njia bora ya kumsahau mwanamume ni kuanza uhusiano na mwanaume mwingine."
Huna haja ya kuomba ngono inatosha
Baadhi ya watu wanafikiri wanawake wanaofanya ngono kwa lengo la kutaka kupewa chochote ni makahaba, si kweli. Ukweli ni kuwa hata walio katika ndoa na aina nyingine za mahusiano ya kimapenzi wanatumia ngono kama silaha ya kuwalazimisha wapenzi wao wawape yale wanayoyataka.
"Ninapotaka kitu fulani kwa rafiki yangu basi nahakikisha usiku nampa raha zote kisha asubuhi inayofuata namwomba kitu hicho, najua hawezi kusema hapana,’" anasema Anna Tagaru
Hata kwenye maeneo ya kazi wanawake wamekuwa wakitumia njia hii kupata nafasi za juu au kupendelewa na wakubwa.
Kinachofanyika mwanamke anaanza uhusiano na wakubwa katika utawala na hatimaye kama ni mshahara aliotaka au cheo vinaongezeka.
Kwa Tagaru hili kwake si tatizo kama anavyobainisha:"Nawajua marafiki kadhaa wanaotumia ngono kujipatia fedha, si makahaba lakini ni wanawake wanaohakikisha wanapata wanavyovitaka kwa gharama yoyote."
Anasema ana marafiki kadhaa waliotoa miili yao kwa wanaume na kufanikiwa kulipiwa pango katika nyumba wanazoishi, kulipiwa bili za bidhaa na kupewa zawadi za gharama kubwa.
“ Wanaume wanalichulia tendo hili kwa uzito mkubwa na wapo tayari kufanya chochote ili walipate. Kwa kufanya hivi wanawapa wanawake nguvu ya kuitumia ngono kama njia ya kutaka wanayoyataka," anaongeza Tagaru, mama wa mtoto mmoja.
Aidha anasema wakati mwingine anatumia ngono kama njia ya kumpa pongezi au kumwadhibu rafiki yake. Atamfariji kimwili pale anapofanya jambo zuri na pale anapoboronga asahau kama kuna kinachoitwa ngono.
Kuongeza uzao
Hii ni sababu maarufu ya wanawake kufanya ngono na hata dini zimekuwa zikisisitiza hili kuwa mojawapo ya malengo makuu ya kufanya jimai kwa wanandoa.
Hivi ndivyo ilivyo japo leo hii sababu zimekuwa nyingi huku baadhi ya wanawake wa kisasa na wasomi wakitaka tu watoto lakini si kwa kupitia ndoa.
Sikiliza anachosema tena Tagaru"Nilipogundua muda unayoyoma, nilichofanya ni kumtafuta mwanaume anayeweza kunizalisha mtoto mwenye sifa ninazotaka."
Kwa nini tusiwe kama wengine?
Kwa miaka mingi wanaume wamekuwa wakiichukulia ngono kutimiza shauku zao na hata kushindana wenyewe kwa wenyewe kujua nani ana nguvu zaidi. Wapo wanawake nao wanasema kwa nini asiwe kama wanaume?
"Nilipokuwa shuleni, marafiki zangu walikuwa wakizungumzia jinsi walivyotembea na wanaume na kuona uzoefu wa tendo hili, nami nikajaribu," anasema Safia Abdul anayefanya kazi kitengo cha huduma kwa wateja katika kampuni moja ya simu.
Anasema alichotaka ni kuona kwa namna gani angeweza kufika kileleni jambo alilokuwa akilisoma tu vitabuni na hata kuhadithiwa na wenzake.
Alipata alichokitaka kama anavyobainisha: "Nilijaribu kufanya ngono na wanaume kadhaa ili nijaribu kufikia kileleni, nilifanya hivyo hadi nikafanikiwa."
Ushindani wa ngono
Hii inaweza ikawa sababu ngeni lakini ipo na baadhi ya wanawake wanaitumia. Hapa nakusudia kundi la wanawake wanaotoka kwenda kumtafuta mwanaume mmoja mzuri na kisha kila mmoja kufanya awezalo kuhakikisha anafanya naye mapenzi.
Safia anasimulia kuwa hili liliwahi kutokea kazini kwake pale wanawake kadhaa walipokuwa wakimtaka mwanaume mmoja aliyeonekana kuwa mzuri wa umbo na aliyejaaliwa fedha mfukoni. Kila mwanamke akiwemo yeye alimtaka.
“Alikuwa ni ndoto ya kila mwanamke, wote tulitaka kujua atamtongoza nani. Nilipoona kila mtu anamtaka niliamua niwe wa kwanza kumpata kwa gharama yoyote, nilijiuliza hivi kuna njia nyingine ya kumpata zaidi ya ngono?’’
*Makala hii ya Christine Chacha kwa mara ya kwanza ilichapishwa katika gazeti la The Citizen toleo la Novemba 14 ikiwa na kichwa cha habari Why Women Have Sex na imetafsiriwa na Abeid Poyo kwa ajili ya wasomaji wa Kiswahili.
'
HABARI HII NIMEIPATA KATIKA GAZETI LA MWANANCHI.

5 comments:

chib said...

Kazi ipo hapo.
Sikuwa na habari kwenye masuala ya kukomoa.... dah

emu-three said...

Ngono ni ni tendo lifanyalo nje ya ndoa ,na likifanywa ndani ya ndoa linapewa utakatifu wa `tendo la ndo’. Swali je kuna tofauti gani kati ya haya mawili.? Utofauti upo, kwasababu unapofanya ngono hufanyi kwasababu `ni wajibu kufanya hivyo’ ila unafanya kwa malengo Fulani, yawe mazuri au mabaya. Na hapa ndipo tunakita katika swali letu muhimu kwanini wafafunzi wafanye ngono?
Kwanza tuelewe kuwa wanachofanya sio sawa na n i makosa huu ndio ukweli hata kama wasanii wataidhinisha kwa manufaa yao binafsi, labda iwe huyo mwanafunzi kaolewa, hapo hatuwezi kuingilia kati. Kwahiyo hoja yetu sio kwa wanandoa, kwasababu wanandoa hilo tendo sio ngono, ni tendo la ndoa, ni tendo takatifu ambalo kila mmoja anatakiwa alifanye ki-upendo na kuhakikisha kila mmoja analifurahia.
Ama kwa ngono , kwanini wanafunzi wajiingize katika kufanya hilo tendon a baya zaidi wanalitenda kwa wanaume tofautitifauti au kwa wanawake tofauti tofauti. Kwanza kabisa ni `tamaa za kuiga’. Kwasababu kasikia, kasoma au kaambiwa basi atataka ajaribu, na kwa vile ni ngono, huwa haikeshi, inakuwa kama `mlamba asali’. Atalamba kidogo anakuta alichoambiwa sio sawa, atajaribu kwingine na kwingine lakini kama walivyonenena wahenga, nyama zote ni sawa tofauti ni majina ya mabucha. Vinginevyo, ni kujitetea tu, kuwa laabda ni kisasi, kuwa labda naondoa mawazo, hili la mawazo ni sawa na yule anayekunywa pombe akidai kuwa anaondoa mawazo, haondoi ila ana-ahirisha tu!
Je swali ni nani ni chanzo cha ngono kwa wanafunzi, ni wasichana au ni wavulana, kwa hili kila mmoja atavutia kwakwe, lakini kama wasichana watasema `mimi sidanganyiki’ wavulana hawana ubavu wa kuipata hiyo ngono, lakini `bwana mkubwa tamaa, hashindwi kwa ushawishi’

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wewe, hamna tofauti jjati ya ngono na tendo la ndoa bwana

Matha Malima said...

Ni kweli wanafunzi wamekuwa akijirahisi sana hasa karne hii sijui ni kwanini bado sijajua sijui hawaelewi umuhimu wa wao wazazi wao kuwapelka shule .Unajua ukaa ukitafakari hasa mama yako kipato chake cha chini amejinyima kwa kila namana ili mradi mwanae ukasome baada ya kwenda kufanya ulichoendea shule lakini matokeo yake unaenda kufanya ukahaba shuleni kwakweli hii tabia mimi siipendi mpaka wanasababisha hata wazazi kufa kwa plesha wazazi wao wanashindwa kufanya maendeleo ili mtoto asome wao waenda kufnya ufuska kwakweli tabia hiyo siyo mzuri yangu ni hayo .acheni iyo tabia nyie watoto wa shule mnaosomeshwa na wazazi wenu hivi ukipata ukimwi utamlaumu nani? achani kwakweli mnatesa wazazi wenu

cytotec said...

obat cytotec i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat telat bulan