Tuesday, August 24, 2010

Ilikuwa Jumapili ambayo sitaisahau!!

Kanisa la Makwai Lundo hapa ni 2007!!



Nataka leo kuwasimulieni kisa kilichonipata wakati nilipokuwa miaka 8-9 hivi:- Haya ungana nami katika simulizi ya kisa hili.

Ilikuwa siku ya jumapili asubuhi wote tukiwa katika maandalizi ya kwenda kanisani. Kanisa letu la Makwai Lundo (Nyasa). Nadhani baadhi yenu mnajua kuwa baba yangu alikuwa mwl. Ndiyo!! basi kama sikosei kulikuwa ni wakati wa kufanya mitihani. Na baba alikuwa na tabia ya kuchukua kazi zake za shule na kufanyia nyumbani.

Asubuhi hii ilikuwa si nzuri kwangu. Baba alikuwa bafuni akioga, kujiandaa kwenda kanisani. Basi akaja kaka yangu na kuniambia "Yasinta njoo tuangalie hii mitihani tuone nani kafaulu, mmmhh! mimi nikasita nikamwambia mimi naogopa, akasema njoo baba anaoga hatatukuta". Nikanaswa nikaenda kwenye ile meza iliyolundikwa makaratasi ya mitihani na ndio nikawa mpekuzi wa ile mitihani na kaka akawa anaangalia kama baba anakuja? Lakini naye akataka kuona na sasa kukawa hakuna mwangalizi baba huyu akatokea.

Eeeehh! bwana weeee, mzeee alikasirika huyo sikuwahi kumwona. Akamtuma kaka yangu akakate fimbo/kiboko. Nawaambieni hapo nilikuwa natetemeka, jasho lilinitoka na nusu nijisaidia hapohapo. Fimbo/kiboka kikaja, baba akatoa amri Yasintaaaa lala chini na bana kanzu yako akiwa na maana nibane gauni langu. We acha tu, maana kiboko kiliingia hicho tena bado nakisikia, kwa jinsi kilivyodunda.
Je wewe unayesoma unadhani jumapili hii iliisha vipi? Na je? ungekuwa wewe ungefanya nini?

Ni mimi kama kawaida KAPULYA wenu au kama wengine waniitavyo MTEMBEZI. Tukutane tena wakati mwingine!!!!

9 comments:

emu-three said...

Mimi kwasasa nasema ilikuwa Jumapili ya `fundisho kwako' Nasema hivi kwasababu unapokuwa mdogo ukichapwa kwasababu ya kosa fulani unaumia sana, na wakati mwingine kumuona yule aliyekuchapa kama mtu mbaya sana,
lakini unapokuwa mkubwa unaliona lile kosa kiundani na kukiri kuwa kuchapwa kule kumekusaidia,kujifunza zaidi, vinginevyo labda tabia hiyo ungeiona ni ya kawaida, na labda ingekuwa ndio tabia yako, na hatimaye ingekufikisha pabaya.
Labda kama una lengo la kuanzisha mjadala wa `fimbo' e unasaidia kwa watoto.
Fikiria kama isingekuwa fimbo ungelikumbuka hilo tukio?

John Mwaipopo said...

najua kanisani ulikwenda tu kwani kwenda chechi ilikuwa lazima ibada haikupanda vyema siku hiyo, au?

Unknown said...

Kwa upande wangu naona kuchapwa huko si kusaidia wala si kufundisha, kwasababu siku zote jinsi vile mtoto anachapwa ndio jinsi anavyokuwa sugu. Nadhani siku hii ilikuwa si siku ya amani kwako kwani uliumia sana na bakora na sidhani kama kanisani kiliingia kitu manake bakora zinavyoumaga hata kukaa chini hatari sasa nadhani ulikuwa unasikilizia maumivu sema kwa yule aliyesema fundisho, sikubaliani nae, kwani fundisho si kwa kutumia kiboko..unaweza ukakanya na mtoto akakuelewa, kwa upande wetu watanzania,watoto wengi wamekuwa masugu kwasababu ya bakora na mara nyingi haisaidii kwani watoto wengi hurudia makosa.

EDNA said...

Hahaaa mtani wangu umeniacha hoi,ufukunyuku ulikuponza(ukapulya) akachapwa bakora....naona kamwe hutakuja isahau hiyo jumapili.

Penina Simon said...

Aisee Pole sana nadhani sku hiyo ibada iliishia hapo hapo kwenye viboko, na fiiria viboo hivyo nahisi viliuingia kisawa sawa, si mchezo kubana gauni, tena hapo nadhani ukiwa na kichupi tu ndani, Hata muda wa kujiandaa kwa kichapo hukuwa nao, sisi kule kiijini ukijua hesabu zimekupiga chenga na unataraji kichapo kwa mwalimu sku hiyo ulikuwa unajiandaa kwa kuweka daftari matakoni na michupi tele.ili ukichapwa fimbo ziwe zinadunda.

Flora Wanna said...

hellow, dada yasinta pole sana kwa kiboko, nadhani ulikua utoto, na sasa umeacha tabia ya kudanganyika, umenikumbusha mbali sana lundo ndo kijiji alicho zaliwa mama yangu, na hilo kanisa nalifahamu sana, yani nimehisi saivi niko lundo nakula ugali wa muhogo na samaki mbichi,

nakutakia siku njema dada angu.

wakunyumba.

Mija Shija Sayi said...

Hii habari nimeshaisoma sijui mara ngapi, kila nikitaka kutoa maoni naishia kucheka.......dah!!

Anonymous said...

huyo anayesema kuchapa hakufundishi ni mwongo mimi babangu mdogo alinikuta baa zamani sana akanichapa mpakaleo nikitaka kuingia baa nakumbuka siku hiyo amenisaidia kutokuwa mlevi mpaka leo taswira inanijia naogopa.ila kuchapa bila sababu za msingi ndio kunamfanya mtoto awe sugu

cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat cytotec