Tuesday, August 3, 2010

Mawazo/Maswali kuhusu Maisha!!!

Nawaza mwenzenu

Muda mrefy au nisema tangu niwe hapa duniani nimekuwa nikijiuliza maswali haya na bila kupata majibu na leo nimeona si vibaya nikiwashirikisha kwani kama tusemavyo umoja ni nguvu ......!Ni hivi:-

1. Kwanini maisha ni mapambano?

2. Kwanini wengi wanafikiri kuwa wanawake ni tegemezi (sio wote)

3. Hivi tabia inatokana na nini?

4. Na jamani maisha ni nini na kwanini watu tunahangaika ili kuishi?

5. Na mwisho , hiv kwanini mtu unaweza ukawa na pesa na ukaona hazina maana, na kuna wakati mtu unaweza ukafanya jambo la furaha wakati unalichukia je? hapa utasema mtu huyu/mimi nina matatizo?

11 comments:

emu-three said...

Hivi nikuulize unaweza kukaa tu bila kufanya kazi ukapata mahitaji yako? Je uanweza kupata elimu bila kuisomea, je unaweza kula bila kutafuta chakula, hayao na mengine mengi yanawakilisha mambo muhimu yanayokufanya usihi, na huwezi kuishi mpaka uyapate yale yanayokufanya usihi kama chakula mavazi malazi, elimu na vinginevyo, na vyote hivyo havipatikani bila bidiii, na bidii hizo ni mapambano, kwasababu ili upate lishe lazima jasho likutoke, ili upate elimu lazima ubongo uchemke na hata starehe huipati bila kuhangaika eti..
Katika kuhangaika huko, zamani kazi za kutafuta mahitaji zilikuwa kwa baba, na mama anafanya kazi za nyumbani, na kwa vile mahitaji ndiyo yanayoonekana kuwa ni muhimu, na anayetafuta ni mwanaume, basi mwanamke akaonekana kuwa ni tegemezi, lakini ni kwa mtizamo wa hayo yanayoitwa mahitai wamesahau kuwa kuna `malazi’ au sehemu ya kutulia amabyo ni muhimu na hii alikuwa akiifanya mwananmke.
Mwanamke ni nguzo muhimu katika maisha ya kila mtu , kwani ndiye mlezi na mtengenezaji wa mtakabali mzima wa maisha ya watoto, na hapa ndipo chimbuko la tabia linapojengwa.Mama akiwa amejengwa vizuri, akajaliwa na kuenziwa atakuwa na muda mnzuri wa kuitengeneza tabia ambayo jamii inaitaka. Tabia huetegemeana na jamii, na huenda tabia nzuri hapa ikawa sio nzuri kwingine, kwahiyo tabia ni mwenendo unaokubaliwa na jamii husika kuwa ni mzuri au ni mbaya.
Ukiangalia kuhangaika, tabia na mhusiano kwa ujumla ni mihamaniko ya kimaisha, ili tufikie malengo Fulani, na huwezi kuona hayo bila kulinganisha. Maisha ni uhai wako ambao hujengwa na dhamira Fulani, kuwa nifanyeje ili niwe vile kutegemeana na wewe mwenyewe au jamii husika. Ndio maana watu wanahangaika kila kukicha ili kuyafanya maisha yawe bora, na ubora huo unapatikana kwa kulinganishana.
Katika kuyahangaikia maisha ndipo watu wakagundua kitu kinaitwa pesa, hiki mwanzoni hakikuwepo, ila baadaye waliona badala ya kugawiana chimvi kwa mkate basi kuwe na kiwakilishi cha thamani sawa na vitu, ndipo pakazuka kitu pesa. Na asikudanganye mtu kuwa ana pesa zinazokosa la kufanya, na sijui kama kuna mtu ameridhika na pesa aalizo nazo, kama yupo mbona halali tu na kufanya ibada kumshukuru aliyempa toka asubuhi hadi jioni, wapo kweli hawo watu, sijui!
Labda niishie hapa

emu-three said...

Hivi nikuulize unaweza kukaa tu bila kufanya kazi ukapata mahitaji yako? Je uanweza kupata elimu bila kuisomea, je unaweza kula bila kutafuta chakula, hayao na mengine mengi yanawakilisha mambo muhimu yanayokufanya uishi, na huwezi kuishi mpaka uyapate yale yanayokufanya uishi kama chakula mavazi malazi, elimu na vinginevyo, na vyote hivyo havipatikani bila bidiii, na bidii hizo ni mapambano, kwasababu ili upate lishe lazima jasho likutoke, ili upate elimu lazima ubongo uchemke na hata starehe huipati bila kuhangaika eti..
Katika kuhangaika huko, zamani kazi za kutafuta mahitaji zilikuwa kwa baba, na mama anafanya kazi za nyumbani, na kwa vile mahitaji ndiyo yanayoonekana kuwa ni muhimu, na anayetafuta ni mwanaume, basi mwanamke akaonekana kuwa ni tegemezi, lakini ni kwa mtizamo wa hayo yanayoitwa mahitai wamesahau kuwa kuna `malazi’ au sehemu ya kutulia amabyo ni muhimu na hii alikuwa akiifanya mwananmke.
Mwanamke ni nguzo muhimu katika maisha ya kila mtu , kwani ndiye mlezi na mtengenezaji wa mtakabali mzima wa maisha ya watoto, na hapa ndipo chimbuko la tabia linapojengwa.Mama akiwa amejengwa vizuri, akajaliwa na kuenziwa atakuwa na muda mnzuri wa kuitengeneza tabia ambayo jamii inaitaka. Tabia huetegemeana na jamii, na huenda tabia nzuri hapa ikawa sio nzuri kwingine, kwahiyo tabia ni mwenendo unaokubaliwa na jamii husika kuwa ni mzuri au ni mbaya.
Ukiangalia kuhangaika, tabia na mhusiano kwa ujumla ni mihamaniko ya kimaisha, ili tufikie malengo Fulani, na huwezi kuona hayo bila kulinganisha. Maisha ni uhai wako ambao hujengwa na dhamira Fulani, kuwa nifanyeje ili niwe vile kutegemeana na wewe mwenyewe au jamii husika. Ndio maana watu wanahangaika kila kukicha ili kuyafanya maisha yawe bora, na ubora huo unapatikana kwa kulinganishana.
Katika kuyahangaikia maisha ndipo watu wakagundua kitu kinaitwa pesa, hiki mwanzoni hakikuwepo, ila baadaye waliona badala ya kugawiana chimvi kwa mkate basi kuwe na kiwakilishi cha thamani sawa na vitu, ndipo pakazuka kitu pesa. Na asikudanganye mtu kuwa ana pesa zinazokosa la kufanya, na sijui kama kuna mtu ameridhika na pesa aalizo nazo, kama yupo mbona halali tu na kufanya ibada kumshukuru aliyempa toka asubuhi hadi jioni, wapo kweli hawo watu, sijui!
Labda niishie hapa

MARKUS MPANGALA said...

somo limetua mahali pake hili. uliwaza nini Yasinta?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

maswali yako ni mazuri najaribu kuyajibu nikiwa na uchovu mkali wa safari, ila ilibidi swali la nne liwe la kwanza, mimi siamini kama maisha ni mapambano, naamini maisha ni masiha, upambane usipambane utaishi tu, ila wengi tumeamua kupambana tu. pesa sio kila kitu, kumbuka furaha, amani, upendo na mafanikio vimo ndani mwetu na sio nje yetu kama vile pesa nk

sidhani kama watu wanahangaika kuishi bali wanaishi. maisha yetu yamekuwa ya kukimbiza kilichombali na kuendelea kung'ang'ania kile ulichonacho japo hakihitaji, tunaishi jama na tunaishikesho na kuacha kuisha 'SASA' ambayo ndiyo tuliyonayo! ndio maana maisha yanakuchanganya binti, take it easy usijekunywa thumu

Sisulu said...

MAISHA NI MAISHA KWA SABABU YANAISHA tutaishi tutaisha, furaha halisi yatoka kwa mungu na kuujua ukweli wa maisha yetu, pesa huunga mkono maisha na si chanzo cha FURAHA, ndio maana watu wengi walio na pesa huchelewa kulala na huwahi kuamka.Katika maisha kumbuka, Jiographia hutufanya majirani, Historia hutufanya marafiki,Uchumi hutufanya wenzi, na mahitaji hutufanya washirika. ujumbe ndio huo. ASANTE

Penina Simon said...

1. Maisha nimapambano kulingana na maagizo ya Mungu, Kila mtu afanye kazi, (1) Apate rizik (2) Kuweka mwili wako fiti
2. Wana matatizo kiakili (Kama ni wanawake hawajiamini) (kama wanaume wana roho mbaya)

3. Inatokana na jinsi mtu unavyojiweka (jitume)

4. Maisha ni uhai, na lazima uhangaike ili uwe hai, (huwezi kaa ukawa unashushiwa riziki)

5- Mambo yote haya bila kuwa na Mungu huwezi kuwana amani wala mtu wa kujiamini,hebu piga hatua kwa Mungu uone

Matha Malima said...

1.maisha nimapambano kwasababu kilamtu ambaye amejipangia malengo yake katika maisha lazima ayatimize malengo ambayo emepanga yatatimia kutoka na jinsi gani avyoangaika katika kazi yake na katika familia yake

2.kwanza nianze kwa wanawake ambao si tegemezi hawa wao lazima uwe na changamoto yamaisha katika familia hata katika maisha ya ujana kwasababu unapokuwa mbunifu katika kuangaikia maisha na hatakumpa ushauri mumeo wa maendeleo katika nyumba nadhani sidhani kama atakataa kwakuwa ajajua kile kitu hata kama atafanya mwanamke unakuwa ni kwa faida ya wote katika familia.Lakini wale wanawake tegemezi wanakaaa wanasubiri mwanaume kila kitu akusogezee hapo ndani mawazo hutowi yoyote ya kushauri kuwa na maendeleo na mipangilio ya maisha yas watoto kusoma wa kujiongeza chochote kimaisha kwakweli wanaume nao wanachoka. si lazima uwe na duka uza hata mboga nyanya,unajua wanawake wengine wajua kuwa na duka au bishara kubwa ndio maisha lakini haksuna waote huwa tunaanzia chini kuja juu. na ndio maana wanaume wengine awaoni umuhimu wa kushirikishwa katika mambo mbalimbali.
3.Tabia ya mtu inatokana jinsi alivyolelewa ,kwanza huyo mtu kalelewamalezi gani kama mtoto alikuwa anaiba toka utoto iyo tabia tegeme kuwa hata akikuwa hata waza kutafuta kazzi ili iweze kumpatia kipato ili aweze kujikimu na maisha yake yeye awaza kuiba tu ,na kama mtu anatabia mbaya hata umrekebishe hataweza kujirudi ili aaache hicho kibaya anacho kifanya.
4. Maisha ni jinsi mtua avyopangilia mipango yake ili aweze kufanikwa.watu wana hangaika ili waweze kukimu mhitaji yetu ya kila siku sidhani dunia ya leo wapo ambao wanapendakuukaa bila kujishughulisha.huku arusha kuna vijana wajituma sana kwanza wao kazi ni kupandisha wazungu milimani na wakirudi huko wanajishughulisha na kunyoa saloon kwakweli wanajituma hata mpaka walkimuona mtu amekaa hafanyi kazi wasnamwonea huruma sana.
5.unaweza ukawa na pesa lakini huma amani kuna watu woko tayari auwe ili apate pesa hivi mtu kama huyo si dhani atakuwa nmani katika yake mngine anakuwa na pesa lakini pesa hizo zinamasherti ya kiushikina utashangaa mtu anaela anatembelea ndala mpaka anakufa huwezi ukamkuta amevaa nguo nzuri au kula vizuri hawa watu wanashida sana.
huyu mtu kwakweli atakuwa na matatizo na ni wakumsaidia .

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mmh! Penina, yaani ushaanza mpaka kumsingizia Mungu?

Haya, mwee! Hayo yote si uhalisia bali utopia tu!

Unknown said...

Nimejifunza jambo humu.......

chib said...

Mimi nimeamua kutowaza lolote, labda kwa sababu nimetingwa sana na kazi

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote na msichoke kuitembela maisha na mafanikio- Wote mnapendwa.