Sunday, August 29, 2010

Jumapili ya leo, Mke: Furaha ya mume wake!!!

Mwanamke ni furaha ya nyumba!!

Kitabu cha Mithali kinaeleza jinsi mwanamke mkamilifu alivyo, mwanamke aliye furaha na fahari ya mume wake. Mwanamke huyu anafanya kazi zake kwa bidii, ana hekima ni mwaminifu na hutunza kwa uangalifu watu na vitu vya nyumbani. (Mit. 31:10-31)


Kitabu kingine, Hakima ya Yoshua bin Sira, kinamsifu mume mwenye mke wa namna hiyo:-

Apataye mke hujipatia mali iliyo bora, msaidia wa kufaa, na nguzo ya kumtemeza. (Y. b. s. 36: 24).


Yu heri mume aliye na mke mwema kweli,

Mwanamke mwema ni furaha ya mume wake,

Ataishi miaka ya maisha yake katika amani.

Mwanamke mwema ni tunu bora,

Mcha Mungu atatunukiwa huyo watajaa furaraha moyoni hata kama ni maskini au tajiri,

Watakuwa na nyuso zilizochangamka wakati wowote. (Bin Sira 26: 1-4)


Hivi ndivyo mwanamke anavyokusudiwa kuwa kwa mwanaume. Katika maneno yake Mungu kwa nabii Ezekieli, mwanamke huwa; "Furaha ya macho". (Ez. 24-16).

Lakini kwa nabii Hosea, mke huyu aliyekusidiwa kuwa furaha yake, amekuwa chanzo cha mateso ya uchungu wake. (Hos. 2: 4-9) mke huyu hana uaminifu naye huenda kwa wanaume wengine. Amina!!

NAWATAKIENI WOTEEE JUMAPILI HII YA MWISHO YA MWEZI HUU WA NANE IWE NJEMA NA PIA BARAKA ZA MUNGU ZITAWALE NYUMBANI MWAKO/MWENU NA POPOTE PALE U/MTAKAPOKUWA.!!!!



8 comments:

EDNA said...

kwako pia mdada Mungu awe pamoja nawe.

Bennet said...

Nyumba ambayo ina mke, akisafiri siku mbili tu ukiingia ndani utajua kwamba hayupo

Na kama utapata mke mwenye malaria isiyooisha kichwani halafu ana mdomo mbona hata nyumba utaiona chungu

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mmmh!

Koero Mkundi said...

Bennet na nyumba isiyo na mume je?

emu-three said...

Mke mwema au mume mwema, haviji kwa maneno tu, kunahitajika huo uwema na wema uwepo kwa vitendo. Nakumbuka jamaa mmoja alisema hivi;
Mke au au mume sio gogo la kuchanga,
Kwani lingelikuwa gogo, angalau ningelichoka kinyago.
Imeniwia kinyongo, na tamaa kuniishia, kwani nilyemdhania mliwaza, kageuka kuwa sanamu.
Haitikisiki wala havutiki, kila kitu nifanye mimi.
Aheri lingelikuwa gogo, ningelichonga kinyago.
Huyu mtu anamuelezea mpenzi wake, kuwa hajishughulishi, yupo gogo, kila kitu anaachiwa yeye, ni aheri angelijua kuwa kapata gogo, hilo anajua lipo tu, na ubora ulifanyie kitu kingine kama kuchonga kinyago.
Huo ni ujumbe kuwa mke mwema au mume mwema ni yule anayetimiza wajibu wake kama mke au kama mume!

MARKUS MPANGALA said...

Nawaangalia tu maana sijui mke wangu nani, maana hata nikisema kwa sifaze, kwani bado hajawa mke wangu jamani, kwa hakika nataka kuona yeye ni nani, na kwanini yuko nami na siyo mtangu wangu Fadhy. Ngoja niwaangalie tu mnavyonipa elimu hii...... LAKINI NITAOA NITAKAPOTAKA

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

haya maandiko mnayoyasingizia kuwa maneno ya Mungu ni ajabu, eti mke ni mali?? sikubali na sidanganyiki kjwa hili, mke wangu sio mali

Matha Malima said...

nashukuru sana kwa ujumbe mzuri kwakweli unatutia moyo sana ubarikiwe na asante kwa kunipa maneno ambayo naweza kuwatia moyo wanawake wenzangu