Thursday, May 14, 2009

WATU WENYE MTINDIO WA UBONGO NAO NI WATU KAMA SISI

Ni watu ambao akili zao zinachelewa kukua. Mtu mzima, mwenye miaka 60 lakini utamwona akili yake ni kama mtoto wa miaka 3. Kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana:- Nasema hivi nikiwa na maana nilikuwa nyumbani TZ. Niliwahi kuona watu wengi wenye watoto wenye mtindio wa ubongo walikuwa wakiwaficha ndani ya nyumba kwa kuona aibu.

Baadaya ya kuishi hapa kwa muda huu nilioishi, nimefanya utafiti na kugundua ya kwamba sisi waAfrika/waTanzania. Kila kitu tufanyacho tupo nyuma yaani tunafanya baada ya wenzetu/Ughaibuni kupiga hatua mbele. Nasi tunafuata nyuma. Ni hivi katika utafiti wangu wao/Ughaibuni pia hapo zamani walikuwa wakipata mtoto mwenye mtindio wa ubongo waliona aibu na hawakumtaka yule mtoto. Walimpeleke kwenye nyumba maalumu. nyumba ya watoto "YATIMA". Ilikuwa ni kinyume na Afrika/TZ wao waliwatunza wenyewe ila hawakutaka waonekane.

Lakini sasa hapa niishipo wenye mtindio wa ubongo wote wanaruhusiwa kufanya chochote kile kutegemea na ulemavu gani anao. Wanaruhusiwa kwenda shule, yaani shule maalumu, wanafanya kazi kulingana na uwezo wao, wanaishi kwenye ghorofani "peke yao" huku wakisaidiwa na wafanyakazi yale mahitaji muhimu. Wamekuwa ni watu wa "kawaida" katika jumuia.

Tanzania pia wamefikia hatua kubwa kidogo ukilinganisha na miaka ya 1980. Kuanzia miaka ya 1990 kulikuwa/kumekuwa na shule ya wenye mtindio wa ubongo. Ila sasa tatizo ni kwamba wakishamaliza pale wanawaacha tu. Hakuna anayewajali watu hawa. Kwa mtazamo wangu naona wao wanaumuhimu wa mahitaji kama sisi wengine. Kwa sababu hawa hawahitaji kazi ya maana sana. Kinachotakiwa ni vijikazi vidogovidogo. Yaani kuwepo na sehemu (nyumba/jengo) ili wawe wanaenda kufanya kazi hata masaa mawili kuliko kuwaacha tu. TUSISAHAU YA KUWA BINADAMU WOTE NI SAWA!!!!

6 comments:

Anonymous said...

Hakuna anayechagua kuzaliwa na hitilafu. Swala hili ni swala muhimu sana na inabidi tuwache kusubiri wengine watatue tatizo hili la kuwaficha hawa watoto. Kiini cha kufichwa ni nini? Aibu kwa maana wazazi hawataki kuwaona watoto wao/wao wenyewe wakichekelewa na majirani... stigmatization bado ipo Africa!

Unknown said...

somo zuri sana yasinta.
Ahsante kwa kutuelimisha

Fadhy Mtanga said...

Nakubaliana na Serina kuwa stigmatization ipo kwa kiwango kikubwa Afrika.
Ahsante sana dada kwa zomo zuri.

Unknown said...

Hongera Yasinta kwa Uchambuzi wa Makala hii nzuri.

Koero Mkundi said...

Kuna kitu nimejifunza katika somo hili. Keep it up dada!

Anonymous said...

Hili ni somo elimishi kwa jamii yetu hasa kwa jinsi ambavyo umelinganisha baina ya jamii mbili zenye nadharia na mienendo inayotofautiana. Ama kwa hakika ni vyema kusema kuwa watu wenye mtindio wa ubongo wapewe haki na heshima kama ilivyo kwa binabamu mwingine yeyote. Suala la ugonjwa au hitilafu lisiwe sababu ya kuwabagua bali kigezo tosha cha kuwakamilisha kutokana na ukamilifu tuliojaaliwa kuwa nao. Msemo wa 'hujafa hujaumbika' unaleta maana katika hali ya kufanana na hii kwani inawezekana kabisa aliye mzima leo akapata ulemavu wa ajali ama kasoro za maisha na akalazimika kuwa mhitaji pengine hata kupita uhitaji wa mtu mwenye mtindio wa ubongo.
Tumeumbwa kwa namna tofauti kila mmoja wetu akiwa mapungufu yake ambayo mara kwa mara hukamilishwa kwa kiasi na binadamu mwingine. Ndiyo kazi ya uumbaji tena, hakuna aliye mkamlifu, ikiwa yupo mkamilifu katika dunia hii basi duniani hapa si mahala pake kwa kuwa sisi sote tunahitajiana kwa hili ama lile kuufikia ukamlifu.

NB: Ni jambo la heri kusoma maoni ya walionitangulia.