Friday, May 8, 2009

MWENZENU LEO NIMEAMKA NA KUMKUMBUKA KWELI MAMA YANGU

8 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Maoni haya niliyaweka katika post yako ya "Sitausahau mwaka 2005..." na hapa naomba kurudia sehemu yake...

Ninachoweza kusema hapa ni kwamba pengine mama yupo kwenye furaha na anakutakia furaha na mafanikio wewe binti yake pamoja na wajukuu zake. Tekeleza aliyokufundisha na zingatia yote aliyoyapenda, fanya alichotamani, shukuru kwa muda uliokaa naye (wengine hata hatukupata bahati ya kuwaona na kuwajua mama au baba zetu) na utaweza kuishi naye daima katika maisha yako na hao wajukuu zake. Kama anavyosema Da Mija - wewe ni mwanamke wa shoka na ndiyo maana badala ya kupondekapondeka, kama askari shujaa ulinyanyuka, ukafuta machozi mashavuni mwako na kusonga mbele! Endelea kufanya hivyo na mama huko aliko ataendelea kufurahi!

Yasinta Ngonyani said...

Asante sana najisikia raha kidogo na nahisi mama yupo nami Ubarikiwe maneno yako yamenifariji.

Mwanasosholojia said...

Dada Yasinta, naanza kwa kusema hakuna kama mama!Kuna wengine huwa nashindwa kuwaelewa wanapowadharau na kuwabeza mama zao! Nafikiri wana matatizo watu wa namna hiyo. Ni hivi karibuni tu nilipewa taarifa kuwa mama yangu ana hali mbaya na amefanyiwa operesheni ya intestinal obstruction hospitali ya Muhimbili Dar es salaam, wakati mimi nipo masafa kibao huku ughaibuni!Kusema ukweli nilijawa na majonzi sana na kuna kipindi nilibubujikwa na machozi hasa nilipokuwa napewa taarifa kuwa ana hali mbaya! Wimbo wa Song for Mama wa Boyz II Men ndio uliokuwa unanifariji kila mara, pamoja na rafiki zangu. Sishangai wewe kumkumbuka mama, ni haki yako kwani hakuna kama mama!

PASSION4FASHION.TZ said...

Pole sana Yasinta nazani mama alikutembelea,kama alivyosema kaka Masangu endelea kumuomba mungu na endelea kutekeleza mafundisho yake.do

Mzee wa Changamoto said...

Pole Dadangu. Pole saana. Ntakuwa wa ajabu kwa haya nitakayosema lakini naamini kwa wema wake nitaeleweka. Kwanza niseme kuwa kumkumbuka Mama kwa namna umkumbukavyo inaonesha kuwa alitenda mengi wakati wa uhai wake. Hii nayo ina maana nyingie kuwa MAMA alimaliza kazi yake na kwa hakika pamoja na kuwa tulikuwa tunamuhitaji, ulikuwa ni wakati wake kupumzika. Na kilicho cha ziada ni kuwa amekuachia mafunzo ambayo twaaminbi unayapitisha kwa wanao. Basi ni wakati mgumu. Wakati wauitao "bitter-sweet". Wakati tunaokumbuka kuwa kila mtu ana wajibu wake duniani na akiumaliza ataondoka. Tatizo ni kwamba watendao mema ndio tuwahitajio zaidi na wakishatenda mema ina maana wamemaliza huduma yao ulimwenguni. Ni vema kuwa wametenda waliyotakiwa kutenda na ni ngumu kukubali kuondoka kwao, lakini bila kufanya hivyo tutakuwa hatuenzi juhudi zao nyiingi walizoweka kwetu.
Mimi mpaka leo nasikitika kuwa nilimlilia Mjomba wangu mpenzi. Na bado nalia kuwa nilimlilia maana naona kuwa sithamini magumu menbi aliyopitia kufanikisha aliyofanikisha.
Sasa najua kuwa njia pekee ya kuwaenzi wanaotenda mema ni kukubaliana na muda wao wa kupumzika. Nasi kuanza kuwaenzi kwa kutenda mema na kuwekeza katika yale waliyotuachia.
MAMA ANAKUPENDA DADANGU na ndio maana unakuwa naye kiroho. Ni kwa uwepo wake unaweza kumhisi na kulala kisha ukaamka na hisia juu yake.
Mama ametenda, na sasa anapumzika pembeni yako. Nasi twamuomba apumzike kwa amani na tunaendelea kushirikiana yale mema watufunzayo.
PUMZIKA KWA AMANI MAMA

Yasinta Ngonyani said...

Asante sana wote mnajua hii huwa naumia sana kwa vile siku ya mazishi sikuwa nyumbani na ilikuwa ghafla

Born 2 Suffer said...

Hakuna kama mama jamani, Mama ni mama hana mfano.

mumyhery said...

Yasinta ndugu yangu pole kwa yote, yaani yote yameisha ongelewa na walio tangulia kutoa maoni, kuhusu mama sipati neno la kuelezea ila basi tu nafikiri nikisema hivyo unanielewa nina maana gani, we acha tu