Wednesday, May 20, 2009

KATIKA MAISHA NI VIZURI KUWAFARIJI MWENYE MATATIZO

Huu ni ushauri wangu mimi kwa wewe uliye na rafiki aliye na matatizo:-

1) Kama rafiki yako ana matatizo usiogope kumwuuliza hali yake kwa ujumla hata kama hali yake inaonekana si nzuri. Kama una matatizo halafu watu/marafiki wanakuuliza U HALI GANI utajisikia amani yaani kuna watu ambao wanakujali haupo peke yako.

Wakati mwingine kunatokea mambo, ambayo si kweli na watu wanafikiri kuwa tayari yule mwenye matatizo amepata msaada. Yaani mtu wa kuongea naye. Wakati kumbe wewe upo peke yako kwa hiyo kuuliza ni muhimu sana.

2) Piga simu au nenda ili kujua mpatwa matatizo ana hali gani. Pia pika chakula, nenda kwake na mle pamoja. Wakati matatizo yanapotokea, inakuwa ngumu kuelezea vitu ulivyozoea kufanya kila siku. Kama una watoto inakuwa ngumu zaidi kuwatunza wakati upo kwenye matatizo/majonzi. Kwa hiyo ni vizuri kusaidiana.

3) Onyesha upendo wako, bila kuonekana ni usumbufu kwa mpatwa matatizo, uwe nusu nusu. Usizidishe au usipunguze. HAPO NDIPO UTAWEZA. Kama nilivyosema hapa juu huu ni ushauri wangu mimi.!!!!

7 comments:

EDWIN NDAKI (EDO) said...

ni kweli tunani tunabidi kuwatendea meam marafiki na hasa hasa watu ambao tunatofauti nao(conflict) maana tutakuwa tunafanya jambo la heri zaidi kuwaleta karibu wenzetu na kupata amani ya kweli.

asante kwa soma nzuri

Fita Lutonja said...

Ok well done keep it up!! I enjoy it so much. It is become aesthetic for me.

Nampangala said...

Mlongo maneno yako ni matamu ni kweli unavyosema ni vizuri kutakiana khali na kuwatembelea malafiki na jamaa zako wakati wanaokuhitaji zaidi. Mlongo mimi niliuguliwa na mwanangu apa Dk na nilifalijiwa sana na watu wenye imani na upendo walitutembelea hospitalini na mwenyekiti wa chama cha watazania apa dk hakuchoka kuja na biblia yake kumuombea mwanangu kweli nilijifunza mengi sana wakati nilipokuwa na kipindi hicho kigumu kwangu mimi na mume wangu. Ndio maana nafurahi kuona katika ukulasa wako huu unashauri vitu kama hivi. chabwina sana mlongo wangu.

Bennet said...

Ni kweli ukiwa na matatizo maneno ya faraja hupunguza uchungu na kujisikia nafuu.
lakini wakati wa kutoa maneno ya pole na kukufariji kuna wengine hawajui namna ya kukufariji, yeye akifikiri anakupa pole na kukufariji lakini maneno yake badala ya kukupooza na kukusahaulisha matatizo yako yanazidisha uchungu ingawa si makusudi yake.

Christian Bwaya said...

Nimejifunza kitu kipya. Asante

Yasinta Ngonyani said...

Asante wote kutakana hali ni vizuri sana na ni kweli inawezekana unaweza ukasema na ukakosea bila kuwa na lengo. Ni vizuri kusaidiana wakati wa raha na shida. Rafiki ni bara kuliko mwanasesere:-)

chib said...

Ushauri wako wapaswa kuzingatiwa haswa. Tunakushukuru Da Yasinta