Friday, May 22, 2009

HIVI KWELI FURAHA NI KITU ADIMU?

Mara nyingi napatwa na hasira sana na pia uchungu.Yaani ninaposikia watu wanasema, fulani yule anaishi maisha mazuri mwenzetu. Yaani watu wanafikiri kuwa na gari nzuri, nyumba nzuri nguo nzuri basi akili zao zinawatuma ya kuwa huyu mtu/mwenzetu sio mwenzetu ana furaha na pia raha sana. Kwa kweli sio hivi:- unaweza ukawa na vitu vyote hivyo na ikawezekana maisha yako hayana furaha. Kwani FURAHA sio vitu.

1. Furaha ni kuwa na marafiki/rafiki wenye/mwenye furaha.

2. kuwa na furaha unaweza ukawa na furaha hata kama huna mali yaani vitu vizuri. Nina maana FURAHA NI MUHIMU KULIKO PESA.

3. Pia furaha ni kuamka kila asubuhi na kujua kuwa ni mzima wa afya pia kuwa na familia ambayo inakujali na kukupenda wewe kama wewe.

Mtu /watu mwenye/wenye furaha huishi maisha marefu.

2 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Unajua watu wanapenda njia za mkato. Wanachanganya kati ya kifo na usingizi, furaha na rindiko la mali na hata ulinzi na amani. Yaani watu wanaamini kuwa ukiwa na askari wengu una amani, wakati ukweli wa mambo ni kuwa una askari wengi kwa kuwa hauna amani. Wanasahau kuwa kuwa na mali nyingi kunakufanya ukose uhuru wa kuwa mtumiaji huru na matokeo yake badala ya kutumia kwa kuwa unahitaji, unatumia kwa kuwa unazo.
Mali na furaha ya kweli ni vitu ambavyo si mara zote huenda pamoja.
Kila kitu chahitaji kuwa na "kiasi" na kwa kuvuka "mpaka" wa kiasi hicho, basi unakuwa unaelekea kwenye mateso na kadhia.
Blessings

Yasinta Ngonyani said...

Yah! nakubaliana nawe Mzee wa Changamota "Mali na furaha ya kweli ni vitu ambavyo si mara zote huenda pamoja". lakini utakuta wengi wanafikiri wakiwa na mali watakuwa na furaha.