Friday, June 6, 2008

Juni 6, 2008 Afrika inahamaia Ughabuni

Sasa hali ya hewa hapa Sweden kama nyumbani Afrika. Kusema kweli sijui wapi ni nyumbani kwangu nikiwa hapa nasema nakwenda nyumbani na nikiwa TZ (Ruhuwiko) nasema nakwenda nyumbani yaani hapa sweden. Ebu nisiwachoshe na hayo ya kutojua wapi ni nyumbani kwangu. niwasimulie ambacho nataka kuandika, ni kwamba leo nimefurahi sana, kwanza kabisa ni kwamba nimekula samaki najua mtashanga ni nini cha ajabu kula samaki hapana sio hivyo ni samaki wa kutoka ziwa nyasa amesafiri mpaka huku. Pia furaha imeongezeka kwani nimenunua majani ya viazi yaani matembele(kilugha nabwaka) Najua wengu wanaona nimepungukiwa hapana nina zangu timamu kabisa. Ni hivi mwanzoni nilipata sana shida yaani nilikuwa natamani sana vyakula vya nyumbani TZ hasa samaki na ugali. Lakini sasa naweza kununua hadi majani ya viazi, karanga, mihogo, ila bado sijaona njugu au mboga ya mabogo(kilugha likolo la nanyungu) na kisamvu hivi navitamani sana. Kwa hiyi ninaweza kupata karibu kila aina ya chakula. Lakini hata hivyo havinogi kama vya nyumbani(TZ) kwa sababu ni safiri ndefu mno mpaka kufika huku pia kama samaki sio moja kwa moja toka ziwani. ukitaka kujua ukweli nenda hapo lundunysa.blogspot.com atakuambia utamu wa vyakula hivi.

Na; Yasinta Ngonyani

3 comments:

Anonymous said...

Nimefurahi sana kwani naamini imesuuza moyo wako wala hujakosea kufurahi ndugu yangu.Yaani nilishangaa kidogo vipi mbona dada anasema afrika imehamia ughaibuni?kumbe utamu wa nyumbani umezidi kipimo,yaani umekukuna sana.Haya kazana lakini hivi huko kuna kauzu?.Vipi dagaa wapo?kama hawapo pole sana.mimi ninakucheka kwa kukosa uhondo lakini mmm nicheke nina mwanya?..

Anonymous said...

kula ni kula mbaya kukomba mboga au mnasemaje wenzangu?hee yaani hizi mboga ukija nyasa ni utamu mtu..

Yasinta Ngonyani said...

Markus ndugu yangu we cheka tu. Hakuna kauzu wala dagaa nyasa ni kweli nakosa sana uhondo. Lakini kwa sasa ninao kauzu nilikuja nao nilipokuwa huko nyumbani mwezi wa kumi na mbili. Bahati mbaya nilisahau mbegu za mabogo na mchicha pia figiri.