Saturday, June 21, 2008

JUNI 21, 2008 UBAGUZI WA RANGI

Bado sielewi kwa nini binadamu tunabaguana, Kwa nini wazungu wanaona wao ni bara zaidi kuliko watu weusi. Wakati wote tukiumia au kujikata maumivu ni yale yale, pia wote damu inatoka. Wakati mwingine unaweza kufikiri ya kuwa kuna mungu wawili au niseme wao wanafikiri hivyo mungu mzungu na mungu mwafrika. Kwani zamani nilikuwa nasikia tu ya kwamba kuna ubaguzi nilikuwa sielewi, lakini sasa naelewa kwani naona mwenyewe kwa macho yangu. Halafu sasa sio wanwabugua watu weusi tu hapana wote ambao si wazungu kwa mfano waarabu, wahindi, wachina n.k.. Yaani wanaogopa hata kukua jirani wakati mpo kwenye basi anakubali kusimama kuliko kukaa siti moja na mwafrika. Wao wanasema wanaogopa wakikaa siti moja basi wao pia watabadilika na kuwa weusi. Wakati mwingine hata kusalia wanaogopa, yaani kushikana mikono. Nasema tena kwa uchungu mwingi sana inaumiza sana tena sana kuona watu wana roho mbaya kiasi hiki. Kwa hali hiyo mtu kila siku unaishi tu yaani siku ikiisha shukuru mungu. Natamani ile ndoto ya Mrtin Luther King ingekuwa kweli, kwamba siku moja mtoto mzungu na mtoto mwafrika watashikana mikono na watacheza pamoja. Je? wasomaji ni kweli sisi waafrika tupo nyumba sana kwa kila hali(jinsi)? Sababu gani wao wanasema waafrika ni wajinga wanakaa tu wanasubiri kupewa wao ni wajinga HAKUNA MTU ANAWAAMBIA WAAFRIKA WANGU WAJINGA. Kwa kweli naumia sana

Na; Yasinta Ngonyani

No comments: