Kila nikijaribu kusoma maandishi haya "Mpumbavu ni Mpumbavu 2 awe amesoma au hajasoma" nahisi kichwa changu kama kimechoka vile na mwisho nimeona afadhali niweke hapa kwani kila wakati palipo na wengi hapaharibiki neno... Halafu baada ya muda nakutana ....Friday, May 6, 2011
TAFAKARI YA IJUMAA HII YA LEO!!!
Kila nikijaribu kusoma maandishi haya "Mpumbavu ni Mpumbavu 2 awe amesoma au hajasoma" nahisi kichwa changu kama kimechoka vile na mwisho nimeona afadhali niweke hapa kwani kila wakati palipo na wengi hapaharibiki neno... Halafu baada ya muda nakutana ....Thursday, May 5, 2011
HIVI HARUSI "NDOA" NI NINI?

Picha hii ya kwanza mnaona wanaharusi ni harusi rahisi kabisa unadhani unaweza kufahamu yupi ni bibi harusi na yupi ni bwana harusi. picha toka kwa kaka Mjengwa
Na picha ifuatayo ni harusi "ndoa" iliyofanyika Ijumaa iliyopita kati ya Prince William na Kate.
Wednesday, May 4, 2011
HONGERA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA KAKA MANYANYA PHIRI!!!
Hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa na kubwa zaidi HONGERA KWA KUTIMIZA MIAKA 50. Kaka huyu siku ya kwenza kabisa kuingia katika blog hii ya Maisha na Mafanikio ilikuwa mwanzoni wa mwaka huu ilipokuwa siku yangu ya kuzaliwa kwa hiyo nami nimeona sina budi kumpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa. HONGERA!!! Ukitaki kumzoma kazi zake unaweza kumtembelea:- goodmanmanyanyaphiri.blogspot.comNajua wengi mtajiuliza huyu Kapulya alijuaje kama Kaka Manyanya anatimiza miaka leo? Ndiyi! nikwamba baada ya kutoa maoni yake katika mada hii ndo nilipogundua hili na nikaona ni kheri tumpongeze. http://ruhuwiko.blogspot.com/2011/04/yale-tuyaitayo-mabaya-ndiyo-hutufunza.html
Goodman Manyanya Phiri said...
Wewe Yasinta unatoka dunia gani? Mbona kila ukitoa kauli ni uhai mtupu? Ubarikiwe sana, Mwanadada!
Umekuwa malaika kwa wengi kutokana na nguvu za kalamu yako. Hasa kwangu nakuona malaika.
Saa iliopita nami nikiwa natangatanga jijini Pretoria kwa matatizo yangu mepya, nilikuwa nawaza: "kwanini maisha yangu Manyanya mie tangu ujana (16) hadi leo... tarehe 4 mwezi ujao (MAY) ninakuwa 50... ni vita tu na vita tupu?"
Hapo nikakumbuka maneno kuhusiana sana na msemo wako [kujifunza katika shida]...maneno kama haya http://pravstalk.com/pravs-world-gods-cup-of-tea/
["WE ARE LIKE TEABAGS, WHOSE STRENGTH COMES OUT WHEN WE’RE PUT IN HOT WATER. SO, WHEN PROBLEMS UPSET YOU… JUST THINK, YOU MUST BE GOD’S FAVOURITE CUP OF TEA!"]
Yule Mungu amekunywa ujana wote wangu... karibu nimtukane: "..Shenzi TYPE!". Lakini sitayasema hayo Kwake kwakuwa Yeye ni Muumba kwangu na malaika wake kama Yasinta wapo chungu mzima kunikumbusha [yote yanania na mwisho Kwake].
Hivi ndivyo nilivyogundua kuwa kaka Manyanya Phiri anatimiza miaka leo 4/5......
HONGERA SANA KWA KUTIMIZA MIAKA 50 MWENYEZI MUNGU AKUONGEZEE MIAKA 50 TENA NA PIA ZAIDI...!!!!!!
Monday, May 2, 2011
NIFANYE NINI ILI MUME WANGU AWE NA HAMU NAMI?
Mume wangu anasema ananipenda sana, nami nampenda sana. Tuna watoto wawili wa kiume. Nimejaribu kila kitu cha kumfurahisha, kama vile kuvaa vizuri, kuandaa chakula kizuri akipendacho na kinywaji lakini Lakini mwenzangu haonekani kuridhishwa na jitihada zangu.Baada ya chakula cha usiku huwa tunakaa na kuangalia Luninga huku tukiwa na vinywaji. Lakini cha ajabu nikimsogelea na kutaka niwe karibu naye ananiepuka. Yaani HATAKI hata nimguse ni kama NINANUKA au ninamsumbua vile.
Je, tatizo ni nini hasa, Je nanuka? Najiuliza na jibu sipati….Alimalizia kusema huyu mama huko chozi likimdondoka…......
Naam mara nyingi hivyo ndivyo inavyokuwa kwa sisi wanawake pale tukutanapo, si jambo geni sana kwa sisi wanawake kushirikiana kihisia. Ni jambo la kawaida kabisa kukuta mwanamke akimsimulia shoga yake anayemuamini juu ya madhila yake. Yote hiyo ni katika kutafuta nafuu na kuondokana na msongo wa mawazo.
Mara nyingi simulizi nyingi zinazowakutanisha wanawake ni zile zinazohusiana na mambo ya Ndoa, mahusiano, watoto au mambo ya kifamilia kwa ujumla, mara nyingi tunatamani kupata mahali pa kulinganishia, ili kutaka kujua kama tatizo nililo nalo lina ukubwa kiasi gani.
Ni hivi majuzi nikiwa kazini na mfanyakazi mwenzangu ndipo aliponieleza kile kinachomsibu kwa muda mrefu sasa, inavyoonekana, ni jambo ambalo alikaa nalo muda mrefu akijaribu kupambana nalo kimya kimya huku likiendelea kumtafuna, dada huyu wa Kiswidish.
Ili kujiridhisha na kutaka kujua ukweli halisi nikamuuliza kama amemuuliza mume wake jambo hili akajibu amefanya hivyo na jawabu alilolipata ni kwamba, mume wake huwa anachoka. Yaani kazi zake ni nyingi pia malezi ya watoto yanamchosha. Nikamuuliza kama hawawezi wakati wa wikiendi watoke ili kuwa peke yao? Hapo nikapata jibu ambalo sikutegemea. Alidai kwamba akisema hivyo mume wake anaona kama yeye anaamua nini wafanye.
Huyu mama akaendelea kusema, mimi ni binadamu Yasinta.,,,,,,,,,, Na nahitaji tendo la ndoa na sitaki kutoka nje kwani nampenda sana mume wangu. Nami sikuachia hapo kama mnavyonifahamu na u-Kapulya wangu nikamuuliza kama tatizo hilo lina muda gani au limeanza siku za karibuni?
Mama yule akashusha pumzi, akaniangalia kwa jicho la huzuni, kisha akajibu kuwa inatokea wanafanya tendo la ndoa mara moja kwa mwezi na hapo ni ile ya haraka haraka na halafu baada ya hapo mume wake anampa mgongo na kulala .
Hapo….akasita kidogo …nikamuuliza ulitaka kusema nini? Akaendelea unajua Yasinta mwanamke anahitaji kuandaliwa kwanza, mimi huwa siandaliwi kabisa........ Mweh! Nikaona makubwa haya ......nilikosa Jawabu la kumpa kwa kweli, nikabaki kuguna tu.
Hata hivyo nilijaribu kumshauri aende kwa washauri nasaha wa masuala ya Ndoa na mahusiano, lakini akadai kuwa mumewe ni mkaidi na hawezi kukubali.
Mwenzenu swala hili limenishinda maana sijui nimsaidieje! Je Wewe kama msomaji unaweza kunisaidia ni ushauri gani nimpe mama huyu, ili awe na furaha katika Maisha ya ndoa yake?
Ushauri tafadhali...........
Thursday, April 28, 2011
YALE TUYAITAYO MABAYA NDIYO HUTUFUNZA HEKIMA!!!
Ujumbe huu nimetumiwa na Dada Frida Magari wa FAJI. Nami sikutaka nifaidike peke yangu nimeona ni vema niuweke hapa kibarazani ili wengi tufaidike pia kujifunza. Ahsante sana dada Frida.
Wednesday, April 27, 2011
HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KWAKO DA´MIJA MWANAMKE WA SHOKA!!!

Napenda kukutakia siku yako ya kuzaliwa kheri na baraka tele. Mwenyezi Mungu na akulinde uwe salama pia uwe na afya njema siku zote. Na pia uwe bibi kizee ili uweze kucheza na wajukuu wako pia vijukuu. HONGERA SANA KWA SIKU YAKO HII TUKUFU KWA KUONGEZA LIMWAKA:-) UWE NA SIKU NZURI NA WALA USITHUBUTU KUTUNYIMA HIYO KEKI!!!
Zaidi unaweza kumwona mwanamke huyu wa shoka kwa kubonyeza Da´Mija.
Tuesday, April 26, 2011
KWA NINI IWE NI WANAUME TU WANAONUNUA MKUYATI?
Wanawake wana matarajio makubwa sana katika kila eneo linalohusu maisha yao, lakini linapokuja swala la tendo la ndoa mambo ni tofauti sana. Kwa kawaida wanawake wengi ambao hawaridhishwi na tendo la ndoa kwenye uhusiano wao huwa wanafanya siri.
Bila kujali kama tatizo liko kwao au kwa waume zao, wanawake hufanya siri kutoridhika kwao kimapenzi, na huweka siri kwa waume zao na hata kwa madaktari. Na ndio maana sishangai kuona kwamba wateja wa wauza dawa zinazohusiana na kuongeza hamu ya tendo la ndoa yaani Mkuyati ni wanaume.
Nilipokuwa nyumbani Tanzania, jijini Dar Es Salaamu nilishangaa sana kuona katika magazeti maarufu ya Udaku, {Tabloids} matangazo mengi ya biashara yanayotawala katika magazeti hayo ni ya kuuza dawa za kuongeza nguvu za kiume au hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume na nyingine zilikuwa ni za kuongeza ukubwa wa maumbile ya kiume, dawa kama Mkuyati, Mzakaru, Super Shaft, Kifaru, Sekwa na nyingine chungu nzima ni maarufu sana jijini Dar Es Salaam.
Sio kwamba wanawake hawana matatizo ya tendo la ndoa, la hasha. Wanawake wanayo matatizo hayo ya tendo la ndoa lakini kwao hiyo siyo agenda, yaani si kitu cha kuwaumiza sana kichwa. Lakini kwa wanaume ni tofauti sana, wanapokuwa na tatizo la kukosa ufanisi katika tendo la ndoa huo utakuwa ni mgogoro mkubwa sana, kwani kwao hili ni jambo linalopewa kipaumbele kuliko mambo yote.
Kwa wanaume kukimbilia hospitalini au kwa mganga wa jadi na kusema “nina tatizo kubwa” ni jambo la kawaida kabisa…. Lakini wanawake hawafanyi hivyo, Badala ya kulifanya tatizo hili ni mgogoro halisi, huwekwa chini kabisa kwenye orodha ya matatizo yao, huwekwa kiporo na litashughulikiwa kwa wakati atakapojisikia kufanya hivyo kwa wakati wake.
Wanawake wanaweza kwenda kuomba ushauri au kuwasimulia mashoga zao, kuhusu matatizo ya ndoa. Lakini ni hadi wachokozwe ndipo wanapoweza kusema kwamba maisha yao ya tendo la ndoa na waume zao hayako sawasawa. Hilo halipewi uzito wa juu au naweza pia kusema hufanywa siri.
Wanawake hawaridhishwi na tendo la ndoa kwa sababu mbali mbali. Lakini bila kujali sababu hizo, kwao ni vigumu sana kusema kuhusu kutoridhishwa kwao. Ukiona mwanamke anatangaza sana kuhusu kutoridhishwa kwake na tendo la ndoa, basi ujue huyo na mumewe wako kwenye uhusiano mbaya sana. Kwani atakuwa anatumia maelezo ya kutoridhika kwake kama adhabu ya kumkomoa mumewe kwa kumuaibisha.
Lakini wale walioko kwenye ndoa imara ni vigumu kuwasikia wakilalamika kwamba hawaridhiki na tendo la ndoa. Inawezekana kutoridhika kwake kunatokana na yeye mwenyewe, yaani labda hana hamu au hafiki kileleni kutokana na matatizo mbali mbali yakiwemo ya kisaikolojia au matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango, lakini bado sehemu kubwa wanaume huchangia. Hata hivyo pamoja na sababu hizo, mwanamke hayuko tayari kusema kuhusu kutoridhika kwake.
Kushindwa huko kunatokana na jinsi jamii ilivyomfunga mwanamke, kutoonesha kuhitaji tendo la ndoa. Akionesha kutoridhika na tendo la ndoa huonekana ni Malaya, kwa hiyo hukaa kimya na kuonesha kutojali.
Lakini bila shaka nadhani umefika muda wa wanawake kuwa huru kuhusu tendo la ndoa na kusema hisia zao wazi wazi bila kuogopa jamii itawaonaje, kwani jamii imekandamiza haki yao ya kuzungumzia tendo la ndoa kwa muda mrefu sasa.
Wanaume nao wanapaswa kujua kwamba wanawake hawapendi au hawawezi kuzungumzia kutoridhishwa kwao na tendo la ndoa, hivyo kutosema kwao kusitafsiriwe kuwa ndio wanawaridhisha, ni vyema kutoa ushirikiano kwa wake au wapenzi wao na kutafuta kujua kama wanawaridhisha. Ni jambo la busara kama mwanaume atadadisi kwa upendo na lugha ya upendo na kuonesha kama yuko tayari kutoa ushirikiano pale ambapo mke au mpenzi ataonesha kutoridhishwa na tendo la ndoa.
Mada hii nilikwisha wahi kuiweka hapa kibaraza , nimevutiwa nayo tena nikaona sio vibaya kuirejea ili kujikumbusha. Kama nisemavyo kila wakati kurudia kusoma kitu ndio kujifunza mengi.
Sunday, April 24, 2011
KHERI KWA SIKUKUU YA PASAKA KWA WOTE!!
BWANA AMEFUFUKA NA WOTE TUFURAHI LEO....KHERI SANA KWA PASAKA!!!
Saturday, April 23, 2011
KUMBUKUMBU:- LEO UMEFIKA MWEZI MMOJA TANGU ASIFIWE WETU ATUTOKE!!
Leo imetimia mwezi mmoja tangu Asifiwe wetu atutoke!Hapa china nilitumiwa barua pepa na kaka Raymond Mkandawile ujumbe huu ufuatao. Nami nimeupenda ni ujumbe mzuri na nimeona ni vizuri niuambatanishe hapa. Ahsante sana.Ujumbe wenyewe ni huu :-
Duania tu wapitaji na hakuna ajuaye siku yake ni lini. Hivyo hatuna budi kujiandaa na kuwa tayari kila itwapo leo.Dada yetu Asifiwe pumzika kwa amani na sisi pia tunafuta....bwana alitoa na yeye ametwaa jina lake libarikiwe.
Si vibaya kama tukisikiliza na nyimbo hizi ambazo Asifiwe alikuwa akisikiliza sana....
HALAFU HUU PIA ALIUPENDA PIA....
WOTE TWAJUA UMETUACHA KIMWILI LAKINI KIROHO UPO NASI NA TUTAKUKUMBUKA NA KUKUPENDA DAIMA!!!
Friday, April 22, 2011
IJUMAA KUU HII IWE NJEMA KWA WAUMINI WOTE!!
Ni ijumaa ambayo Bwana Yesu Kristu atapata mateso kwa ajili yetu. Sijui kama kuna mtu angeweza kujitoa roho yake kwa ajili ya mwingine kama Bwana wetu Yesu anavyofanya kwa ajili yetu?..Na nawaombeni usisahau leo ni ile siku ambayo ni siku moja tu kwa mwaka ambayo tunaombwa kuacha kula vyakula vya damudamu hasa nyama ....Mwenyezi
ungu na atawala Nyumbani mwenu. Amina. IJUMAA KUU IWE NJEMA KWA WOTE....
Thursday, April 21, 2011
HESHIMA KWA WANAWAKE
Kweli huu uungwana?Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote;
IMAGINE:
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa
anakusamehe halafu anasahau!!!
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye
anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni
kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia
chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila
manung'uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma
kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala
halalamiki!
CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna
maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena
inaweza tokea hii; hana kinyongo!
UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale
imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo
ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana
kashasahau na kukusamehe!
UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto
anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina
atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi
kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!
Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE,
WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!
HIVI INGEKUWA WANAUME TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?
Nimeipenda habari hii na nimeona niwahabarisha na wenzangu kwani elimu ni kuelimishana. habari hii imetoka Jamii Forum.
Wednesday, April 20, 2011
Kwa nini watu wanapima joto kwenye paji la uso??
Kwa vile joto haliwezi kupimwa sawasawa na mkono, kwa hiyo mbinu hii haitoshi. Hivi karibuni kumeanzishwa aina mpya checha za vipimajoto, ambavyo vitaweza kupima joto katika paji la uso. Katika utafiti inaonyesha kwamba joto la paji la uso linayumba na 1,5 C kutoka joto kamili la Mwili. Kwa maana hii njia hii sio nzuri.
Njia nzuri zaidi ni kupima joto makalioni. Pia sikioni au mdomoni. Lakini upungufu ni sawasawa. Ni muhimu/lazima kuongeza nusu C kwa kupata joto kamili.
Chanzo: Illustrerad Vetenskap nr 6/2011
Monday, April 18, 2011
WANAUME NA KAULI HIZI: 'HUYO SIO WA KUOA, NI WA KUCHEZEA TU'
Kwa kawaida vipimo vya uzuri wa mwanamke kwa wanaume vimegawanyika. Wanaume wengi hupima uzuri wa mwanamke kwa sura au umbo, lakini linapokuja swala la kuoa, suala la tabia na mwenendo hupewa nafasi kubwa.
Na ndio maana wakati mwingine unaweza kushangaa kukuta mwanaume ambaye ni hodari wa kuchagua wanawake wazuri, lakini ukija kumuona mke aliyemuoa, utakuta ni mbaya kwa sura na umbo, lakini kwa upande mwingine utakuta mke huyo ni mzuri katika maeneo mengine kama vile, tabia nzuri,upendo, wema, na anayemudu malezi ya watoto katika familia.
Sifa nyingine ni zile za kumkubali mwingine kirahisi, kuwa tayari kusaidia yanapojitokeza matatizo katika familia, mpenda amani na kumfanya mume wake aone kuwa hakukosea kumchagua yeye kuwa mke wake. Kwa kifupi wanawake wa aina hii hata kama wangekuwa ni wabaya kwa sura na umbo bado wako kwenye nafasi ya kuonekana kuwa ni wazuri, na huolewa kirahisi zaidi.
Wanawake wazuri kwa sura na umbo ambao tabia na mienendo yao hairidhishi wako kwenye nafasi kubwa ya kuishi bila kuolewa, na kwa bahati mbaya zaidi wanawake wengi wanaohesabika kuwa ni wazuri, tabia na mienendo yao ni ya kutilia mashaka. Wanaume wengi huvutiwa na wanawake hao kujenga uhusiano nao hasa wa kimwili tu na si vinginevyo, na ndio maana wanawake wazuri kwa sura na umbo wanalo soko kubwa sana kwa wanaume, lakini huishia kuchezewa zaidi kuliko kuolewa.
Wanaume nao kwa upande wao wamejenga dhana kwamba wanawake wazuri sana sio wa kuoa na hivyo kuwaogopa. Wanaamini kwamba wanawake wazuri sana ni wasumbufu, kitu ambacho kina ukweli kwa kiasi fulani. Wanaume wanaamini kwamba wanawake wazuri sana kwa sura na umbo huwasababishia waume zao maradhi ya moyo,shinikizo la damu na wakati mwingine hata kuwafanya kupata matatizo fulani ya kiakili, na hiyo inatokana na waume hao kuwa katika mashaka ya wake zao kuchukuliwa na wanaume wengine wakati wowote kutokana na uzuri wao. Hata hivyo wanawake wazuri nao huwaendesha waume zao wakijua kuwa ni wazuri na soko lao liko juu na waume zao nao huwanyenyekea wakihofia kuachwa.
Na ndio maana usishangae kuona kuwa wale wanawake ambao watu wamekuwa wakiamini kuwa ndio wabaya kwa sura au umbo lakini tabia na mienendo yao ni mizuri ndio wanaoolewa na hata ndoa zao zinadumu, tofauti na za wale wanaoonekana kuwa ni wazuri sana kwa sura na umbo na ambao tabia na mienendo yao si mizuri, ndoa zao hazina umri mrefu.
Sunday, April 17, 2011
PASAKA HIYOOO INAPIGA HODIIII:- LEO NI DOMINIKA YA MATAWI!!!
Friday, April 15, 2011
IJUMAA YA LEO: HEBU FIKIRIA MILO YETU HII YA ASILI, WANAODHARAU VYAKULA KAMA HIVI HAO WANA HASARA HASWA!!!
Na mchana ni ugali, samaki, mboga majani kidogo, mchuzi, maharagwe kinywaji maji. Mmmm!! yam yam yam!!utamu jamani ...karibuni tujumuike basi....
Jioni naona tubadili mboga, tutakula KISAMVU ..yaani hapa mimate hadi inanidondoka si mchezo ..karibuni sana jamani tufaidi uhondo huu... Picha hizi kutoka kwa kaka Mjengwa . IJUMAA NJEMA WANDUGU!!!
Thursday, April 14, 2011
AJALI YA RESTIELI
Kama mnakumbuka niliwahi kuweka ushuhuda wa binti mmoja aitwae Restieli Moses Mbwambo akieleza kisa chake cha kuungua na mafuta akiwa mdogo (ukitaka kujikumbusha waweza kubofya hapa). Juzi nimepata taarifa kuwa familia ya binti huyo akiwemo mwenyewe Restieli, walipata ajali katika maeneo ya Lembeni mkoani Kilimanjaro.
Ajali hiyo ilihusisha gari lao dogo aina ya Toyota RAV 4 waliyokuwa akisafiria kutoka Upareni kurejea Moshi hapo mnamo siku ya Jumanne ya tarehe 5/04/2011. Ajali hiyo ilitokea baada ya tairi la mbele la gari hilo kupasuka na hivyo kupinduka mara kadhaa. Habari nilizozipata ni kwamba wote walisalimika katika ajali hiyo isipokuwa walipata majeraha kadhaa mwilini ambapo walitibiwa na kuruhusiwa.
Mleta habari amebainisha kwamba kutokana na ajali hiyo gari lao limeharibika vibaya, na ukiliangalia hutaamini kama waliokuwa ndani ya gari hilo wote wamepona.
Blog ya Maisha na Mafanikio inapenda kuchukua nafasi hii kuwapa pole wote walionusurika katika ajali hiyo, na ninaamini Mungu ataendelea kuwalinda.
Wednesday, April 13, 2011
Tafakari ya leo:- Umpendaye ndiye?
Monday, April 11, 2011
MWENZENU NIMEGUNDUA KUWA!!!!!...............

Tembo wa afrika wana masikio makubwa na pembe kubwa.

Masikio yao yanafanana na Ramani yetu ya Afrika!!

Tembo wa India wana masikio madogo na pembe ndogo.

Pia masikio yao yanafanana na Ramani ya India .
Je Uligundua hili wewe pia??
Sunday, April 10, 2011
NAPENDA KUWATAKIA WOTE JUMAPILI NJEMA KWA UJUMBE HUU
Macho ya huruma hufurahisha moyo, habari huburudisha mwili. Kuchukiana huendekeza fitina, kupendana husitiri makosa yote. Nilikuwa mgonjwa ukaja kuniona .Nilikuwa na njaa ukanilisha. Kumhudumia mgonjwa ni wito. Jumapili njema jamani:-) ngoja tusikilize wimbo huu kuhusu Afrika yetu .
Muwe salama wote na kumbukeni wote mnapendwa!!!
Saturday, April 9, 2011
Nimekumbuka enzi zangu? Je? Unaweza kugundua nimesimama wapi?
Friday, April 8, 2011
MAJINA YETU/LEO TUANGALIE MAJINA YA KISUKUMA!!!
Thursday, April 7, 2011
Tuesday, April 5, 2011
NIMEMKUMBUKA KWELI MDOGO WANGU ASIFIWE LEO
Asifiwe! Asifiwe! sauti zetu sikia,
Asifiwe! Asifiwe! kweli unatusikia?
Asifiwe! Asifiwe! mbona hujaitikia?
Asifiwe umekwenda, dunia 'meikimbia,
Wajua tulikupenda, ila Mungu kazidia,
Mauti yamekutenda, wewe umetangulia,
Pumzika kwa amani, Asifiwe Ngonyani.
Umetwachia majonzi, hakika twakulilia,
Tumejawa na simanzi, hatuwezi elezea,
Mdogo wetu mpenzi, uchungu 'metuachia,
Pumzika kwa amani, Asifiwe Ngonyani.
Ulijawa na adabu, nao ukarimu pia,
Kwa wako utaratibu, ni nuru imepotea,
Umekwenda kama bubu, kwa heri hukutwambia,
Pumzika kwa amani, Asifiwe Ngonyani.
Wewe mtu mwuungwana, kwa njema yako tabia,
Tulikupenda kwa sana, nd'o maana twaumia,
Mfano wako hakuna, kwa pengo kulizibia,
Pumzika kwa amani, Asifiwe Ngonyani.
Kuondoka kwatuliza, kila tukifikiria,
Twatamani tungeweza, kifo tungekizuia,
Mwaka huu kumaliza, nayo inayof'atia,
Pumzika kwa amani, Asifiwe Ngonyani.
Lakini sisi ni nani, Mungu tukamwamulia?
Tukamwuliza kwa nini, wewe amekuchukua?
Mwamuzi ndiye Manani, aloiumba dunia,
Pumzika kwa amani, Asifiwe Ngonyani.
Pengo halitozibika, wewe ulotuachia,
Daima 'takukumbuka, wema'wo kusimulia,
Tukimwomba Rabuka, mwanga kukuangazia,
Pumzika kwa amani, Asifiwe Ngonyani.
Upumzike salama, kwa Mola twakuombea,
Akupe pahala pema, nuru kukuangazia,
Asifiwe mtu mwema, buriani twakwambia,
Pumzika kwa amani, Asifiwe Ngonyani.
Shairi hili nimeliandika maalumu kwa marehemu Asifiwe Ngonyani, mdogo wa kike wa dada yetu, rafiki yetu na mwanablog mwenzetu Yasinta Ngonyani. Asifiwe alipatwa na mauti Jumatano 23.03.2011. Asifiwe umetuacha kimwili tu, kiroho tungali pamoja nawe. Tunakuombea pumziko salama la milele. Amina. AHSANTE SANA MTANI FADHY KWA SHAIRI HILI!!
Sunday, April 3, 2011
HEBU SIKILIZA HAPA JINSI WALIVYOJUA KUIGIZA...KAAZI KWELIKWELI
Muda mrefu nimekuwa mkimya bila kusikiliza miziki kwa ajiliya machungu yaliyonipata katika upekuzi wangu nimekutana nao hau kwa kweli wamenifanya nitabasamu kiduchu.. sijui nanyi wenzangu mtajiunga nami???






