Wednesday, April 13, 2011

Tafakari ya leo:- Umpendaye ndiye?

Moyo wa mtu ni kichaka na watamanianao huonekana wengi bali wapendanao ni wachache na hawajulikani. Hebu fikiria leo Mungu akisema kila moja asimame na ampendaye Je? Wewe utasimama na nani? Na huyu umdhaniaye ukimkuta amesimama na ampendaye utafanyaje? Haaaaaa…..!! Unacheka?

20 comments:

Unknown said...

Kaaaazi kweli kweli patakuwa hapatoshi apo.Mimi nitasimama na uyu uyu nimpendaye sasa.

Goodman Manyanya Phiri said...

Wapendanao kweli ni dhahabu. Ufunguo waPOST yako ya leo nimeupata pale unaposema: "...Wapendanao wachache na hawajulikani" kwani mara nyingi wanaokupenda unawagundua ukiwa katika shida tu na siyo penye raha au vicheko vya hovyo.

Upendo au mapenzi ya ukweli ni zawadi yaMwenyezi peke yake.

Asante sana kwa mawazo ya leo, NaNgonyani!

Mwanasosholojia said...

Ni kweli,maana siri ya mtu anaijua mwenyewe moyoni mwake.Na kwa tabia ya mwanadamu inawezekana anachokitamka sicho anachokimaanisha!Lakini suala linabaki palepale, lazima kuna mtu "anayemzimikia" vilivyo, sasa tuombe tu itokee wawe "wanazimikiana" ili wasimame pamoja...ikiwa tofauti...hapo ndo tutakapoona "unayemzimikia" kasimama na mwingine "anayemzimikia" na hata wewe kaja kusimama na wewe mwingine tena "anayekuzimikia" ambaye hata hukuwa unamtarajia!teh!teh!

nyahbingi worrior. said...

Je,wewe Da Yasinta ungesimama na nani?

Koero Mkundi said...

Mimi ningesimama na Fadhy kwa masaa kadhaa halafu ningehamia kwa Markus Mpangala kisha kwa Kitururu, halafu kwa.........

Yasinta Ngonyani said...

nyahbingi worrior! mimi nitasimama na yule nimpendae kwa dhati na pia anipendae kwa dhati!!

Fadhy Mtanga said...

...bora mie nimewekwa wa kwanza

Unknown said...

Ndipo hapo patashika itakapokolea.

Sipati picha hali itakuwaje ikitokea hivyo, maana!!!! Mh...!?

Sasa hivi tutajitutumua kujibu ila kiukweli siku hiyo Mungu asimamie kwa dhati kuwa ni wanaopendana na sio waliozoeana...utata.

Raymond Mkandawile said...

Nimeipenda sana hii dada Yasinta,good thinking and big up kwa sana...

Anonymous said...

KUPENDA NI KITUKIDOGO SANA,KATIKA MAISHA YA BINAADAMU,HASA KATIKA KITU KINACHO ITWA MAHUSANO IWE MUME NA MKE AU HATA UHSIANO KIMAPENZI KABLA YA KUAMUA KUOWANA.LA MUHIMU HAPA KWA MTAZAMO WANGU NI UNAPOAMUA KUMKUBALI, MUME/MKE KWA MAISHA HAPO NDO PATAMU,KUMKUBALI MTU NIZAIDI YA KUPENDA,WAWEZA KUPENDA EMBE,KIATU NCHI,HALAFU UKABADILISHA MAWAZO KUWA HUKIPENDI TENA HICHOKIATU HIVYO HUKINUNUI TENA. HAYA NIMAWAZO TU.KAKA S

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

ntasimama mwenyewe!...lol!

ADELA KAVISHE said...

kupendana katika shida na raha ndiyo mpango mzima jamani angalia mtu anayekupenda kuwa makini usijikute mikononi mwa asiyekupenda au usiyempenda raha ya mapenzi mpendane tena kwa mapenzi ya dhati uaminifu na uwazi ue nguzo yenu.

Rachel Siwa said...

Duhh nikutata amesisi na ampendaye ambaye si mimi?Mungu nisaidie!!

Naungana na :dada Sarah Gau Goloka miyeeeeeee hapahapa tuu

Anonymous said...

Itakuwa sawa tu kwani hata mie atakuwepo tu ambaye ananipenda lakini akakuta nimesimama na mwingine,hivyo maumivi yatakuwa pande zote kwangu na kwa yule nisiyempenda. Ndo hivo lakini "LIFE IS KNIFE WHICH CUTS LIFE"

Poa wana blog.

Salehe Msanda said...

Ni kweli wengi tunachanganya kati ya kupenda na kutamani

Ni hatari lakini ndo hali ilivyo.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante wote kwa kutafakari tafakari hii pamoja nami...Mt. Simon mbona unaguna vipi?

Simon Kitururu said...

@Yasinta: Namuwaza nimpendaye na natafakari kwanini Koero anafikiria Fadhy na Markus watamuachia kirahisi ili nami nijilievyangu kiulaini zamu yangu ikifika!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Mt.Simon Koreo labda ameona akisimama na Fadhy kidogo kisha Markus laki wewe ndiyo mwenyewe tusibiri labda atatujibu.. ni wazo langu tu. lakini inaonekana tayari una umpendaye na unamfikiria kwa hiyo itabidi mdogo wangu Koero labda abadili mawazo.....

MARKUS MPANGALA said...

@ Dada Yasinta: Kwa hakika hili ni fumbo kama lile la KILA MTU, MTU, MTU na HAKUNA MTU. Ninakumbuka pia ile dhana ya “Siyo kila anayekuchekea anakupenda”, kwasababu tayari umetueleza hawajulikani. Na mioyo ya watu inamengi, yenye harara kuyajua. Lakini umpendaye ndiye lakini si kila mtu siye, na ndiye hawezi kuwa yeye bali mwingine naye ni yeye. Ni wazo tu hili wala usifikirie sana, ni katika kuwasha taa ya upendo moyoni mwangu……
@Koero, kumbe una ujua raha ya kuwekwa mtu kati, maana mie nikiwa katikati inakuwa swadakta yaani nakaba kila kona yaani nitakukaba hadi harufu yako… Lol……. Mjini hapa ukizubaa wanamega…… bora kukaba hadi harufu…… dakika 90
@ Mtani umenichekesha, wewe umewekwa wa kwanza kwasababu ya FASTA FASTA tu ha ha ha ha hakuna sauti za mitaa na ile miguno ya mioyo na upumuaji wenye kasi kama Usain Bolt au Mbwana Samatta…. Ha ha ha ha ha yaani wa kwanza mweeeeeeeeee hata harufu ya upendo tu inakutosha lakini ikihamia kwangu, nakaba kweli kweli hadi harufu halafu namwachia Kitururu kulee akalalamikiwe aaaaahh nimechokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, niache nipumzikeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ha ha ha ha ha ha ha ha!!! Jamani mweeeeee niache nipumzikeeeeeeeeeeeeeeeeeeee yaani mtakatifu anapata mabaki ya mioyo ya upendo………………. Lol…

@ mtakatifu a.k.a mtaka-TIFU unamuwaza unayemmezea mate Koero?? ha ha ha ha jiulize kwanini mimi wa kati kisha kuna HALAFU KWA......

Simon Kitururu said...

@Mkuu Markus: Yani eti mie niko mwisho yani!


Mie naanza kuhisi wewe na Fadhy mmeenda kumnywea KIKOMBE kwa BABU loliondo KOERO ! Kikombe cha MAPENZI! Ndio maana ni mpaka nyie mchoke ndio namimi nifaidi!

Ngojea niendelee kuwaza !

Yani KOERO roho inaniuma kweli!:-(