Saturday, April 9, 2011

Nimekumbuka enzi zangu? Je? Unaweza kugundua nimesimama wapi?

Natumai wakumbuka enzi hizi lakini waweza kunikumbusha mimi nimesimama wapi katika picha hii manake nilikuwepo teeeeh teeeeehhhh,...kaaazi kwelikweli

13 comments:

Mwanasosholojia said...

Teh!teh!teh!Kweli kazi da'Yasinta,naona kama haka ka-pili kulia kanashabihiana na haiba yako ulipokuwa mtoto...teh!ndo wewe nini?

Anonymous said...

Wewe naona ndiye uliyeshika hiyo fimbo au macho yangu hayaoni vizuri??

Baraka Chibiriti said...

Dada Yangu....hapo haupo, acha usanii, ha ha ha haaaa....!!!!!! Nimecheka sana, asante!

Simon Kitururu said...

Kuna mambo mengine kikisia zangu nahisi sio vizuri kuyafanyia utani!:-(

Na Posti hii nahisi wahusika kikweli kama wanahisi kama mimi kuna utani kwenye mambo ambayo sio utani ya mpaka ya utapia MLO ,...
.. labda posti hii haina teh the, LOL au hata :-)-hasa kwa kuwa ,...
Hivi kichekeshaco kwenye picha hiyo hasa ni kipi?

Nawaza tu kwa sauti!:-(

Simon Kitururu said...

Kuna mambo mengine kihisia zangu nahisi sio vizuri kuyafanyia utani!:-(

Na huu ni UTANI nahisi ambao sio lazima una ULAZIMA kuwepo leo!:-(



Na Posti hii nahisi wahusika kikweli kama wanahisi kama mimi kuwa kuna utani kwenye mambo ambayo sio utani ya mpaka ya utapia MLO ,...
.. labda posti hii haina teh teh, LOL au hata :-)



....-hasa kwa kuwa ,...
Hivi kichekeshaco kwenye picha hiyo hasa ni kipi?

Nawaza tu kwa sauti!:-(

Nimerudia komenti kwa kuwa wadau ambao niko nao wamekuwa ofendedi kama mimi walipoona hii posti kiaina.

Ni hilo tu!:-(

Raymond Mkandawile said...

Hahahahaha......Inapendeza sana kuwa na kumbukumbu kama hiyo japo sijakutambua wewe pale,do me a fever and identfy yourself please?

EDNA said...

Hahahaa haka kapicha kamenifurahisha sana.Lakini mbona wewe sikuoni? Upo kweli hapo?

Anonymous said...

asante kwa picha hawa watoto wanaonekana wana afya lakini wamekosa nguo na usafi tu

Mbele said...

Dada Yasinta, hii imenikumbusha utoto wangu. Baada ya timu kukamilika namna hii, ilikuwa sasa akipita panzi hapo kwenye anga zetu ni kumfukuza kwa mawe na hizo fimbo hadi kutokomea naye maporini :-)

PASSION4FASHION.TZ said...

Minaomba tukupe ka mji......Songea, nimejaribu kuangalia kwa mbali nimeshindwa kukutambua hata nilipojaribu kuivuta picha na kuikuza bado nimeshindwa kukugundua,hivi kweli wewe upo kwenye hiyo picha?

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote! mimi nipo hapo nyuma ukiangalia vizuri utaona naonekana kasura kwa mbali nilikuwa naogopa kamera:-)

Anonymous said...

Uongo huo, hii picha ya kwetu tuliipiga pale Msalato Dodoma mwaka 1989. Mimi niko ni wa pili kushoto.

Anonymous said...

Hongera kwa kutunza kumbukumbu, la hasha kwa kutafuta kumbukumbu. Kuna watoto sasa hivi hawawezi kulikubali hili, kama ambavyo hawawajui chawa wala kupe. Wewe hapo hupo, na kama kweli upo, basi ni yule aliye nafuu kimavazi kuliko wote. Una utani mbaya teeeeehee