Tuesday, March 8, 2016

PALE WATOTO WANAPOSHIRIKI KAZI KAMA HIZI.....

Hapa tunaona jinsi watoto hawa wannavyobeba matofari  na kupanga  tanuru la matofari. Je? hapa ni kujifunza kazi au ajira mbaya kwa watoto. Maana nina uhakika kwa umri wao ilibidi wawe darasani.Au unafikiri labda ni kazi tu za ziada baada ya shule kujitafutia pesa za kununua daftari na kalamu? ..mmmhh Kweli watu tumetoka mbali....
Mtoto huyo na jembe begani, hii imenikumbusha mbali sana...maana nilikuwa nikitoka tu shuleni najificha kukwepa kwenda shambani kupalilia viazi (mbatata):-) Naona nisiseme sana... TUPO PAMOJA...KILA LA KHERI!

3 comments:

ray njau said...

Haifurashi na wala haitii moyo kabisa!!

William Mwingira said...

Ni vizuri kufundisha watoto kazi lakini zisiwe kazi ngumu sana tofauti na umri wao, na pia zisiathiri ratiba zao za masomo,mazingira mengi ya kwetu yanahitaji sana kuwajenga watoto kifikra wajitume na kupenda kufanya kazi. Haifai kumlea mtoto kama yai.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Ni kweli haifurahishi wala kutia moyo kabisa...ila naweza kusema kuna kipimo chake cha kuwapa watoto kazi kama hizo.

Kaka Mwingira! Kwanza napenda kukukaribisha katika kibaraza hiki KARIBU SANA. Nakubaliana nawe ni kweli inabidi ratiba za shule zifuatwe kwanza... Na kama nilivyo sema hapo juu kazi za Aina hiyo inabidi ziwe na kipimo chake...