Wednesday, May 28, 2014

UMOJA NI NGUVU !!!

 Ni raha pale wote mnaposaidiana kazi  sio kumwachia mmoja tu. Hapa akina mama na watoto wanamenya karanga ingawa wengine wanapeleka mdomoni lakini wamejumuika kuifanya kazi...inavyoonekana ni karanga kwa ajili ya mbegu au labda kuunga mboga....Raha sana kushirikiana.....
....na hapa vijana hawapo nyumba wanasaidia kazi za nyumbani hapa wanakoboa mahindi. Wananikumbusha enzi hizi tulivyokuwa tukikoboa mahindi au kutwanga mihogo na kaka zangu. Nani anasema kazi ya kutwanga au kukoboa ni ya akina dada/mama tu?  Nimependa sana hii Je na wewe umependa?:-)

3 comments:

Rachel Siwa said...

Inapendeza kwa kweliii...

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki! Ni kweli kabisa nimekumbuka sana enzi zileeeee......

sara Chitunda said...

Hata mimi nimeipenda sana inanikumbusha mbali kwani nimezifanya sana kazi hizo