Friday, May 23, 2014

VYAKULA NILIVYOTAMANI IJUMAA YA LEO.....SAMBUSA NA EMBE!!!


Leo nimetamani kweli SAMBUSA kitu ambacho kinachosha ni kwamba nimewahi kujaribu kutengeneza na sikuweza kama inavyotakiwa na huchukua muda mwiiiingi sana. Sijui kuna njia rahisi zaidi? Halafu......

.....nikajikuta naota ndoto ya hili tunda EMBE...Songea ndo zinakwisha kwisha sasa....Kaaaazi kwelikweli ngoja niache kuota .....IJUMAA NA MWISHO MWEMA WA JUMA!!

4 comments:

Anonymous said...

Da Yasinta, kuna mikate ya sambusa readymade, sijui kwenu kama inapatikana, inakua imekupunguzia kazi ya kutengeneza mkate wake. Mi nasubiria zawadi yangu ya maboga au hata sambusa zinafaa! By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu Ahsante kwa ushauri nitajaribu:-) Nadhani hii zawadi ya maboga itabidi usubiri sana labda tuchukue sambusa:-)

Manka said...

Jamani Dada yangu nimekumisi kweli.Natamani Sana nikutumie hizo sambusa na embe nipo nyumbani.

Yasinta Ngonyani said...

Nimekumiss pia Manka! Sasa ww kunitamanisha hivyo kweli:-) uwe na wakati mzuri sana...