Ukiwa mpekuzi  utakutana na mengi. Leo katika pita pita kwa majirani zangu nimekutana na hiii kutoka DinaMarios.blogspot.com -- Haya niliyapata  kutoka kwa mshauri wa masuala ya mahusiano, ndoa na vijana Frederick  Kyara. Hizi ni baadhi tu nakuwekea hapa japo kuna vitu pia wanawake  hawavipendi kutoka kwa wenzi wao wanaume. 
NAYO NI HAYA HAPA UNGANA NAMI KUJADILI JAMBO HILI ambalo kwangu nimeona ni changamoto au niseme sikujua.
1. Wanaume hawapendi kuambiwa cha kufanya na wenzi  waoMwanamke unapotaka mwanaume afanye jambo usimwambie  alifanye bali fanya kama una mpa ushauri.Kwamba John hivi kwa nini tusiweke  balbu hapa kwenye korido maana kuna giza kweli. Badala ya hivi wewe John huoni  hapa kwenye korido kuna giza balbu imeungua mwezi sasa hujabadilisha kwa nini?  Weka balbu bwana. Atafanya au asifanye kabisa kwa sababu umemwambia cha  kufanya.
2. Wanaume hawapendi mwenzi mwenye  makelele, mlalamishi
Yeye ni kulalamika kuanzia Jumatatu  hadi Jumapili. Japo wanawake nao wanasema kuna wanaume walalamishii balaaa. Na  wenye gubu wanasusa kula mpaka kuongea wanawanunia wake zao  mmmmh!
3. Wanaume hawapendi mwenzi  mchafu
Mchafu wa mwili wake na hata nyumbani kwenye suala  la kutunza nyumba wanayoishi. Uchafu hufanya mwanamke apoteze  mvuto.
4. Wanaume hawapendi mwenzi  mbishi
Japo na wanawake wanasema wanaume ndio wabishi  zaidi. Utampa mwanaume  ushauri lakini haufanyii kazi ubishi  mwingi.
5. Wanaume hawapendi kuamrishwa na mwenzi  wao
Mwenzi mbabe anaetoa amri na  kumtawala  hawataki.
6. Wanaume hawapendi kuhisiwa  hisiwa na kusachiwa sachiwa
Kumpekua kwenye simu,  mifuko ya suruali kwamba unamulika mwizi. Hawapendi, tena pengine hawajafanya  jambo la kuwafanya wahisiwe vibaya.
 
 
No comments:
Post a Comment