Sunday, May 4, 2014

JUMAPILI YA LEO NIMETAMANI KWELIKWELI DAGAA WA ZIWA NYASA...NYUMBANI LUNDO

LUNDO:- Nimekumbuka sana leo, ugali wa mhogo, dagaa, kisamvu, matembele(mbwaka) bila kusahau samaki wa aina mbalimbali ndicho chakula kilichonikuza. Dagaa hawa ni watamu zaidi pale uwapatapo tu  yaani wabichi ..hasa lile wanaota (lighanda) ikiwa na maana zilizochomshwa na kukaushwa maji yote  usisahau chumvi na kapilipili kwa mbaliiii....Duh! najitesa bure hapa ngoje niache ila nitazile muda si mrefu Mungu akipenda:-)  JUMAPILI NJEMA!

2 comments:

Anonymous said...

Jamani, nimekosa neno. Wacha nijinyamazie! By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu...ahsante kusema neno:-)