Monday, September 9, 2013

PALE INAPOFIKIA MSIMU WA BUSTANI KUVUNA/KWISHAKWISHA KWANI MSIMU WA BARIDI UNAKARIBIA SASA

 Hapa ni maboga yanakaribiwa kuwa makubwa na tayari kwa kuliwa..kwa uzowefu wangu inabidi yawe na rangi ya njano kidogo ili kujua yamekoma ..ila sijui ni kweli naomba ushauri wenu....
 Hapa ni mboga ya maboga mnaona inakaribia kufa/ kwisha ila nimekula sana na akiba nimeweka kwa hiyo karibuni sana .
 Nyaya ndo bado, zinaendelea kuiva  kila siku ila nasikitika  sina sehemu ya kuzihifadhi hapo baridi itakapozidi
 Mchicha nao umechokachoka na pia umeanza kuchanua na hapo ndipo nitakapopata mbegu za mwakani ila sijui kama zitawahi kukauka...Je naweza kuzitoa kabla ya kukauka na kuhifadhi sehemu ..akina bwana shamba na wataalamu naomba ushauri....
 Na hapa ni ile figiri niliyowaambia nitapanda nyingine imekuwa kufikia hapa. Ni kwamba natumia ujanja wa kufunika na kitambaa fulani chembesi sana ili wale viwavi jeshi wasile na naona inakuwa vizuri. Kwa figiri huwa inavumilia sana baridi maana hizi mbegu nimepata Njombe na baridi ya Njombe ni sawa na hapa mwanzono mwanzoni....
 Kapulya si mpenzi wa kulima bustani za mboga tu ni mpenzi wa bustani wa maua na maua ya kupanda kwenye makopo...Ua hili huwa linanikumbusha shule nyingi za msingi na secondary nyumbani Tanzania.

Hapa pia ni ua ambalo nimelitunza na limenipita hadi urefu mimi mwenyewe ..mnaona kazi hiyo...hapa huwa nakaa na kutafakari mengiiiii nikiliangalia hili ua.
HAYA NAWATAKIENI WOTE JUMATATU IWE NJEMA NA PIA WOTE MNAPENDWA...KAPULYA WENU

11 comments:

Anonymous said...

Da Kapulya, kweli wewe ni mtoto wa mkulima! Sasa hayo maua ya mwisho ni mauaridi au? Hizo tomato labda unaweza kuziweka kwenye friza sina uhakika. Hongera kwa kupata dawa ya figiri! By Salumu.

sam mbogo said...

Hongera sana dada yasinta mboga za majani ni muhimu sana kwa afya zetu. natamani ningekuwa karibu ningesaidia sana kupunguza hizo mboga za ziada. hapa kwangu mamaa ndo mtu wakulimalima vi mboga mboga,sasa hivi nasi tumevuna sana nyanya, na mboga za majani kdogo hasa maharagwe/ maharage. msimu wa barido/baridi unaanza,kwa hakika napenda hali hii ya barido/baridi naisubiri kwa hamu. haya nakutakia siku njema wewe na familia yako.kaka s.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salum Ahsante ...Hilo ua la mwisho laitwa Geranium...ni nzuri na nalipenda..Nikiweka kwenye friza hizo nyanya naona kama zitaharibika maana zitaganda mno...ila ahsante kwa ushauri

Kaka Sam..ahsante...mbona hapa si mbali njoo tu yaani utafaidi kweli na ntakufungia vifurushi. Ww kaka ww unapenda baridi??? haya bwana..Hongera nanyi kwa kuvuna minyanya mingiiii.

Rachel Siwa said...

haya nitawahi hapo kabla hayo Maboga hamjavua..Honngera sana KADALA wa mimi..

Kaka Sam Mwana wa mbogo na Wifi wachoyo kumbe nyie jamaniii.. Yaani hata majirani hamtukaribishi kuchuma mboga?
Haya sawa nami nimepanda, maua yangu ya saa 4..msiombe.

Interestedtips said...

hongera sana dada, kazi nzuri, mbegu za mchicha ziache hadi zikomae ili mwakani ukipanda ziweze kuota vizuri, hilo ua mlangoni limenikumbusha pia nyumbani Tabora mama kayapanda kwa wingii

Bennet said...

Ngoja nije na kikapu changu nikusaidie kuvuna, ni kweli maboga kuwa ya njano ni dalili ya kukomaa lakini hata yakiwa machanga hayana tatizo kuyala ila kinachopungua ni virutubisho tu

ray njau said...

Nahisi kuwa wewe unastahili kuwa mkulima stadi na mwenye sifa zote njema.Hongera sana mkulima wetu na pongezi zako pokea.Hakika uvivu ni mtu kuamua mwenyewe tu kuwa mvivu.

Penina Simon said...

Aisee hadi raha hayo maboga na nyanya duh i cant figure out

Anonymous said...

Inaonekana wakati wa kukutembelea ni huu...napitwa na mazuri! hoppas ni mår väl :) Kramar!

Mija Shija Sayi said...

Hahahaaa SerinaSerina unaona mbali, umenifurahisha na comment yako..lol!!

Yasinta hiyo nyumba mbona safi hivyo??..hadi raha!!

Yasinta Ngonyani said...

Kachika wewe njoo yaani karibu sana sana tena utakuwa mpishi!
Esta! Ahsante ..na ahsante kwa ushauri

KJaka Bennet! Njoo hata na makapiu mawili...Nitajitahidi mwaka kuwekla virutubisho..Ahsante

Kaka Ray ..zimepokelwa kwa mikono miwili huku magoti yametua sakafuni...
Dada P..yaaani ni raha juu ya raha:-)
Serina ndugu wangu duh! umepotea kweli ww karibu uje kunisaidia na kusafisha shamba kwa ajili ya mwakani...Vi mår bara bra..Kramar tillbaka
Dada mkuu msaidizi wa mimi Mija! ahsante alo basi karibu siku moja tutakaa hapo na kunywa chai:-)