Tuesday, August 13, 2013

NILICHOKUTANA NACHO ASUBUHI YA LEO WAKATI NAFANYA MAZOEZI YANGU YA KUKIMBIA......ADUI KA/NYOKA!!!!

Nimekimbia nimekimbia mchaka mchaka ,chinja, mchaka mchaka chinja, alimselma Hadijax2...Bahati mbaya nzuri macho yalikuwa yakiangalia chini ..weweeeee nilipoona hako kanyoka niliruka sikumbuki hatua ngapi utadhani wale wanariadha wanapokimbia na kuruka . Ni kadogo lakini nyoka ni nyoka tu....nikasimama nikuchukua picha hii, kwanza nikakarushia aina ya jiwe, halafu hiyo fimbo muionayo kimya kusogea karibu ...kumbe amekufa. Nilikasema moyoni duh! nilikuwa na bahati sana maana siwapendi nyoka.UJUMBE WANGU:- Tuwe waangalifu tunapokuwa tukitembea na hasa mstuni na hata barabarani.

5 comments:

ray njau said...

WANAVYOSABABISHA MAAFA: Nyoka wana kasi sana na sehemu yoyote katika mwili wa binadamu inaweza kuwa kugongwa na kiumbe huyo hatari.Lakini ni hatari zaidi nyoka anapomgonga mtu kwenye mshipa wa damu kwani hiyo huharakisha kusambaa kwa sumu ya kiumbe huyo.Nyoka hutumia sumu yao kumlegeza mtu na pengine kumpotezea fahamu.Majoka makubwa kama Mfalme Kobra (King Cobra) yanaweza kusimama hadi usawa wa kichwa cha binadamu,huku wengine wakiweza kutema na kurusha sumu yao kutoka mbali kwenda kwenye macho ya mwanadamu.

JINSI YA KUWAKWEPA: Mara nyingi nyingi nyoka hushambulia pale tu pale anapobughudhiwa.Kwahiyo ushauri muhimu wa kuepuka shambulizi kutoka kwa viumbe hao ni kujiepusha nao (Stay away!).Pia ni muhimu kuvaa mabuti kwenye mazingira yanayoweza kuwa na nyoka.Epuka mapori yanayoweza kuwa makazi ya nyoka.Na ikitokea umeomwona nyoka,inashauriwa urudi kinyumenyume taratibu kwani anaweza kujirusha mara nusu ya urefu wake,na mtikisiko kidogo tu unaweza kumasha hasira za kiumbe huyo hatari.

mumyhery said...

Pole sana

Penina Simon said...

Yasinta unanipa raha!!! Uliipiga picha kbs?

Unknown said...

Pole Da yasinta na kwel nyoka n nyoka tu hata km mdg.

Anonymous said...

Mungu ni mwema alikuwa amekufa na uliomwona mapema. Mungu anakupenda. Ila naona summer hii imekuwa na kajua jua kakali hivyo imeibua wadudu/ wanyama wengi wengi. Hivi kungekuwa hakuna winter ulaya nao wangekuwa na matatizo mengi kama vile nyoka, mbu, mchwa, viwavi jeshi, inzi nk. kwa sababu ya winter viumbe hivyi havistahimili baridi kali na snow hivyo vinawajibika kufa au kutokuwepo kabisa! Hiyo ndio raha ya ulaya sio kama kwetu joto kali linaandamana na mbu weengi, inzi, nk. Mungu atupe ka winter kidogo Tz ili tuondokane na mbu angalau. Si mnaona wakati wa summer huku ulaya kunakuwa na mbu pia, ila hawana malaria, inzi pia ingawaje sio weeengi kama kwetu ila wapo. Mh kwetu ni pazuri Tz nimeishapakumbuka. Siku njema Yasinta.