Monday, August 26, 2013

HUU NI MCHANA MWINGINE YA JUMATATU .....KARIBU TUJUMUIKE HAPA JAMANI....

Picha hii imenikumbusha mbali sana huu ni mtindo mzuru sana kula hivi sahani moja ....Ila kuna kitu kimoja kilikuwa kinanishinda hapa nilikuwa nakula taratibu mno na ninaposhtuka ugani umeisha. Ni mtindo mzuri maana hapo ndipo wote mnaweza kukusanyika na kuongea pia ila si sana maaana kila mtu anakuwa hana nafasi ya kuongea.....isipokuwa kushiba....Je nawe msomaji unakumbuka hii?
JUMATATU NJEMA!!!!

4 comments:

ray njau said...

Hii inanikumbusha zama hizo zisizoweza kujirudia tena kwa wajukuu kukutana uwanjani kwa babu na bibi na palikuwa hapatoshi.

Anonymous said...

Kula sahani moja na wenzio ina raha zake. Siku hizi maisha yamebadilika sana, wengi wanapenda kula kila mtu na sahani yake. By Salumu.

Penina Simon said...

Dah hapa ugali unakuwa mtamu ajabu, sababu mnakula kwa kunyanganyana

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! nakwambia hii ndiyo ilikuwa zamani na naitamani zamani yangu...ndo maana hadithi nyingiu tulizosimuliwa bado twakumbuka.

Kaka Salumu! Watanzania tunapenda sana kuiga tunaacha utamaduni wetu na kufuata ya wengine hata kama si tamaduni nzuri twende tu...
Dada P! yaani kama vile tulikuwa tukiishi nyumba moja ......